Monday, December 3, 2018

PAMOJA FOUNDATION YAZINDUA HOSTEL YA WASICHANA KWA SHULE ZA SERIKALI

Diwani wa Kata ya Tuangoma iliyopo Mbagala Dar es Salaam Mohamed Suleiman akifungua Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam, hosteli iliyojengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation.Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Pamoja Foundation Haji Mrisho.
Diwani wa Kata ya Tuangoma iliyopo Mbagala Dar es Salaam Mohamed Suleiman akizungumza wakati wa uzinduzi wa Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam leo, hostel hiyo imejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation. Kushoto kwa Diwani ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Pamoja Foundation Haji Mrisho.
Diwani wa Kata ya Tuangoma iliyopo Mbagala Dar es Salaam Mohamed Suleiman (kulia) akiangalia vitanda katika moja ya vyumba vya Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam, hosteli hiyo imejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation. Wa pili Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Pamoja Foundation Haji Mrisho.
Diwani wa Kata ya Tuangoma iliyopo Mbagala Dar es Salaam Mohamed Suleiman akikata utepe kuzindua Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam, hosteli hiyo imejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Pamoja Foundation Haji Mrisho akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam iliyojengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation.
Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi ya Pamoja Foundation Khamis Awadh akizungumza katika hafla ya kuzindua Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam, hosteli hiyo imejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation.
Baadhi ya akina mama waliojitokeza katika hafla ya kuzindua Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam hosteli hiyo imejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika hafla ya kuzindua Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam hosteli hiyo imejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation. 

…………………………………………………………………………. 

Na Mwandishi wetu 

Katika kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu kwa ufanisi zaidi taasisi ya Pamoja Foundation kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation imezindua hostel kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa shule za serikali. 

Uzinduzi wa hostel hiyo uliogharimu jumla ya shilingi milioni 50 umefanywa leo na Diwani wa Kata ya Tuangoma Mohamed Suleiman kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la Mbagala Ally Mangungu katika eneo la Mzinga wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa hostel hiyo, Diwani wa Kata ya Tuangoma Selemani amepongeza ubunifu uliofanywa na taasisi ya Pamoja foundation kwa kuanzisha mradi wa kusaidia wasichana hasa katika masuala ya elimu na kuzitaka taasisi nyingine kushirikiana katika kusaidia masuala ya elimu ili kuleta maendeleo katika sekta ya elimu. 

Aidha, aliwaasa wananchi wengine kuiga mfano wa mwananchi wa eneo la Mzinga kwa kutoa eneo la wakfu kwa ajili ya kujengwa hostel hiyo ambapo alisema uamuzi huo utawezesha kujenga hostel nyingi na kubainisha kuwa eneo la Tuangoma ulipo mradi wa viwanja 20000 yeye kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la Mbagala ataangalia namna ya kupata kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa hostel kwa kuwa katika mradi huo kuna maeneo yametengwa kwa ajili ya shule. 

Diwani huyo wa kata ya Tuangoma alizishauri taasisi nyingine kuangalia namna ya kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo katika fani mbalimbali katika eneo la uchumi ili baadaye nao waweze kusaidia watu wengine. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Pamoja Foundation Haji Mrisho alisema hostel iliyozinduliwa yenye uwezo wa kuwatunza wanafunzi 40 itajulikana pia kama Kituo cha Kuendeleza Wanafunzi ni kwa ajili ya wanafunzi wa shule za serikali. 

Kwa mujibu wa Mrisho, uamuzi wa kuanzisha hostel hiyo unatokana na utafiti uliofanywa na taasisi yake katika wilaya za Ilala, Temeke na Kigamboni kuonesha wanafunzi wanaoishi shule za bweni wanafanya vizuri ukilinganisha na na wale wa shule za kutwa. 

Mkurugenzi huyo wa Pamoja Foundation alisema, kiwanja ilipojengwa hostel ni kiwanja kilichotolewa wakfu na kubainisha bila msaada huo ingekuwa vigumu kuamilisha mradi huo lengo kuunga mkono juhudi za ardhisetikali elimu bure na kuhamiasisha kuunga mkono Serikali kwa kuwa wadau wanaweza kusaidia aidha kwa maabara, hostel ama madarasa. 

Alisema Taasisi yake imeanzisha hosteli hiyo ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kutoa elimu bure na mwakani taasisi hiyo inatarajia kuanzisha hostel ya wavulana sambamba kuwa na kituo cha mafunzo ya ujasiriamali ili kuwawezesha watakaoshindwa kuendelea na masomo katika viwango tofauti kupata taaluma zitakazowasiadia kimaisha. 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa Pamoja Foundation, mbali na makazi wanafunzi watakaoishi katika hostel hizo watapatiwa elimu,vifaa mbalimbali vya kujisomea pamoja na mpango wa afya ili wasihangaike katika masuala ya elimu. 

Mrisho alibainisha kuwa, awali taasisi ya Pamoja Foundation ilikuwa na mpango wa kupanga jengo kwa ajili ya hostel lakini kupatikana kwa jengo la kudumu kumewapa faraja kubwa kwa kuwa sasa wamepata mradi wa kudumu. 

Mrisho alisema, lengo Ia uanzishwaji hostel ya wasichana kwa wanafunzi wa shule za Serikali ni kuwawezesha kusoma vizuri hasa ikizingatiwa watoto wa kike wamekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo majukumu mengi wanapokuwa majumbani ukilinganisha wavulana. 

Mlezi wa Kituo cha Malezi cha Ibnu Jazar kilichopo Vikundi Picha ya Ndege Dar es Salaam Mfaki Mohamed alishauri wasichana watakaopata fursa ya kukaa katika hosteli hiyo kutunzwa vyema ikiwa ni pamoja na wale watakaokuwa na jukumu la kuwalea kuzungumza nao katika njia iliyo bora na kuachana na ile dhana ya kuona kuwa viboko kama njia pekee ya kuwalea wasichana ama wanafunzi na kusisitiza ulelewaji mzuri kwa wasichana basi kutaepusha mzozo 

Kwa mujibu wa Mfaki kwa sasa kuna adui mazingira kwa wasichana ambapo kumekuwa na vishawishi vinavyorudisha nyuma wasichana hasa katika masuala ya maadili na kushauri njia bora ya kukabiliana na hali hiyo ni kuwandaa wasichana kimaadili ili kuepukana vishawishi mbalimbali kwa wale watakaopata fursa katika hosteli hiyo.

No comments: