
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya wananchi wa Nanyumbu (hawapo kwenye picha), wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya na uhamasishaji kwa wananchi kujiunga na Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akipitia ubao wa matangazo ya gharama za matibabu katika Hospitali ya Rufaa Nanyumbu, akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya na uhamasishaji kwa wananchi kujiunga na Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara.

Waziri wa Afy, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisoma cheti cha mtoto aliyefikishwa na baba yake Hospitali ya Wilaya Nanyumbu ili kupata huduma za Afya.

Wananchi wa Nanyumbu wakiongozwa na Wazee waliojitokeza kumsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu pindi alipokuwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya na uhamasishaji kwa wananchi kujiunga na Bima ya Afya Mkoa wa Mtwara.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiwasalimia wanafunzi wa shule ya awali pindi tu alipowasili kwaajili ya mkutano wa hadhara na wananchi wa Nanyumbu ili kusikiliza kero zao na kuwaeleza Maendeleo ya Sekta ya Afya kwaujumla.
Na WAMJW - Nanyumbu, Mtwara
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu ametoa onyo Kali kwa Wauguzi wote kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini wanaovunja maadili na miiko ya kazi za uuguzi ikiwemo matumizi ya lugha chafu kwa wagonjwa na wanaowapiga akina mama wajawazito wakati wakijifungua.
Ameyasema hayo wakati alipotembelea Hospitali ya Wilaya Nanyumbu, akiwa katika ziara yake Mkoani Mtwara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na uhamasishaji kwa wananchi juu ya umuhimu wa kujiunga na Bima ya Afya hasa katika msimu huu wa Biashara ya Korosho.
Waziri Ummy alisema kuwa Serikali kupitia Baraza la Uuguzi litawafutia usajili Muuguzi yeyote atakayegundulika ametenda kosa la kumpiga mama mjamzito au kumtolea lugha chafu wakati wa kujifungua.
"Tunataka kumjua huyo, ambae ni hodari sana wakupiga wanawake wajawazito, makofi wakati wakujifungua, kwa kweli huyo ni wa kumfukuza kazi, Mimi mkiniletea namfutia Leseni yake kabisa, hafanyi kazi Serikalini, hafanyi kazi Sekta Binafsi" alisema Waziri Ummy.
Pia, Waziri Ummy alitoa Maagizo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe.Hamis Dambaya kuhakikisha Wauguzi na Watumishi wote wanavaa vitambulisho vya kazi wakati wote wakiwa eneo la kazi ili wananchi wanaokwenda kupata huduma za Afya waweze kuwatambua majina yao.
"Tumewaambia wavae vitambulisho, ili mtusaidie kutaja jina la Wauguzi wanaovunja maadili ya kazi zao, hapa naomba nisiwahukumu wote, Mganga Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi mpo hapa, nikirudi tena nisisikie kuna Muuguzi anapiga makofi wajawazito wanaokuja kujifungua" alisema Waziri Ummy.
Kwa upande mwingine Waziri Ummy amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya italeta mashine mpya ya kisasa ya digitali ya X-Ray ndani ya miezi mitatu itayosaidia wananchi wa Nanyumbu hasa kutokana na Wilaya hiyo kuwa katika Bara bara kuu ya kutoka Masasi hadi Songea.
Aidha, Waziri Ummy ametoa Rai kwa wananchi wa Nanyumbu kuhakikisha kabla ya kufika Disemba 31 mwaka huu, kaya zote katika eneo hilo lazima liwe limejenga na kutumia choo bora ili kupunguza magonjwa ya Bakteria yanayoigharimu Serikali pesa nyingi katika matibabu na Dawa.
"Ndugu zangu nendeni pale Hospitali, katika kila Wagonjwa 100, Wagonjwa 60 wana magonjwa ya kuhara,magonjwa ya tumbo, magonjwa yanayohusiana na kiwango duni cha usafi, nimekuwa nikiimba wimbo huu tangu nikiwa Waziri wa Afya, na hapa tulipofikia ni agizo la Waziri Mkuu pindi alipokutana na maafisa Afya wa Halmashauri na Mkoa jijini Dodoma" alisema Waziri Ummy
Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa akiwa kama Waziri wa Afya kazi kubwa aliyonayo ni kuhakikisha anawakinga watu wasiumwe na pale wanapoumwa waweze kupata Huduma Bora za Afya, lazima niwe mkali kwenye kinga, mimi ni Waziri wa Afya sio Waziri wa Wagonjwa" alisema Waziri Ummy.
1 comment:
UTAJIRI AU FEDHA ZA NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MFUPI
(Kwanza kabisa nataka kukwambia kwamba hakika utajili ni azina kutoka kwa mwenyezi mungu na pia kuna viumbe alio wapa mamlaka na nguvu ya kumiliki mali)
MPAKA MASAA 72(SIKU3) PAPO HAPO KWA MASHARTI MAALUM KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......
KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA
kwa maelezo kamili piga namba +255742162843
(KWANINI USUMBUKE,HACHA KUTANGATANGA, NA MAISHA NI MAFUPI PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI (Tumia ufahamu kujinasuaUTAJIRI WA NDAGU(MASHARTI) NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......
NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO
(HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)
MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE, KAMA UNASUMBULIWA NA MAJINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI.
NIPIGIE 0742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.
(kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
1. uwe una umri wa miaka 18+
2. uwe tayari kupokea masharti yote
3.uwe na uwezo wa kutunza siri
4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote
KARIBU SANA KWA SHIDA NYINGINE PIA ULIYONAYO AMBAYO SIJATAJA INSHAALAH ITATATULIWA IKIWA NDANI YA UWEZO WANGU.
Post a Comment