Wednesday, May 1, 2013

KIKWETE ALIVYOLAKIWA KWA SHANGWE MBEYA

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAISI PROFESA MARK MWANDOSYA AKIWA NA MKEWE LUCY MWANDOSYA WAKIJIANDAA KUMPOKEA RAISI KIKWETE.
VIONGOZI MBALIMBALI WA MADHEHEBU YA DINI PIA HAWAKUWA MBALI KATIKA MAPOKEZI YA MHESHIMIWA RAISI KIKWETE.
WANANCHI WAKIMSUBIRI MHESHIMIWA RAISI KIKWETE NJE YA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA SONGWE MKOANI MBEYA.
VIJANA WA CHAMA CHA WAENDESHA BAJAJI JIJI LA MBEYA NAO HAWAKUWA MBALI KUMLAKI RAISI KIKWETE AMBAPO WALIKUWA NA MABANGO YA KUMSHUKURU NA KUMPONGEZA.
MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA MBEYA DR. MARY MWANJELWA AKIWA NA MKE WA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAISI BI LUCY MWANDOSYA WAKIJADILI JAMBO KATIKA CHUMBA CHA KUSUBIRIA ABIRIA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WAKIMSUBIRI RAISI  KIKWETE.
MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CRISPINI MEELA AKIMSIKILIZA WAZIRI WA NCHI  OFISI YA RAISI PROFESA MWANDOSYA.
MKUU WA WILAYA YA ILEJE BI ROSEMARY SENYAMULE AKITETA JAMBO NA WADAU WA HABARI MKOANI MBEYA HUKU WAKIMSUBIRI MHESHIMIWA RAISI.
MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CRISPIN MEELA AKIBADILISHANA MAWAZO  NA BAADHI YA WANAHABARI WA MKOA WA MBEYA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI ATHUMANI AKISISITIZA JAMBO KWA WAANDISHI WA HABARI WALIOJITOKEZA KUMLAKI MHESHIMIWA RAISI.
MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI ( SUGU) CHADEMA NAYE HAKUWA MBALI KUMLAKI RAISI KIKWETE
MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBASI KANDORO AKITETA JAMBO NA MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA MBEYA ATANUS KAPUNGA.

NDEGE ALIYOPANDA MHESHIMIWA RAISI IKIWASILI KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA SONGWE MKOANI MBEYA TAYARI KWA ZIARA YA SIKU MBILI.
RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE AKITEREMKA KWENYE NDEGE BAADA YA KUWASILI KATIKA UWANJA WA KIMATAIFA WA SONGWE MBEYA(SIA)
AKISALIMIANA NA VIONGOZI MBALIMBALI
BAADA YA KUVALISHWA SKAFU KUTOKA KWA VIJANA WA GREEN GUARD
AKISALIMIANA NA WANANCHI

NGOMA ZA ASILI ZIKITOA BURUDANI
AKIONDOKA KATIKA UWANJA WA NDEGE HUKU AKIWAPUNGIA WANANCHI MKONO.

Picha na Mbeya yetu

Behind the Scene of Bad Gyal Music Video

 Bad Gyal car park scene



 Bad Gyals in Position
 Bad Gyals doing their thing
 Bad Gyal in control
Bad Gyal rule

SHEREHE ZA MIAKA 49 YA MUUNGANO ZAFANA MUSCAT, OMAN

Ubalozi wa Tanzania mjini Muscat, Oman chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh, uliandaa sherehe iliyofana sana ya kuadhimisha miaka 49 ya Muungano. Sherehe hii ilifanyika katika ukumbi wa Jibrin kwenye hotel ya kitalii ya Intercontinental Muscat. 
 Mgeni rasmi katika sherehe hii alikuwa Mheshimiwa Ahmed bin Mohamed bin Salim Al Futaisi, Waziri wa wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Oman aliyeongoza ujumbe mzito wa Serikali ya Oman ambao ulijumuisha Mheshimiwa Mohamed bin Yousuf Al Zarafi, Naibu Katibu Mkuu , Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman, Mheshimiwa Khalil bin Abdullah Al Khonji, Mwenyekiti wa chama cha wafanya biashara na wenye viwanda wa Oman pamoja na wabunge Wabunge la Oman pamoja na wakuu wa Idara na maafisa waandamizi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman. 
 Sherehe hii pia ilihudhuriwa na mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini Oman , wananchi wa Oman , wafanyabiashara , watanzania waishio Oman , pamoja na waomani wenye asili ya Tanzania Katika hotuba yake Mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh alisifu juhudi za serikali za Tanzania na Oman katika kukuza uhusiano baina ya nchi mbili ambo ni wa kihistoria na unazidi kuimarika kadri siku zinavyoenda. Alieleza kuwa ziara ya Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyoifanya nchini Oman mwezi oktoba 2012 imeongeza kasi mpya katika Uhusiano wa Tanzania na Oman.
Katika ziara hii mikataba kadhaa ilisainiwa ikiwa ni hatua ya kuboresha mazingira ya kisheria katika Uhusiano wa Tanzania na Oman, mikataba hii ni Mkataba wa kulinda na kuendeleza vitega uchumi , mkataba wa ushirikiano katika masuala ya kumbukumbu na nyaraka, Mkataba wa ushirikiano wa katika Elimu ya Juu kati ya Oman na Zanzibar, mkataba wa kuunda baraza la pamoja la biashara kati ya Tanzania na Oman.. 
 Mheshimiwa Balozi alieleza pia kuwa ziara ya waziri wa Elimu ya Juu wa Oman Mhe. Rawiyah Al Busaidi nchini Tanzania na uzinduzi wa mfuko wa uzamini wa masomo ya Elimu ya shahada za juu, kufanyika kwa kikao cha kwanza cha tume ya pamoja ya ushirikiano baina ya Oman na Tanzania na kusainiwa kwa mkataba wa maridhiano kuhusu mashauriano ya kisiasa baina ya Tanzania na Oman kuwa ni mambo yanayozidi kuimarisha na kuboresha uhusiano wa kindugu uliopo baina ya Tanzania na Oman. 
 Sherehe hizi zilizofana sana zilipambwa na Kikundi cha Taifa cha sanaa kutoka Zanzibar ambacho kilitumbuiza kwa ngoma za kutoka sehemu mbalimbali Tanzania bila kusahau ngoma maarufu ya Msewe ambayo ilikuwa kivutio kikubwa kwa wageni waalikwa . Mheshimiwa Balozi na mgeni Rasmi walikata keki ikiwa ni ishara kuitakia mema Tanzania na Oman.
 Balozi wa Tanzania nchini Oman Mhe Ali Ahmed Saleh akipozi na kikundi cha utamaduni kilichotumbuiza katika siku hii adhimu

Balozi Ali Ahmed saleh akikata keki na mgeni rasmi katika sherehe hii Mheshimiwa Ahmed bin Mohamed bin Salim Al Futaisi, Waziri  wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Oman 
 Ngoma ya utamaduni toka Zanzibar
 Balozi Ali Ahmed Saleh akisoma hotuba yake
 Hotuba
 Balozi akiwa na maofisa wa Ubalozi Muscat
 Balozi Ali Ahmed Saleh akihutubia
 Ngoma ya msewe toka Zanzibar ilitia fora
 Wageni wakisikiliza hotuba

Watanzania wa Ujerumani wafanikisha Sherehe za miaka 49 muungano mjini kolon


 Dada Nashe Mvungi akionyesha bidhaa za Tanzania kwa wageni
Dada Tabia Mwanjelwa(mwenye) gitaa akiwa na wasanii wenzie jukwaani

 Naibu Balosi Mhe Ali Siwa akizungumza na Mzee.Katabalo, mtumishi mstaafu wa UN
 Naibu Balozi Mhe Ali Siwa akitoa hotuba ya Ufunguzi
 Naibu Balozi  Mhe. Ali Siwa akiwa na Msanii John Gambula kutoka Bagamoyo.
 Msanii Dada Joanita Henry(Mwenyeji wa muungano Day Koloni) akiwa na msanii mwenziwe kutoka Zimbabwe.
 Maana ya muungano yakubalika na watoto wa kimataifa !ngoma inogile.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Shah Smooth akiwarusha wageni
 Muungano oyeeee! huyu dogo naye ndani ya nyumba

Watanzania Ujerumani wakiduarika ktk Sherehe za muungani,mjini Koloni
 Hakubaki mtu nyumbani.

 wageni mbali mbali wakiipongeza Tanzania, mwenyekiti wa UTU Mh. Mfundo aliyevaa shati la kitenge akiongoza shughuli
 wageni wakijichagulia Bidhaa za Tanzania
 Wasanii wa kikundi cha Wabantu group wakiipeperusha TZ
Wasanii wa kitanzania wakiiepeperusha TZ katika maigizo 

Nathan mpangala aka Kijasti atembelea NEW YORK

 Darasani
 Mitaa ya Madison
 Balaa
 Ukumbi maarufu
 Mitaani... kama Dar unaambiwa...
 Neshno la Yankees
 Mradi wa babu
 Ndani ya basi la kitalii