Na Francis Godwin Blog NAIBU katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Bara Mwigulu Nchemba awahakikishia wananchi wa jimbo la Iringa mjini kuwa muda wa mbunge wa jimbo hilo kuongoza umefika kikomo na kuwa ataongoza mapambano ya kumng’oa mwakani katika uchaguzi mkuu.
Akiwahutubia wananchi wa jimbo la Iringa mjini leo katika uwanja wa Mwembetogwa Nchemba ambae ni naibu waziri wa fedha alisema kuwa mbali ya mbunge huyo kupewa nafasi hiyo ya bure mwaka 2010 ila bado ameshindwa kuwa na huruma na wananchi wa jimbo hilo na kuendelea kujinufaisha yeye badala ya kuwekeza kwa wananchi hasa vijana na ndio sababu ya kushindwa kufanya vikao na wanachama wake na kuendelea kuitisha maandamano badala ya kufanya kazi.
“Tutajipanga vema kila kona ya jimbo la Iringa mjini ili kulirudisha jimbo mikononi mwa CCM kwa kumpata mbunge ambae atawatumikia wananchi na sio wa kujitumikia yeye na kuwa mbunge wa maandamano kwa kipindi chake chote”
Nchemba alisema kuwa kutokana na kazi kubwa iliyopfanywa na vijana wa jimbo la Iringa kwa kumpigania mbunge Msigwa alipaswa kuwa na roho ya huruma kwa vijana hao ikiwa ni pamoja na kuwageuza daraja na kuwafanyisha maandamano yasiyo kwisha badala ya kuwaanzishia miradi ya kiuchumi.
“Hivi tazameni leo maeneo yote ya makanda wa Chadema majimboni mwao ni maandamano kila siku kila wakati utasikia hakuna kulala makamanda huku mbunge anashindwa kuwasaidia …..na siku hizi wanakuja na hoja ya makamanda pambaneni tutachukua nchi huku hata kata kwao ni ndoto sasa niwaambie leo hata nusu ya nchi hii kamwe hawatapata”
Asema mmoja kati ya mke wa kiongozi mojawapo wa Chadema alimuuliza hivi kwa nini mume wake anapenda sana maandamano alimjibu kuwa mume wake huyo akichukia huwa anafanya maandamano ndani ya chumba cha kulala.
Nchemba pia ameponmgeza utendaji kazi wa mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati na kuwa siku zote amekuwa akiwapigania wananchi wa jimbo la Iringa mjini bungeni tofauti na mbunge wa jimbo mchungaji Msigwa ambae amekuwa akiongoza kwa kufanya maandamano.
Katika hatua nyingine Nchemba alisema amesema kuwa muda wa matajiri kuendelea kujinufaisha na misamaha ya kodi umekwisha na kuwa anajipanga kupeleka sheria bungeni itakayowabana wafanyabiashara wakubwa kulipa kodi kama wanavyolipa wafanyabiashara wadogo.
Alisema kuwa watu wanapata misamaha hadi inakatisha tamaa kwani ni pesa nyingi za kimaendeleo zinapotea kutokana na utitiri wa misamaha inayoendelea kutolewa .
“Napeleka sheria katika bunge hili la bajeti itakayofuta misamaha ya kodi kwa viwanda na wafanyabiashara wakubwa…inakuweje wananchi masikiti hata wanapotaka kuanzisha saluni wanalipizwa kodi ila wafanyabiashara wakubwa na baadhi ya watu pia nitapeleka sheria ya kubana matumizi ya fedha za umma”
Alisema kuwa inashangaza kuona mashirika ya umma yanavuna na kutumia huku wanyonge wakiendelea kuteseka na walimu na askari wakiendelea kukosa kulipwa madai yao.
“hatuwezi kusema leo walimu ama askari ni wengi wakati watu wanakwepa kulipa kodi huku wanafunzi wakikosa mikopo ya elimu ya juu eti kutokana na kukosa fedha wakati watu wengine wanakwepa kodi….hili ni jambo la aibu sana najua wapo wabunge watakaopinga ila wananchi mtaona ni nani ni mbunge wa wananchi …kwani najua wapo wabunge ambao hawalipendi hili watapinga ila lazima nilifikishe hata kama chungu ila lazima suala hili likomeshwe”
|
No comments:
Post a Comment