Monday, November 19, 2018

WAHUKUMIWA MIAKA 20 KWA KUKUTWA NA VIPANDE VITANO VYA MENO YA TEMBO NA UHALIFU

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewahukumu wakulima wawili na mfanyabiashara mmoja kutumikia kif ungo cha miaka 20 gerzani baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na vipande vitano vya meno ya tembo na kuongoza uhalifu.

Washtakiwa waliohukumiwa ni Amiri Fransis (44),  mkulima Mkazi wa Tanga, Jairab Rashid (33), mkulima na Ibrahim Mkande (30) ambaye ni mfanyabiashara.

Hukumu hiyo imesomwa leo Novemba 19 mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa Jamhuri uliowasilishwa mahamani hapo pamoja na vielelezo vinne ikiwemo hati ya tathimini ya nyara za Serikali.

Hakimu alisema washtakiwa walikuwa wanatuhumiwa na makosa mawili ya kuongoza mtandao wa kiarifu na kukutwa na nyara za Serikali, Mahakama imewakuta na hatia, ambapo watatumikia kifungo cha miaka 20 jela.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu Shaidi amesema, makosa haya ni makubwa sana, yanapelekea kuharibu utalii wa Taifa zima."Nyie ni wabinafsi sana m nataka kujinufaisha kibinafsi kwa Mali ambazo zinasaidia Taifa zima" amesema Hakimu Shaidi.

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Hakimu Shaidi aliuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote la kusema dhidi ya washtakiwa, ambapo wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde alisema hawana kumbukumbu zote za nyuma za washtakiwa, lakini ameiomba Mahakama kutoa adhabu Kali kwa washtakiwa ili iwe fundisho kwao  kwa wengine ambao wanaingilia na kuharibu utalii wa Taifa.

Katika kesi hiyo upande wa mashtaka uliwasilisha vielelezo ambavyo ni meno ya tembo, hati ya kukamatia mali, hati ya tathimini ya nyara hizo na maelezo ya onyo.Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, washtakiwa walisema hawajaridhika na hukumu hiyo na mbapo wanatarajia kukata rufaa, Mahakama Kuu.

Katika kesi hiyo inadaiwa kati ya Januari 15 na 22, 2016, wakiwa maeneo ya mbali mbali ya Jiji la Dar es Salaam na Manyara washtakiwa waliongoza mtandao wa kiuhalifu kwa kupokea, kusafirisha na kuuza vipande vitano vya meno ya Tembo bila kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Pia inadaiwa Januari 22, 2016 washtakiwa wakiwa walikamatwa na vipande vitano ya vya meno ya tembo, vya uzito wa kilogramu 7.9, vyenye thamani ya USD 30,000 ambazo ni sawa na Sh milioni 65.6 bila kibali.

Akizungumza nje ya mahakama, Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amesema, kwa upandw wa mashtaka wameridhishwa na hukumu ya Mahakama kwani uamuzi huo ni ushindi katika vita vya kupambana na Maliasili.

No comments: