Saturday, December 8, 2018

WAJUMBE ALAT SHINYANGA WATEMBELEA ILEMELA,SENGEREMA KUPIGWA MSASAWajumbe wa ALAT wakipata ufahamu wa namna maji ya Ziwa Victoria yanavyovutwa na kusafishwa kasha kusambazwa kwa wananchi walipfanya zaiara wilayani Sengerema.
Wajumbe wa ALAT wakiwa katika mtambo wa kusafisha maji kabla ya kusambaza kwa wananchi walipfanya zaiara wilayani Sengerema.
Wajumbe wa ALAT waendelea kupata elimu katika mtambo wa kusafisha maji kabla ya kusambaza kwa wananchi walipfanya zaiara wilayani Sengerema.
Wajumbe wa ALAT wakipanda tangi la kuhifadhi na kusambaza maji ya Ziwa Victoria walipotela ya kusambaza kwa wananchi walipfanya zaiara wilayani Sengerema.……………………….

Na Robert Hokororo

Wajumbe wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Shinyanga wamefanya ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Wilaya ya Sengerema jijini Mwanza kujifunza namna ilivyofanikiwa katika miradi ya maendeleo.

Miradi iliyotembelewa na wajumbe hao ni pamoja na urasimishaji na upimaji wa ardhi manispaa ya Ilemela pamoja na mradi wa maji ya Ziwa Victoria katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema. Ziara hiyo ilihusisha wajumbe wa ALAT kutoka Halmashauri za Wilaya za Kishapu, Ushetu Msalala, Shinyanga, Mji wa Kahama na Manispaa ya Shinyanga pamoja na baadhi ya wataalamu wake.

Katika kikao kilichowakutanisha wataalamu wa Ardhi na ujumbe huo kutoka mkoani Shinyanga walipata taarifa kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na idara hiyo ambazo zimesaidia kutatua migogoro ya ardhi. Akielezea kuhusu miradi hiyo, Afisa Mipango Miji Manispaa ya Ilemela, Shukrani Kyando alisema katika mwaka uliopita walipanga kupima viwanja 16,000 na hadi sasa wamepima 33,200 huku matarajio ni kufikia 52,000.

Alisema hadi sasa tayari wana michoro ya viwanja 52,000 ambapo wanaandaa michoro ya mipango miji baada ya kuchukua taarifa za kila nyumba ili kuweza kuwa na mji uliopangika vizuri. Kwa upande wao baadhi ya wananchi kutoka Kata ya Shibuda kuwa mradi wa urasimishaji wa ardhi wameupokea vizuri na kueleza kuwa umeweza kuondoa migogoro ya ardhi.

Wakishukuru na kupongeza Idara ya Ardhi katika manispaa hiyo, wananchi hao walisema wamepimiwa vizuri viwanja kupitia upimaji shirikishi ambao umefanyika bila kuharibu mipango miji. Akitoa maoni kuhusu mradi huo Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Shinyanga, Ngasa Mboje aliupongeza na kusema kuwa hilo ni jambo zuri na linalofaa kuigwa na halmashauri za mkoa huo.

Alibainisha kuwa wao kama wajumbe wa ALAT Mkoa wa Shinyanga wanayo mengi ya kujifunza kutoka katika mradi huo wa upimaji ardhi unaotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.

“Tumeona tujifunze kutoka kwa wenzetu hawa wa Ilemela na na ni jambo zuri kwani unapima kulingana na eneo lilivyo na sisi kule kwetu (Shinyanga) tuna miji iliyoanza kupanga kwa mfano kule Mhunze (Wilaya ya Kishapu) na Old Shinyanga (Manispaa),” alidokeza Mboje.

Wakiwa wilayani Sengerema wajumbe hao walitembelea mradi wa maji ya Ziwa Victoria na kujionea shughuli za uzalishaji maji kutoka chanzo hicho na kuyasambaza mji wa Sengerema.

No comments: