Monday, June 2, 2014

MGOMO BARIDI WA USAFIRI DAR ES SALAAM BAADA YA DALADALA KUZUIWA KUTUMIA KITUO CHA MWENGE NA KUTUMIA CHA MAKUMBUSHO

 Abiria wakiwa wanashangaa Daladala zinapita kituo cha Mwenge jijini Dar es salaam bila kusimama, ikiwa ni siku ya kwanza wasafirishaji hao kuamriwa kutumia kituo cha Makumbusho ambacho inaelekea hawaafiki.
 Daladala zikiwa zinapita bila kusimama sehemu yoyote
 Kituo cha kwenda Tegeta , Kawe na Mbezi kikiwa Kitupu Muda huu
 Kituo cha Mabasi Mwenye Cheupe hakuna hata Daladala hata moja
 Bajaji ndizo zimegeuka kuwa daladala na ni Tsh 1000 tu kwa mtu mmoja mpaka Mwenge
 Eneo ambalo Daladala zilikuwa nyingi sasa hakuna tena mabasi hayo

 Bajaji zikiendelea na Kazi
 Upande wa Mwenge kwenda Morocco Pia hakuna mabasi na kama yapo basi hayasimami
 Hali ya utulivu Mwenge
 Peupe hakuna Mabasi
 Abiria wakingoja Magari
 Wafanya Biashara Wadogo wadogo wakiwa wanajikusanya kwa ajili ya kujadili jinsi ya kuanza Mgomo na kushinikiza waanze kuweka meza zao pia hawataki ushuru
 Wafanya Biashara wakiwa wanaendelea kukusanyika ili kuandaa Mgomo wao
 Kushoto ni Meza moja ya Biashara ikiwa imeinuliwa ishara ya kuweka Meza na Kuanza Mgomo rasmi na kushinikiza kuwa waanze Biashara zao hapo kama kawaida na kutotaka ushuru wa kulipia pesa nyingi. Endelea Kufuatilia hapa... Mpaka tunaondoka eneo la tukio Polisi walikuwa wamesha wasili kwa kuanza Doria  na kuangalia usalama. Picha na Dar es salaam yetu blog

WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUSHIRIKIANA NA TMF ILI KUPUNGUZA UTEGEMEZI WA MATANGAZO

DSC_0540
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya bure kwa waandishi wa habari kwenye maeneo matano, sekta ya uchimbaji, unyanyasaji wa kjinsia, kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na kuzuia utumiaji wa madawa ya Kulevya kwa waandishi wa habari na utayarishaji na utengenezaji wa vipindi vya luninga na wanawake watangazaji jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma. kushoto kwake ni Msaidizi wa Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu, Dorothy Temu –Usiri na Mkurugenzi wa Mfuko wa vyombo vya habari, Ernest Sungura.(Picha zote na Zainul Mzige).

Na Damas Makangale

WAANDISHI WA HABARI nchini wamehimizwa kushirikiana kwa karibu na Mfuko wa Vyombo vya Habari (TMF) ili kuacha kutegemea zaidi matangazo kwa sababu kuna weka taaluma yao rehani.

Akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari jinsi ya kuripoti mambo ya sekta ya uchimbaji, unyanyasaji wa kijinsia, kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na kuzuia utumiaji wa madawa ya Kulevya na watayarishaji wa vipindi vya luninga, Waziri wa kazi na Ajira, Mhe, Gaudensia Kabaka amesema kwamba vyombo vya habari lazima vishirikiane na mfuko huo ili kuwa huru wakati wa kuripoti.

“kuendelea kutengemea matangazo kutoka kwenye makampuni mbalimbali ili kujiendesha kuna wafanya kutokuwa huru katika uandishi wetu na tasnia ya habari kwa ujumla,” amesema Kabaka
Amesema mradi huo wa mafunzo ya bure kwa waandishi ni muhimu kwa taifa kwa sababu tatizo kubwa la ajira hasa kwa vijana na wanawake linachangia kwa kiasi kikubwa vijana wengi kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
DSC_0434
Baadhi ya wadau na wageni waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi hayupo pichani.

Kabaka aliongeza kuwa mafunzo haya yatakayotolewa kwa ufadhili wa TMF ni muhimu ili kuelimisha jamii madhara ya kuuza na kusambaza dawa za kulevya na matumizi yake yanavyoathiri kizazi na kizazi.

“kwa sasa nchi yetu ya Tanzania ni moja ya nchi zilizoathirika sana na matumizi ya dawa za kulevya na mbaya zaidi kutumika katika njia ya kusambaza madawa hayo hatari,”
“kwa mujibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii tuna jumla ya watu 20,626 walioathirika na dawa za kulevya na kwa sasa wanapatiwa matibabu,” alisisitiza Kabaka.

Amesema nchini matumizi ya dawa za kulevya kwa zaidi ni Bangi, Heroin, Mirungi na Cocaine na cha kutisha matumizi haya yanaathiri pia wanafunzi wa sekondari na shule za msingi nchini.
DSC_0515
Msaidizi wa Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu(UNFPA), Dorothy Temu Usiri akitoa nasaha zake kwenye uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.

Kwa upande wake, Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu, Dorothy Temu-Usiri amesema kuwa kuongezeka kwa vitendo vya kikatili vya kijinsia na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi vimechochea kushirikiana na TMF kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari hapa nchini.

“kwa kuanzisha mafunzo haya ya bure kutasaidia waandishi wa habari kuandika kwa kina juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ambazo ndio kichocheo cha ukatili wa kijinsia hasa kwa Wanawake,” amesema Usiri.

Usiri aliongeza kwamba nchini Tanzania idadi kubwa ya watu wenye nguvu ya kufanya kazi ni vijana kwahiyo ni muhimu jamii ya kimataifa kushirikiana na serikali na taasisi zingine ili kunusuru kundi hili muhimu kwenye nchi.
DSC_0423
Mkurugenzi wa TMF nchini, Ernest Sungura akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa mafunzo ya bure yanayofadhiliwa na mfuko wake ambapo amesema kwamba malipo madogo kwa wahariri na waandishi wa habari kunadidimiza taaluma ya uandishi wa habari pamoja na swala la kutokubobea katika sekta husika (Specialization).
DSC_0490
Wadau watakaoshiriki kwa ukaribu kwenye mradi huo wakitambulishwa kwa mgeni rasmi kutoka kushoto ni Dkt. Pilly Said kutoka kitengo cha madawa ya kulevya hospitali ya Mwananyamala, January Nzisi Mkuu wa Kitengo cha Mtandao Tume ya Kudhibiti Madawa ya kulevya, Geodfrey Nzowa, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, kitengo cha Kupambana na Madawa ya Kulevya, Bi. Aida Teshe Kaimu Kamishina kutoka Tume ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya (DCC) na Florence Bahati Khambi Afisa Habari kutoka Tume ya Kudhibiti dawa za kulevya.
DSC_0458
Wadau mbalimbali na wageni waalikwa wakifuatilia yaliyojiri kwenye uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya bure kwa waandishi wa habari kwenye maeneo matano, viwanda, jinsia, madawa ya kulevya, kuzuia madawa ya kulevya kwa waandishi wa habari na utayarishaji na utengenezaji wa vipindi vya luninga na wanawake watangazaji jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
DSC_0498
Afisa Habari kutoka kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Habari (UNIC), Stella Vuzo amesema kwamba mradi huo umekuja katika muda mwafaka kwa taifa la Tanzania kwa sababu takwimu za matumizi ya dawa za kulevya zinatisha kwa vijana ni lazima taasisi za ndani na jamii za kimataifa kushirikiana kupambana na janga hili.
DSC_0405
Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo katika maeneo mbalimbali.
DSC_0406
DSC_0410
DSC_0395
DSC_0418
Afisa Habari kutoka kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Habari (UNIC), Stella Vuzo (kulia) pamoja na Bw. Phillip Musiba kutoka UNIC.
DSC_0432
Afisa mafunzo wa TMF, Bi. Raziah Mwawanga akinakili mambo muhimu yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi huo.
DSC_0414
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA(Mstaafu) Ananilea Nkya (kushoto) na Mwandishi wa Habari Mkongwe Mama Eda Sanga (katikati) ambaye ni miongoni mwa mentors kwenye mradi huo. Kulia Sawiche Wamunza kutoka UNFPA.

Sunday, June 1, 2014

MWIGULU NCHEMBA AMUUMBUA MBUNGE MSIGWA JIMBONI ASEMA ATAONGOZA MAPAMANO YA KUMNG'OA, APANIA KUPELEKA SHERIA BUNGENI YA KUFUTA MISAMAHA YA KODI

Naibu katibu mkuu wa CCM bara Mwigulu Nchemba akiwahutubia  wananchi wa  jimbo la Iringa mjini leo
vijana wa CCM wakifurahia  hutuba ya Nchemba leo
Wananchi  wa  jimbo la Iringa mjini wakimsikiliza Nchemba katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mwembetogwa
Viongozi  mbali mbali wa CCM mkoa  wa Iringa

Nchemba akipongezwa na kada wa CCM kutoka chuo cha Mkwawa
Kamanda  wa UVCCM mkoa  wa Iringa Salim Asas wa pili kulia akiwa na viongozi mbali mbali
Nchemba  akiwaaga  wana Iringa
Na Francis Godwin Blog
NAIBU katibu mkuu wa  chama cha mapinduzi (CCM) Bara Mwigulu Nchemba awahakikishia  wananchi wa jimbo la Iringa mjini kuwa  muda wa mbunge wa  jimbo hilo kuongoza umefika kikomo na kuwa ataongoza mapambano ya kumng’oa mwakani katika uchaguzi mkuu.

Akiwahutubia  wananchi  wa jimbo la Iringa mjini leo katika uwanja wa Mwembetogwa Nchemba ambae ni naibu  waziri wa fedha  alisema  kuwa mbali ya mbunge  huyo kupewa nafasi hiyo ya bure mwaka 2010 ila bado ameshindwa kuwa na huruma na wananchi wa  jimbo hilo na kuendelea kujinufaisha yeye badala ya kuwekeza kwa  wananchi hasa  vijana na ndio  sababu ya kushindwa kufanya vikao na wanachama wake na kuendelea kuitisha maandamano badala ya kufanya kazi.

“Tutajipanga  vema kila kona ya jimbo la Iringa mjini ili kulirudisha jimbo mikononi mwa CCM kwa  kumpata mbunge ambae  atawatumikia  wananchi na sio wa kujitumikia yeye na kuwa mbunge wa maandamano kwa kipindi chake  chote”

Nchemba  alisema  kuwa kutokana na kazi  kubwa iliyopfanywa na vijana wa jimbo la Iringa kwa kumpigania mbunge Msigwa alipaswa  kuwa na roho ya huruma kwa vijana hao ikiwa ni pamoja na kuwageuza daraja na kuwafanyisha maandamano yasiyo kwisha badala ya kuwaanzishia miradi ya kiuchumi.

“Hivi tazameni leo maeneo  yote ya makanda wa Chadema majimboni mwao ni maandamano kila siku kila wakati utasikia hakuna kulala makamanda huku mbunge anashindwa kuwasaidia …..na siku hizi wanakuja na hoja  ya makamanda pambaneni tutachukua nchi huku hata kata kwao ni ndoto  sasa niwaambie  leo hata nusu ya nchi hii kamwe  hawatapata”

Asema  mmoja kati ya mke wa  kiongozi mojawapo wa Chadema alimuuliza hivi kwa nini mume wake anapenda  sana maandamano alimjibu  kuwa mume  wake huyo akichukia huwa anafanya maandamano ndani ya chumba cha  kulala.
Nchemba  pia ameponmgeza  utendaji kazi wa mbunge wa  viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati na kuwa  siku  zote  amekuwa akiwapigania wananchi wa jimbo la Iringa mjini bungeni tofauti na mbunge wa jimbo mchungaji Msigwa ambae amekuwa akiongoza kwa kufanya maandamano.

Katika hatua  nyingine Nchemba  alisema amesema kuwa muda wa matajiri kuendelea  kujinufaisha na misamaha ya kodi  umekwisha na  kuwa anajipanga kupeleka sheria bungeni itakayowabana wafanyabiashara wakubwa kulipa kodi kama  wanavyolipa wafanyabiashara  wadogo.

Alisema kuwa  watu  wanapata misamaha  hadi inakatisha tamaa kwani ni pesa nyingi za kimaendeleo zinapotea  kutokana na utitiri wa misamaha inayoendelea kutolewa .

“Napeleka sheria katika bunge  hili la bajeti itakayofuta misamaha ya kodi kwa viwanda na wafanyabiashara  wakubwa…inakuweje  wananchi masikiti hata wanapotaka kuanzisha  saluni wanalipizwa kodi ila wafanyabiashara  wakubwa na baadhi ya  watu pia nitapeleka sheria ya kubana matumizi ya  fedha za umma”

Alisema kuwa inashangaza  kuona mashirika ya umma yanavuna na kutumia huku wanyonge wakiendelea  kuteseka na walimu na askari  wakiendelea kukosa kulipwa madai yao.

“hatuwezi  kusema  leo  walimu ama  askari ni wengi  wakati watu  wanakwepa kulipa kodi huku  wanafunzi  wakikosa mikopo ya elimu ya juu eti kutokana na kukosa fedha  wakati watu  wengine  wanakwepa kodi….hili ni jambo la aibu sana najua  wapo wabunge  watakaopinga ila  wananchi mtaona ni nani ni mbunge wa wananchi …kwani najua wapo  wabunge ambao hawalipendi hili watapinga ila lazima nilifikishe hata kama chungu ila lazima suala hili likomeshwe”

Mwili wa Mama Yake Mbunge Zitto Kabwe Wasafirishwa Kwenda Kigoma

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Kabwe akiwa na Mwenyekiti wa CUF Profesa  Ibrahimu Lipumba wakati wa kuuaga Mwili wa mama yake kipenzi Bi Shida Salumu aliyefariki leo kabla ya kusafirishwa kwenda Kigoma kwa mazishi
Ndege Ikiandaliwa Ili kuweza Kuingiza Mwili wa Marehemu Mama yake Zitto Kabwe
Waheshimiwa Wabunge na Baadhi ya Viongozi wakibeba Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Mama Yake Zitto Kabwe Bi Shida Salum  kuingiza kwenye ndege Tayari kwa safari ya kwenda Kigoma Kwenye mazishi
Prof Ibrahimu Lipumba akijadili jambo na Mwenzie baada ya kupakia mwili wa marehemu kwenye ndege kuelekea kigoma Kwenye maziko
Rais wa TASWA Juma Pinto akiwa VIP ya Terminal 1 JKN Airport alipokutana na Cardinal Pengo wakati wa kuaga mwili wa Mama yake Zitto Kabwe