Wednesday, December 5, 2018

MRADI WA LTA WAMALIZA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA KIJIJI CHA MAGUBIKE KWA KUTOA HATI MILIKI ZA KIMILA

Mwenyekiti wa halmashauri ya iringa Stephen Mhapa akiwa na mkurugenzi wa mradi wa feed the future Malaki Msingwa wakati wa kukabidhi hati miliki za kimila kwa wananchi wa kijiji cha Magubike kilichopo kata ya Nzii mkoani Iringa 
Mwenyekiti wa halmashauri ya iringa Stephen Mhapa akiwa na mkurugenzi wa mradi wa feed the future Malaki Msingwa wakimkabidhi hati mmoja wa wananchi wa kijiji cha Magubike
Mwenyekiti wa halmashauri ya iringa Stephen Mhapa akiwa na mkurugenzi wa mradi wa feed the future Malaki Msingwa wakicheza nyimbo za asili pamoja na wananchi wa kijiji cha Magubike wakati wa ugawaji wa hati za kimila



NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Migogoro ya ardhi katika kijiji cha magubike kata ya nzii wilaya ya iringa imebakia kkama historia baada ya mradi wa feed the future (LTA) kufanikiwa kupima ardhi na kuwakabidhi hatimiliki ya kimila kwa wananchi wa kijiji hicho.

Akizungumza wakatika wa kukabidhi hati hizo za kimila mwenyekiti wa halmashauri ya iringa Stephen Mhapa alisema kuwa kutolewa kwa hatimikili za kimila kunamaliza migogoro ya ardhi kwa wananchi wote waliopata hati hizo.

“Sasa tunaelekea kipindi cha kilimo ambapo ndio kuna kesi nyingi za mipaka ya ardhi, hivyo uwepo wa mradi huu wa LTA umetusaidia kumaliza kabisa migogoro ya ardhi naomba kuchukua nafasi hii kwa niaba ya serikali kuwashukuru kwa kazi mliyoifanya” alisema Mhapa 

Mhapa aliwaomba viongozi wa mradi wa LTA kuhakikisha wanapima vijiji vyote vya halmashauri ya wilaya ya Iringa ili kuondoa migogoro yote ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya wananchi.

“Kama serikali ikisema ipime ardhi yote ni kazi nzito,kazi hii ilitakiwa kufanywa na serkali kutokana na ukosefu wa rasilimali fedha na rasilimali watu imekuwa tatizo kubwa kwa serikali hivyo lazima mpongezwe kwa kazi yenu mnayoifanya” alisema Mhapa

Aidha Mhapa alisema kuwa kutolewa ka hati miliki za kimila zinaondoa kabisa mfumo dume kwa kuwa kwa sasa wanawake nao wamepewa hati kutoka kwa waume zao.

“Akina mama walikuwa hawatambuliwi kutokana na mila zetu zilivyo lakini hii leo kupitia mradi wa feed the future (LTA) wanawake hii leo wanamiliki ardhi na kuondoa kabisa mfumo dume kwenye sekta ya ardhi na kuwa na maamuzi ya matumizi ya ardhi yao” alisema Mhapa

Mhapa aliwataka wananchi wa kijiji cha Magubike wazingatie kuzitunza hati miliki za kimila kwa kuwa sasa ni dhamana ya maisha yetu hivyo mnatakiwa kuwa makini kwa kuzitunza vilivyo hati hizo.Naye naibu mkurugenzi wa mradi wa feed the future Malaki Msingwa amesema kuwa kupatikana kwa hati hizo kunawakuwa na uhakika wa kumili ardhi ambayo huwezi kusumbuliwa na mtu yeyote Yule.

“mradi huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kutoa Hati kwa usawa Wanawake na Wanaume” alisema Msigwa.Msigwa aliwapongeza wataalamu wa mradi huo kwa kuhakikisha wanawasaidia wananchi wa kijiji cha Magubike kupima maeneo yao na kupata hati miliki za kimila ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwenye maendeleo ya kiuchumi.


“Baadhi ya miradi imeibuliwa wakati wa upimaji wa ardhi hivyo ni fursa sasa kwa wananchi wenyewe kuitumia vizuri ardhi waliyopimiwa na kupewa hati miliki za kimila na kwa kuwa asilimia fulani kijiji hiki kimepimwa hivyo wanaweza kuwa kijiji cha mfano kwa kuwapa maendeleo hata wawekezaji wazuri kwa faida yao” alisema Msigwa

Msigwa alisema kati ya vijiji hivyo 41 vitakavyotayarishiwa mipango ya matumizi bora ya ardhi na kila mwenye ardhi kupimiwa na kupewa hati miliki za kimila, vijiji 36 vipo wilayani Iringa na vitano vipo wilayani Mbeya.

“Baada ya kukamilisha zoezi la upimaji mashamba na urasimishaji wa kijiji chote cha Lupembelwasenga, hivi sasa mradi unaendelea na upimaji mashamba katika vijiji vya mradi ambavyo vipo wilayani Iringa” alisema Msigwa

No comments: