Wednesday, October 3, 2012

Siku tatu za Flora na Emmanuel Mbasha mjini Goma, DRC

 Flora Mbasha na mumewe Emmanuel Mbasha  wakitambulishwa kwa mashabiki wao lukuki kwenye onesho lao mjini Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako walivunja rekodi kwa wingi wa mashabiki
 Kina Ras Makunja wa DRC ilibidi waletwe kuhakikisha ulinzi ni wa kutosha
 Flora na mumewe wakifanya vitu vyao kwa furaha
 Flora na mumewe wakisindikizwa hotelini kwao
 Msafara kuelekea kwenye onesho
 Ulinzi kwa Emmanuel Mbasha

 Flora akipozi na mlinzi wake
 Flora na mlinzi wake
 Flora akiwasili 
 Nyomi ikimsubiri Flora Mbasha
 Nyomi
 Ras Makunja na gitaa lake akilinda
 Flora na Emmanuel Mbasha Jukwaaani
 Emmanuel Mbasha akighani
 Uzalendo unamshinda mlinzi wa kina Mbasha
 Hapo ni Sebenen kwa kwenda mbele
 Flora na Emmanuel Mbasha wakipagawisha huku mlinzi wao akienda nao sambamba jukwaani
 Goma palikuwa hapatoshi
 Nyomi ya kufa mtu
 Flora na Emmanuel Mbasha wakienda sambamba na kwaya ya Goma
 hatari tupu
 Patashika ya nguo kuchanika
 Siku ilikuwa ya kihistoria kwa mji wa Goma
 Nyomi
 Hakuna hata pa kutemea mate
 Onesho likiendelea
 Mikono juuuu..
 Emmanuel Mbasha akifunguliwa mlamngo wa gari na Ras Makunja
 Gitaa nje nje...
 Ras Makunja akiripoti kazini
 Flora akiwa tayari kwenda oneshoni
Flora Mbasha akijiandaa kuondoka kuelekea oneshoni

Monday, October 1, 2012

Airtel kwa kushirikiana na Equity Benki yatoa mikopo kwa wafanyabiasha wadogowadogo



·         Zaidi ya wafanyabiashara (maarufu kama Machinga) 5000 kufaidika na mikopo hiyo

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Equity bank pamoja na Kampuni ya Ear promotion mwishoni mwa wiki hii imezindua mradi utakaowawezesha  wafanya biashara wadogo wadogo wa soko la machinga complex jijini Dar es saalam  kupata mikopo nafuu kwaajili ya kuendesha na kukuza biashara zao ambapo mikopo hiyo itatolewa na benki Equity kwa kupitia huduma ya Airtel money na wao kuwa wakifanya marejesho ya mikopo hiyo kwa kutumia Airtel money

Akizungumza wakati wa halfa ya uzinduzi wa mradi huo, Meneja uendeshaji wa benki ya Equity bw, David Mukaru  alisema” equity benki iko  mstari wa mbele kuisaidia  jamii katika huduma za kibenki ikiwemo mikopo ya riba nafuu hasa akina mama wa vikundi mbalimbali.

Benki yetu imekuwa sehemu ya maendeleo ya kukuza biashara na mtaji wa wafanyabiashara wadogo hadi wakubwa nchini. Leo kwa kushirikiana na Airtel kupitia huduma ya Airtel money tunawawezesha wafanyabiasha wa soko hili la machinga complex zaidi ya  efu tano kupata mikopo ya riba nafuu ambayo kwa hakika itakuza mitaji na kuwapatia ufanisi zaidi katika biashara zao”. 

Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja uhusiano wa Airtel bwn Jackson Mmbando alisema ”Airtel tunaendelea na mikakati yetu ya kusaidia jamii katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo kwa kupitia huduma  ya Airtel money, katika mradi hu Airtel tunarahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia simu yako ya mkononi, tunawawezesha wafanyabiashara hawa kupokea na kufanya marejesho ya mikopo yao kwa kupitia huduma ya Airtel money”

“lengo letu  Airtel ni kurahisi uendeshaji wa mikopo hii,  kuhakikisha usalama wa fedha, na kupunguza usumbufu wa wafanyabiashara hawa kutembea umbali mrefu kufanya marejesho ya mikopo hii”.  aliongeza Mmbando.

Naye mwenyekiti wa wafanyabisahara wa soko la machinga complex bw. Abdubakar Rakesh alisema ”ninaishukuru  kampuni ya Airtel pamoja na Equity benki kwa kutufikia sisi wafanya biashara wadogowadogo kwa kupitia mradi huu wa mikopo nafuu. ni kwa muda mrefu wafanyabiashara wa soko la machinga complex wamekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupata mikopo nafuu ambayo itawawezesha kukuza mitaji na kuweka bidhaa mbalimbali zitakazo wavutia wateja kufanya manunuzi katika soko hili, hivyo kwa kupitia mradi huu tunaamini tutafanikisha matarajio yetu ya kuwa na soko la kisasa lenye miundo mbinu na hadhi kwa wafanyabishara na wateja wetu.

Naye bw, Brian Kikoti Mkurugenzi wa Ear promotion Kampuni inayosimamia na kuratibu mradi huo amewasifu Equity Benki pamoja na Airtel kwa kuungana nao katika kusaidia kusimamia ufanisi wa soko hilo na la wafanyabiashara wadogowadogo.

Mbali na ushirikiano huu wa kibiashara na  Equity bank,  Airtel tayari inashirikiana na mashirika mbalimbali yakiwemo GEPF , LAPF, DAWASCO, TANESCO, USA EMBASSY, COCACOLA na mengine mengi katika kutoa huduma zao kupitia huduma ya Airtel money.

VODACOM YACHANGIA UANZISHWAJI MFUKO WA WALEMAVU ZANZIBAR


·        Yachangia 15M. Ni mfuko mpya maalum wa serikali
·        Yalilia juhudi zaidi kukomboa walemavu
·        Vodacom Foundation kuendeleza misaada zaidi Zanzibar

 Ikikadiriwa kuwa na watu wenye ulemavu wapatao 9000 Visiwani Zanzibar, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha mfuko maalum wa maendeleo ya watu wenye ulemavu hatua iliyoungwa mkono kwa dhati na kampuni ya Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation”kwa kuchangia Shilingi 15 Milioni.
Vodacom Foundation imechangia fedha hizo katika hafla maalum ya kuchangisha fedha iliyoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya umma na binafsi katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort,Mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.
“Vodacom Tanzania inaipongeza sana serikali ya Zanzibar hasa Ofisi ya Makamu wa Rais wa Kwanza kwa kuchukua hatua za ziada kubuni njia za kusaidia jamii ya watu wenye ulemavu ambao wanakabiliwa na changamoto kadhaa za kimaisha, Hili ni jambo jema na tunlaiunga mkono” Alisema Mkuu wa Mawasiliano na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Bi. Joseline Kamuhanda Bi Kamuhanda akimueleza Rais wa Zanzibar Dk. Shein.
 Kabla ya kukabidhi hundi ya mfano wa fedha hizo Kamuhanda alisema Vodacom Tanzania inatoa fedha hizo kupitia mfuko wake wa Vodacom Foundation wenye shabaha ya kusaidia juhudi za ustawi wa jamii nchini kwa kutambua umuhimu wa mchango wa sekta binafsi kuunga juhudi za serikali za kuboresha maisha ya watu.
“Tunapongeza juhudi zako Mheshimiwa Rais Dk. Shein na kipekee tunampongeza Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad kwa ubunifu wa kuanzisha mfuko huu, ni imani yetu kwamba shabaha ya uanzishwaji wake itafikiwa na kuleta faraja kubwa kwa ndugu zetu wenye ulemavu.” Aliongeza Joseline Kampuni ya Vodacom kupitia Vodacom Foundation imekuwa ikichangia juhudi mbalimbali za kijamii Zanzibar katika maeneo ya elimu, afya, uwezeshaji wananchi kiuchumi hususan wanawake kupitia mradi wa MWEI na imeahidi kuendelea kufanya hivyo.
“Shabaha ya kampuni ya Vodacom hapa nchini sio tu biashara bali pia kuona maisha ya jamii  zinazotuzunguka yananufaika na uwepo wetu kazi inayofanywa kupitia Vodacom Foundation na ndio maana leo Mh. Rais Vodacom ni moja ya wahisani wakuu waliofanikisha kuanza kazi kwa mfuko huu.” Aliongeza Joseline
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  Dk. Mohammed Shein akizungumza katika hafla hiyo aliwashukuru wadhamini waliowezesha kupatikana kwa fedha za kuanza kwa mfuko huo Vodacom Tanzania ikiwa moja ya wadhamani wakuu na hivyo kuzinduliwa rasmi na kutoa rai kwa michango ili kasi iliyoanza nayo mfuko huo iwe endelevu huku Makamu wa kwanza wa Rais, Maalim Seif, akiuelezea mfuko huo kuwa umelenga kuwezesha watu wenye ulemavu kujiajiri, mafunzo, uwezeshaji, afya, unyanyapaa n.k
Mfuko huo upo chini ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na kuanzia sasa watu mbalimbali wanauwezo wa kuchangia kutumia huduma ya Vodacom M – pesa kupitia namba 0755 222666, namba maalum iliyo tolewa kwa hisani ya Vodacom ili kurahisisha uchangiaji wa fedha katika mfuko huo.
Mwisho……

MZEE MWINYI AWAKABIDHI KWADELO TANGI LA MAJI, KITANDA CHA KUJIFUNGULIA


 Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, Omari Kariati akimsalimia Mama Sitti Mwinyi nyumbani kwa Rais Mstaafu Ali Hassani Mwinyi (kushoto), Mikocheni jijini Dar es Salaam. kabla ya hafla ya wananchi wa Kata hiyo kukabidhiwa tangi la maji na kidanda cha kujifungulia kina mama, iliyofanyika nyumbani hapo Jumapili.
 Diwani Kariati akiongozana na Mzee Mwinyi na Mama Sitti Mwinyi kwenda eneo la tukio
 UNAONA MAMBO YA KILIMO KWANZA? Akasema Omari Kariati wakati akitazama maembe yaliyopo kwenye mwembe wa kisasa uliopo nyumbani kwa Mzee Mwinyi.
 












Kina mama wa Kwadelo wakiwa kwenye viwanja vya shughuli ya makabidhiano ya vifaa hivyo
 "Kwanza tunamshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mzee wetu  Ali Hassan Mwinyi kwa kutukaribisha nyumbani kwake kukamilisha hafla hii. Shughuli iliyotuleta hapa ni Mzee wetu kuwakabidhi wana-Kwadelo tangi kubwa la maji la sh. 650,000 na kitanda cha kujifungulia kina mama, kisha atamapatia sh. 200,000 kijana wetu aliyemuahidi kwa ajili ya kukamilisha masomo yake ya ualimu pale Ununio" akasema Diwani wa Kwadelo Omari Kariari kufungua shughuli. pembeni ni Mzee Mwinyi na Mkewe Mama Sitti, wakimsikiliza.
 













Kisha mzee Mwinyi na mkewe wakasongea pamoja na waalikwa pahala vilipokuwa vitu vya kukabidhi. Hapa anakabidhi kitanda
 












Kwa furaha baada ya kukabidhiwa, mama mmoja wa Kwadelo akakifanyia majaribio kidogo kitanda hicho.
 













Kisha Mzee Mwinyi akakabidhi tangi la lita 5000 kwa Mwadham Msami (kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kerereng'ombe, palepale Kwadelo. Naye Omari Kariati akishuhudia
 Baada ya kurejea meza kuu, Mzee Mwinyi akakabidhi sh. 200,000 kwa kijana, Kassim Omar kwa ajili ya kumalizia masomo yake ya ualimu Chuo cha Ununio, Bagamoyo.
 













Kisha Mzee Mwinyi akaeleza yake ya moyoni kuwahusia wana Kwadelo na Watanzania kwa jumla akisema "wanaodhani maandamano yanaleta maendeleo wanapotea, maendeleo yanaletwa na kujituma na kutumia fursa zilizopo kufanya kazi kwa bidiii". Kushoto ni Mama Sitti Mwinyi.
 












Picha za pamoja na Mzee mwinyi zikapigwa kwa makundi ya wananchi wa Kwadelo waliohudhuria hafla hiyo
 Hawa ni kina mama wa Kwadelo wakiwa na Mzee Mwinyi
 












Na kina Baba wakachangamkia 
 Vijana wa Kwadelo wakiwa nyumna ya Mzee Mwinyi katika picha ya pamoja
 Hawa pia ni vijana wa Kwadelo kati ya 50 wanaofanya shughuli zao jijini Dar, waliojitolea kwenda kulima katika kata hiyo 
 Waandishi nao wakatumia fursa hiyoo adhimu kupigapicha na Mzee Mwinyi. Kulia kabisa ni Mimi
 











Hapa pia ni waandishi wakichangamkia fursa hiyo.
 "Karibuni Chai" akasema Mama Sitti kuwakaribisha wageni mwishoni mwa shughuli
Wageni wakachangamkia chai