Monday, December 3, 2018

SCANIA WAZINDUA LORI LA 'NEW GENERATION' AMBALO NI RAFIKI WA MAZINGIRA, JANUARI MAKAMBA AWAPONGEZA

 Waziri was Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano January Makamba (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Scania Lars Eklund wakati wa uzinduzi wa aina mpya ya malori ya Scania jijini Dar es Salaam.Wengine ni sehemu ya maofisa wa Shirika la Scania.
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano January Makamba (kulia) akisalimiana na moja ya wadau wa usafiri nchini wakati wa uzinduzi wa lori la Scania 'New Generation' .Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano January Makamba akizungumza wakati wa uzinduzi wa malori mapya ya Shirika la Scania .Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano January Makamba akiwa ndani ya Lori la Scania ikiwa ni ishara ya kulizindua rasmi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Scania nchini Lars Eklund akizungumza wakati wa uzinduzi wa lori mpya ya Scania ambayo ni rafiki wa Mazingira na yenye kutumia mafuta kidogo
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SHIRIKA la Scania Tanzania imezindua kizazi kipya cha malori kwenye sekta ya usafiri nchini 

huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano January Makamba akilisifu shirika hilo kwa kuzindua malori hayo ambayo ni marafiki wa mazingira.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo wa kizazi kipya cha malori ambayo mbali ya kuwa rafiki wa mazingira yemetengenezwa katika mfumo wa kuhakikisha dereva 

anakuwa salama hata inapotokea ajali pamoja na ulaji mdogo wa mafuta, Makamba amesema analipongeza Shirika la Scania Tanzania kwa kutambua dhana ya kutunza mazingira ambapo imeamua kuja na malori ambayo mfumo wake ni rafiki wa mazingira.

"Huko tunakoelekea iko haja ya kuhakikisha tunakuwa na vyombo vya usafiri ambavyo vitakuwa rafiki wa mazingira badala ya kuwa usafiri ambao unaharibu wa mazingira.Kuna baadhi ya vyombo vya usafiri vinatoa moshi mwingi ambao ni hatari kwa mazingira yetu, hivyo 

lazima tuwe na usafiri rafiki katika kuhakikusha tunakuwa salama zaidi,"amesema Makamba.Pia Makamba amesema dunia ikiwa ni pamoja na Tanzania inakaribia hatua ya kusonga mbele ambapo kuunganishwa kwa teknolojia mpya na mifano mbalimbali ya biashara inaleta ufumbuzi wa usafiri wa kudumu na utoandoa usafiri wa kawaida.

Ameongeza mbeleni usafiri utakuwa wa hewa nzuri ,safi, umeme , automatic na kidigitali na kwamba uzinduzi wa lori mpya za scania utasaidia kuonesha na kutekeleza mambo mbalimbali yaliyokubaliwa katika mazingira tafatiliwe.

Amesisitiza kwa namna ambavyo shirika la Scania limejikita kwenye teknolojia ya hali ya juu katika kutengeneza malori maana yake ni kwamba inalenga kuwa kiongozi katika usafiri endelevu ambapo kwa kushirikiana na ujuzi itasaidia katika ukuaji ."Ustawi pia ni mojawapo ya kitu muhimu kinachoangaliwa katika uzinduzi huu Tanzania, kwa kuwa hii itakuwa muhimu katika ushindani wa baadae wa scania na wateja wake."

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Scania Lars Eklund amesema Tanzania haina usafiri ambao hupunguza athari kwenye mazingira na itafanya hivyo kwa kuboresha ufanisi ambao utatoa faida za kiuchumi , kwasababu hiyo pia ni motisha kwa kila biashara." Kwa maneno mengine itaboresha afya salama katika mazingira kwa wakati mmoja."

Pia amesema kuwa ustawi wa pia ni usalama wa barabarani , hivyo wanahitaji kupunguza ajali kwa manufaa ya binadamu , kwa jamii na kwa manufaa ya biashara , mambo hayo daima huenda kwa mkono kwa mkono na faida ya ustawi na kwamba lori hiyo mpya inatoa msaada kwa dereva kikamilifu kumsaidia dereva kuendesha kwa usalama na ufanisi zaidi.

No comments: