Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok na Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Grayson wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa duka jipya la vifaa vya Samsung Posta jijini Dar es salaam leo kulia ni Abraham Okore Mkuu wa Usambazaji Samsung na kushoto ni Suleiman Mohammed Meneja Mkazi wa Samsung.
Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok na Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Grayson, , Abraham Okore Mkuu wa Usambazaji Samsung na Suleiman Mohammed Meneja Mkazi wa Samsung wakiingia dukani mara baada ya kukata utepe wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Graysonmara baada ya kuzinduliwa kwa duka hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok akifuatana na Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Graysonwakati akitembelea duka hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Grayson kuhusu mashine ya kufulia moja ya vifaa vya kielektroniki vinavyopatikana katika duka hilo kulia ni Abraham Okore Mkuu wa Usambazani Samsung.
Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok akiangalia moja ya simu za Samsung zinazopatikana dukani hapo kulia ni Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Grayson na katikati ni Bw. Abraham Okore Mkuu wa Usambazaji Samsung.
Baadhi ya wananchi mbalimbali wakiwa wamejitokeza katika uzinduzi wa duka hilo.
Suleiman Mohammed Meneja Mkazi wa Samsung akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok akizungumza wakati wa uzinduzi hui uliofanyika leo Posta jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Grayson akizungumza katika uzinduzi huo.
....................................................................................................
*Viongozi wazungumzia ubora wa bidhaa zao, waipongeza Serikali
*Watakaonunua bidhaa kwao kuingia kwenye droo kila siku
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
DUKA kubwa la kisasa linaouza bidhaa za aina mbalimbali za Samsung zenye viwango vya hali ya juu katika ubora limefunguliwa Posta katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Uzinduzi wa duka hilo umefanyika leo Desemba 24 mwaka 2018 ambapo viongozi wa ngazi mbalimbali wa kampuni ya Samsung ndani na nje ya Tanzania pamoja na baadhi ya wananchi wa Jiji hilo wameshuhudia uzinduzi huo uliokwenda sambamba na punguzo la bei pamoja na droo mbalimbali za kujishindia zawadi kwa wanaonunua bidhaa zao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo lililopo jengo la Askari Posta Mpya jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Grayson amesema Samsung ni bidhaa kubwa duniani na yenye ubora wa uhakika.
“Tumeamua kufungua duka hili eneo la Posta mpya jijini Dar es Saam kwa ajili ya kuhakikisha bidhaa zetu zinapatikana kwa urahisi na gharama nafuu.Hatutaki watu wanaohitaji bidhaa za Sumsung wasumbuke kuzipata.
“Tunayo maduka mengi nchini ikiwemo jijini Dar es Saalam lakini umuhimu wa duka hili unatokana na ukweli kwamba kuna bidhaa zote za Samsung ambazo mteja anahitaji kununua kutoka kwetu,”amesema.
Amefafanua uzinduzi huo unakwenda sambamba na punguzo la bei la asilimia tano kwa watakaonunua bidhaa kwa siku ya leo ambapo pia wataingia kwenye droo ambapo mshindi atashinda luninga ya Samsung yenye inchi 24 kila siku.Pia kutakuwa na droo ya kila wiki.
“Ili kuingia kwenye droo hiyo mteja wetu baada ya kununua bidhaa ya Samsung atatakiwa kuhakikisha anasajili.Jinsi ya kusajili ;kwenye uwanja wa kutuma sms andika neno sajili *serial No#tuma kwenda 15685.Utapata tisheti ya buree pindi unaponunua na kujisajili na utaingia kwenye droo ya kushindania Samsung TV 24”,amesema.Kwa upande wake Meneja Mkazi Tanzania wa Samsung Suleiman Ahmed amewahakikishia Watanzania katika duka hilo bidhaa zote za Samsung zitapatikana.
Kuhusu ubora wa bidhaa zao amesema wamekuwa wakiuza bidhaa ambazo ni bora na zenye uhakika na hiyo imewafanya bidhaa zao kuaminika na kukubalika.Ameelezea namna ambavyo Samsung wanafurahishwa na hatua ambazo Serikali inachukua katika kuhakikisha bidhaa zinazoingia nchini zinakuwa na ubora huku akishauri wanaotaka kununua bidhaa zao ni vema wakafika kwenye maduka yao.
“Serikali imefanikiwa kudhibiti bidhaa zisizo na ubora kwa kiwango kikubwa.Hata hivyo nishauri ni vema wanaohitaji kununua bidhaa zetu wakafika kwenye maduka yetu likiwemo na hili ambalo tumelizindua leo,”amesema Ahmed.
Wakati huo huo Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok amesema wanayo maduka mengi lakini duka hilo la Posta Mpya jijini Dar es Salaam ni muhimu zaidi kutokana na aina ya bidhaa ambazo wanauza kwa ajili ya wateja wao.
No comments:
Post a Comment