Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Bw. Jabir Shekimweri akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge wakati wa hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akizungumzia mambo yatakayofanyika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani ikiwemo wiki ya maonesho itakayoenda sambamba na kuanzishwa kwa jiji cha vijana ndani ya uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma ambapo vijana watajifunza masuala mbalimbali ikiwemo Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Upimaji wa Virusi vya UKIMWI, Ushauri nasaha, upimaji wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama shinikizo la damu na kisukari .
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI (UNAIDS) hapa nchini Dkt. Leo Zekeng wakati wa hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI (UNAIDS) hapa nchini Dkt. Leo Zekeng akizungumzia hali ya UKIMWI Duniani ambapo alibainisha kuwa takribani watu milioni 37 wameambukizwa virusi hivyo, hayo yamejiri leo wakati wa hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Bw. Jabir Shekimweri (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya wananchi walioshiriki katika wa hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI.
Kikosi cha Bendi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikiongoza matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI kwa lengo la kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF).
Sehemu ya washiriki wa matembezi ya hisani yaliyolenga kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF) , matembezi hayo ya hisani yamefanyika Jijini Dodoma.
Mmoja wa wasanii walioshiriki katika hafla ya uchangiaji fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF) , Bi. Hadhara Charles akionesha umahiri wake katika kumiliki mpira wa miguu wakati wa hafla hiyo iliyotanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia UKIMWI na Madawa ya Kulevya Mhe. Oscar Mukasa ambaye ni Mbunge wa Biharamulo akizungumzia faida za wananchi na wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania leo Jiji Dodoma wakati wa hafla ya kuhamasisha na kuchangia mfuko huo, hafla hiyo ilitanguliwa na matembezi ya hisani.
Msanii wa Jijini Dodoma Bi. Judith Jenaro akiimba wimbo wa kuhamasisha wananchi kujitokeza kupima virusi vya UKIMWI ili watambue hali zao ili waweze kuchukua hatua stahiki.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Bw. Jabir Shekimweri (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu wanafunzi walioshiriki katika hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia UKIMWI na Madawa ya Kulevya Mhe. Oscar Mukasa (Kushoto) ambaye ni Mbunge wa Biharamulo akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI (UNAIDS) hapa nchini Dkt. Leo Zekeng mara baada ya hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF).(Picha zote na MAELEZO na TACAIDS)
…………………………………………………………
Wananchi na Wadau wa Maendeleo wamehamasishwa kujitokeza kuchangia fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF) ili kujenga uwezo na kuongeza mapambano dhidi ya ugonjwa huo ambapo takribani milioni 15 zimechangishwa katika hafla iliyofanyika leo Jijini Dodoma ikitanguliwa na matembezi ya hisani.
Akizungumza leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge , wakati wa hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri amesema kuwa kuna umuhimu Mkubwa wakuchangia mfuko huo ili Taifa liweze kujitegemea katika kuendeleza mapamabano dhidi ya UKIMWI.
” Tuwe wepesi kuchangia mfuko huu kupitia namba 0684909090 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kupambana na UKIMWI hapa nchini”; Alisisitiza Mhe. Shekimweri
Akifafanua amesema kuwa kuna haja ya kuweka mikakati ya pamoja katika mapambano dhidi ya UKWIMWI hapa nchini ikiwemo kuangalia namna bora yakuwaelimisha vijana hasa walio mashuleni kwa kutumia mbinu za kisasa. Aliongeza kuwa, Kwa sasa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI katika mkoa wa Dodoma yameongezeka kutoka asilimia 2.5 hadi asilimia 5 mwaka 2017 hali inayotaka mikakati zaidi ikiwemo udhibiti wa nyumba za kulala wageni na elimu kwa makundi maalum kama wanafunzi wa Shule na Taasisi za elimu zilizopo katika mkoa huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibi Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko amesema kuwa matembezi yaliyofanyika ni sehemu ya matukio yatakayofanyika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani.Matukio menegine yatakayofanyika ni pamoja na wiki ya Maonesho ya UKIMWI itakayoenda sambamba na ushauri nasaha na upimaji, mafunzo ya ujasiriamali, Kongamano la wataalamu wa Sayansi na wiki ya Vijana.Aliongeza kuwa Vijana ni kundi ambalo linatakiwa kutumia fursa ya maadhimisho hayo kupata elimu kuhusu masuala ya UKIMWI.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI Dkt. Leo Zekeng amesema kuwa kwa sasa Dunia ina takribani watu milioni 37 wanaoishi na Virusi vya Ukimwi na sehemu kubwa wakiwa wanaishi katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Akifafanua amesema kuwa Shirika hilo liko tayari kuendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya UKIMWI.
Siku ya UKIMWI Duniani inaadhimishwa kila Novemba Mosi kila mwaka ikilenga kuhamasisha wananchi na wadau kushirikiana katika mapambano hayo, ” Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni Pima Jitambue, Ishi”; Maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika Jijini Dodoma ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
No comments:
Post a Comment