Na Stella Kalinga, Simiyu.
Kuelekea
katika kipindi cha maandalizi ya bajeti ya mwaka 2019/2020 wito
umetolewa kwa Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani Simiyu na maeneo
mengine kote nchini kuyapa kipaumbele masuala ya Lishe katika mipango na
bajeti za Halmashauri zao, ili kukabiliana na tatizo la udumavu kwa
watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.
Wito
huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Sera, kutoka Ofisi ya Raisi
TAMISEMI, Bw.Eleuter Kihwele wakati mafunzo maalum yaliyotolewa kwa
baadhi ya viongozi na maafisa Lishe, katika kikao cha Maandalizi ya
Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020
kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.
Kihwele
amesema takribani asilimia 34 ya watoto wenye umri chini ya miaka
mitano nchi nzima wana udumavu, hivyo ipo haja ya kutilia mkazo suala la
lishe ili kutoathiri maendeleo ya ukuaji wa watoto, uwezo wao wa
kufikiri na maendeleo yao kitaaluma(shuleni).
“Asilimia
34 ya watoto wa nchi nzima wenye umri chini ya miaka mitano wana
utapiamlo, suala hili linaathiri sana watoto, mfano matokeo yao shuleni
na uwezo wa kufikiri, ndio maana serikali imeweka lishe kama kipaumbele
na Ofisi ya Rais TAMISEMI kama wasimamizi tunapita kwenye Halmashauri
nchi nzima kuhamasisha uzingatiaji wa masuala ya lishe katika bajeti ya
mwaka 2019/2020” alisema
Ameongeza
kuwa katika mafunzo yanayotolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa Viongozi
pia yamelenga kuwakumbusha juu ya utekelezaji wa vipengele vya
mikataba ya afua za lishe iliyosainiwa katia ya Wakuu wa Mikoa na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI na kutenga shilingi 1000 kwa kila
mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano katika bajeti zao.
Naye
Afisa Lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bi. Mariam Nakuwa ametoa
wito kwa Halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya masuala ya lishe kwa
kuzingatia miongozo na kuhakikisha fedha zinazotengwa zinatumika katika
shughuli zilizopangwa ili kuondokana na tatizo la utapiamlo
Aidha,
Bi. Mariam amesema pamoja na kukabiliana na tatizo la utapiamlo fedha
hizo zielekezwe katika huduma za utoaji wa virutubisho vya nyongeza kama
vile virutubisho vya Vitamini A na vidonge vya kuongeza wekundu wa damu
kwa akina mama wajawazito.
Kwa
upande wake Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini aliwasisitiza
Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani Simiyu kuyachukulia masuala ya lishe
kama kipaumbele, huku akiwataka kuhakikisha wanafanya vikao vya kamati
za lishe za wilaya kila baada ya miezi mitatu kama ilivyoanishwa katika
miongozo.
Diwani
wa Kata ya Dutwa Mhe.Mapolu Mkingwa akizungumza kwa niaba ya
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe.Richard Buyamba
amesema maelekezo na mafunzo waliyoyapata watayapelekea katika Mabaraza
ya madiwani na kuhakikisha mipango na bajeti zinazopitishwa zinazingatia
umuhimu wa afua za lishe.
Mkuu
wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe amesisitiza viongozi na
watendaji wakiwemo wajumbe wa kamati za lishe kubadilika na kuachana na
mazoea katika kufanya ufuatiliaji na kutekeleza mipango ya masuala ya
lishe badala yake wafanye kazi kulingana na miongozo ili kuwa na matokeo
mazuri katika masuala ya lishe.
Timu
ya Wataalam kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI ipo katika ziara ya
kuhamasisha Viongozi katika Halmshauri na Mikoa kuzingatia vipaumbele
kwenye maeneo ya lishe na kupanga mipango ya bajeti inayojibu changamoto
za lishe, ili kufikia malengo ya mikataba ambayo Wakuu wa Mikoa
walisaini na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwenye usimamizi wa
afua za lishe katika maeneo yao.
Mkurugenzi
Msaidizi Sera, kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI, Bw.Eleuter Kihwele
akizungumza na baadhi ya viongozi na Wataalam Lishe wa mkoa wa Simiyu,
katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani
Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12,
2018.
Afisa
Lishe kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI, Bi. Mariam Nakuwa akiwasilisha
mada kuhusu mipango na bajeti ya masuala ya lishe Mkoani Simiyu kwa
baadhi ya viongozi na Wataalam Lishe wa mkoa wa Simiyu, katika kikao
cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe kwa mwaka 2019/2020
kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akisisitiza jambo katika
kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu
kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI katika Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Bw. Kai.B. Mbaruk akizungumza na baadhi ya viongozi na
Wataalam Lishe wa mkoa wa Simiyu, katika kikao cha Maandalizi ya Mipango
ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020
kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018 wakati akiwa katika ziara
ya kikazi mkoani Simiyu.
Mkuu
wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani akichangia hoja katika
kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu
kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018
wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu.
Diwani
wa Kata ya Dutwa Mhe.Mapolu Nunde Mkingwa akichangia hoja katika kikao
cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa
mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018, ambapo
alimwakilisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi,
Mhe.Richard Buyamba.
Mkuu
wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt.Seif Shekalaghe akichangia hoja katika
kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe kwa mwaka
2019/2020 Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.
No comments:
Post a Comment