Wednesday, December 12, 2018

MAHAFALI YA MRADI WA MALEZI NA MAKUZI KWA WATOTO (PLAY LAB) YAFANA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


MRADI wa malezi na makuzi kwa watoto (Play lab Program) wamefanya maadhimisho ya mahafali ya pili ya watoto kwa mwaka 2018 uliotekelezwa na Shirika la Brac Tanzania na jumla ya watoto 1200 wamefanikiwa kumaliza mafunzo hayo.

Mradi huo wa malezi na makuzi kwa watoto hujifunza kupitia elimu ya malezi kwa wazazi, ulinzi na usalama kwa watoto.

Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke John Bwana amesema elimu waliyoipata watoto hawa ni msingi mkubwa katika kuwaandaa na elimu ya awali na wenine shule ya Msingi ambapo imetia chachu katika kuwaimarisha watoto katika maendeleo ya kiakili , kimwili, kihisia na lugha.

John amesema, kupitia mradi huu wazazi wa watoto wamepewa mafunzo ya malezi kwa watoto wao kwani ni muhimu sana kwa sababu msingi wa ukuaji  wa motto huanzishwa na mzazi mwenyewe.

Pia. Amesema wazazi wamekuwa mstari wa mbele katika kushiriki kazi mbalimbali za mradi kama utenenezaji wa vifaa vya asili kwa ajili ya watoto kutumia katika mafunzo yao na hii imesaidia katika kuwajenga watoto wetu kuwa na ujasiri , ukakamavu, kujiamini, kuchangamana na watoto wengine , kuwa na nidhamu bora na hata kuwa na msaada kwa wazazi wake.

Aidha, ameishukuru Brac Tanzania kwa kuleta mradi huu unaomalizika 2020 kwa kuweza kuwapatia fursa ya elimu ya makuzi nna malezi kama msini katika maandalizi ya elimu ya awali na msingi,.

Kwa upande wa Mtathmini wa mradi wa malezi na makuzi unaosimamiwa na Brac Tanzania Lilian Josephat amesema kuwa jumla ya watoto 1200 wa miaka 3-5 wamefanikiwa kupata mafunzo hayo na wengine kuanza elimu ya awali au msingi.

Amesema jumla ya michezo 232 imeweza kutumika kufundishia mafunzo hayo katika masomo ya sayansi, hesabu, kuandika, sanaa, kusoma na michezo huru kwa watoto hao ndani ya miaka miwili ya mafunzo.

Lilian amesema, mradi huu ulianza mwaka 2016 na unamalizika 2020 ila mpaka kufikia sasa jumla ya wafaidikla wa mradi huo ni Miloni 3.4 katika Nyanja mbalimbali za mafunzo kwa vitendo.

Aidha ameeleza kuw Brac imeweza kutoa elimu ya sekondari kwa wasichana 114 na kati yao 80 wamefaulu elmu hiyo, huku watoto 1050 wamemaliza elimu ya awali na 1024 kufanikisha kuingia darasa la kwanza.

Wasichana 4282 wamefanikiwa kupatiwa elimu ya stadi za kazi na maisha kwa mkoa wa Tanga kupitia Shirika la Brac nchini, wasichana 1985 wakipatiwa elimu ya ujasiriamali na vifaa huku wasichana 4000 wakipata mafunzo ya elimu ya afya ya uzazi.


Katika mahafali hayo Kaimu Mkurugenzi aliweza kukabidhi vyeti na zawadi ya madaftari kwa watoto waliomaliza mafunzo hayo na kuwataka waendelee kujifunza na kuacha matendo yasiyo mema. Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke John Bwana akitoa vyeti kwa watoto waliohitimu mafunzo ya malezi na makuzi (play lab) unaoratibiwa na Shirika la Brac Nchini wakati wa mahafali ya pili yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Mtathmini wa mradi wa malezi na makuzi (play lab) Lilian Josephat akitoa risali wakati wa maadhimisho ya mahafali ya pili ya watoto kwa mwaka 2018 uliotekelezwa na Shirika la Brac Tanzania na jumla ya watoto 1200 wamefanikiwa kumaliza mafunzo hayo.Watoto wakiwa katika matukio tofauti.

No comments: