Friday, November 16, 2018

NHC YAWATAKA WALIOPEWA HATI MRADI WA SAFARI CITY KUANZA UJENZI ILI HUDUMA ZIWAFIKIE

Mkurugenzi wa shirika la nyumba la taifa Dkt.Maulidi Banyani akiwa na Kaimu mkurugenzi wa Auwsa Mhandisi Humphrey Mwiyombela wakikabidhiana hati ya kiwanja na kibali cha ujenzi wa ofisi za AUWSA kwenye eneo la Safari City nje Kidogo ya jiji la Arusha Picha na mahmoud ahmad wa globu ya jamii Arusha.



Na Ahmed Mahmoud Arusha

Shirika la taifa la Tafa (NHC)Limewataka wale wote walikabidhiwa hati za viwanja walivyopewa katika la eneo la Safari City lililopo kata ya Mateves nje kidogo ya jiji la Arusha kuhakikisha wanaendeleza maeneo yao ili kuhakikisha huduma muhimu za umeme na maji zinasogezwa katika mji huo mpya.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Hati ya umiliki wa eneo na kibali cha ujenzi kwa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira(AUWSA) iliyofanyika katika kata ya matever jijini hapa Mkurugenzi wa shirika la nyumba la taifa(NHC)Dkt.Maulidi Banyani amesema kuwa shirika hilo katika kuhakikisha linafikia malengo ya kusogeza huduma zake kwa jamii ya watanzania wa vipato vyote na kupunguza gharama za ujenzi kuendana na mazingira.

Ameeleza kuwa limeingia makubaliano na AUWSA na kuwapatia eneo lenye ukubwa wa squaremita elfu 13 kwa ;lengo la ujenzi wa ofisi kuu ya kanda,Karakana,Bohari na Kituo cha Taarifa za mita hatua hiyo itasaidia kupunguza tatizo la maji katika eneo hilo baada ya mamlaka hiyo kuonyesha nia ya kusogeza huduma hiyo kupitia mradi huo.

Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa AUWSA Mhandisi Humphrey Mwiyombela amelishukuru shirika la nyumba kwa kuwapatia eneo hilo nakuhaidi kujenga jengo lenye ukubwa wa ghorofa sita litakalotumika kama ofisi kuu ya kanda ambalo litafungwa mitambo maalumu ya kupokea taarifa za mbali mbali katika mtandao wao wa huduma za maji.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Auwsa Dkt Richard Masika amesema kuwa ujio wa mamlaka ya maji katika eneo hilo la safari City litakuwa ni mkombozi kwa jamii inayozunguka katika eneo hilo na maeneo ya jirani kwa kuwa kutakuwa na mtandao mabomba ya maji wawenye teknolojia mpya na hivyo kuondoa tatizo la maji katika eneo hilo na kuwa kituvu cha mradi huo wa billion 520 kwa kuboresha mawasiliano.

“sio tu kwamba tunaboresha mji wa Arusha bali tunapunguza changamoto ya msongamano na kila mwananchi anayo fursa ya kukimbilia kwenye eneo hilo kwa lengo la kupata huduma muhimu za maji sanjari na kuwa kwenye makazi bora nampongeza sana mwenyekiti wa bodi na mkurugenzi wa Shirika la nyumba kwa kuteuliwa kwao na kuwataka ushirikiano wao uendelee”alisema

Aidha katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Auwsa amesema kuwa ujio wa mradi huo ni faraja kwa mkoa huo na kuendelea kupanuka na kuondoa msongamano katika jiji la Arusha

Amezitaka taasisi zingine zikiwemo za serikali kama Polisi,Tarura Tanesco na idara ya Zimamoto kuiga mfano wa AUWSA kuja kuchukuwa maeneo kwa ajili ya ofisi na hivyo kuboresha makazi ya jiji la Arusha na kusogeza huduma kwa wananchi sanjari ambao wamekuwa na changamoto ya kutafuta huduma hiyo katikati ya jiji pekee hali inayowawiya vigumu pindi kunapotokea mahitaji ya huduma zao.

No comments: