· Yachangia 15M. Ni mfuko mpya maalum wa
serikali
· Yalilia juhudi zaidi kukomboa walemavu
· Vodacom Foundation kuendeleza misaada
zaidi Zanzibar
Ikikadiriwa kuwa na watu wenye ulemavu wapatao 9000
Visiwani Zanzibar, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha mfuko maalum wa
maendeleo ya watu wenye ulemavu hatua iliyoungwa mkono kwa dhati na kampuni ya
Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation”kwa
kuchangia Shilingi 15 Milioni.
Vodacom Foundation imechangia fedha hizo katika hafla maalum ya
kuchangisha fedha iliyoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya
umma na binafsi katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort,Mjini Zanzibar mwishoni
mwa wiki.
“Vodacom Tanzania inaipongeza sana serikali ya Zanzibar hasa Ofisi ya Makamu
wa Rais wa Kwanza kwa kuchukua hatua za ziada kubuni njia za kusaidia jamii ya
watu wenye ulemavu ambao wanakabiliwa na changamoto kadhaa za kimaisha, Hili ni
jambo jema na tunlaiunga mkono” Alisema Mkuu wa Mawasiliano na Mahusiano wa
Vodacom Tanzania Bi. Joseline Kamuhanda Bi Kamuhanda akimueleza Rais wa
Zanzibar Dk. Shein.
Kabla ya kukabidhi hundi ya mfano wa fedha hizo Kamuhanda alisema
Vodacom Tanzania inatoa fedha hizo kupitia mfuko wake wa Vodacom Foundation
wenye shabaha ya kusaidia juhudi za ustawi wa jamii nchini kwa kutambua umuhimu
wa mchango wa sekta binafsi kuunga juhudi za serikali za kuboresha maisha ya
watu.
“Tunapongeza juhudi zako Mheshimiwa Rais Dk. Shein na kipekee
tunampongeza Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad kwa ubunifu wa
kuanzisha mfuko huu, ni imani yetu kwamba shabaha ya uanzishwaji wake itafikiwa
na kuleta faraja kubwa kwa ndugu zetu wenye ulemavu.” Aliongeza Joseline
Kampuni ya Vodacom kupitia Vodacom Foundation imekuwa ikichangia juhudi
mbalimbali za kijamii Zanzibar katika maeneo ya elimu, afya, uwezeshaji
wananchi kiuchumi hususan wanawake kupitia mradi wa MWEI na imeahidi kuendelea
kufanya hivyo.
“Shabaha ya kampuni ya Vodacom hapa nchini sio tu biashara bali pia
kuona maisha ya jamii zinazotuzunguka
yananufaika na uwepo wetu kazi inayofanywa kupitia Vodacom Foundation na ndio
maana leo Mh. Rais Vodacom ni moja ya wahisani wakuu waliofanikisha kuanza kazi
kwa mfuko huu.” Aliongeza Joseline
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Mohammed Shein akizungumza katika hafla
hiyo aliwashukuru wadhamini waliowezesha kupatikana kwa fedha za kuanza kwa
mfuko huo Vodacom Tanzania ikiwa moja ya wadhamani wakuu na hivyo kuzinduliwa
rasmi na kutoa rai kwa michango ili kasi iliyoanza nayo mfuko huo iwe endelevu huku
Makamu wa kwanza wa Rais, Maalim Seif, akiuelezea mfuko huo kuwa umelenga
kuwezesha watu wenye ulemavu kujiajiri, mafunzo, uwezeshaji, afya, unyanyapaa
n.k
Mfuko huo upo chini ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na
kuanzia sasa watu mbalimbali wanauwezo wa kuchangia kutumia huduma ya Vodacom M
– pesa kupitia namba 0755 222666, namba
maalum iliyo tolewa kwa hisani ya Vodacom ili kurahisisha uchangiaji wa fedha
katika mfuko huo.
Mwisho……
No comments:
Post a Comment