Tuesday, November 13, 2018

MBIO ZA NAMTUMBO SELOUS MARATHON ZAFANA, DC KIZIGO ATOA NENO LA SHUKRANI KWA WATANZANIA ,WANARIADHA

Na Ripota Wetu ,Globu ya jamii

WILAYA ya Namtumbo mkoani Ruvuma imefanya Mbio za Namtumbo maarufu kama Namtumbo Selous Marathon ambapo wanariadha mbalimbali akiwamo Godefrey Masaki wa JKT Arusha walishiriki.

Katika mbio hizo Masaki alishinda kwa kushika nafasi ya kwanza baada ya kushinda mbio za kilometa 21 huku akimuacha Mohemed Dule kutoka kikosi cha KG Songea aliyesgika nafasi ya pili wakati nafasi ya tatu ikishikiliwa na Ostin Kinyunyu kutoka mkoani Njombe.

Pia kwa upande wa wanawake katika mbio hizo Magdalena Crispin kutoka Arusha ameibuka mshindi wa kwanza wa mbio za Kilometa 21 huku mkimbiaji machachari Fabiola John kutoka Jeshi la Polisi Dar es Salaam akiibuka mshindi wa pili na kumwacha Adelina Irasias kutoka Dar es Salaam akishikilia nafasi ya tatu.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mbio hizo Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Mfaume Kizigo aliyeshiriki mbio za kilometa 2.5 akivalia nambari 021 amewashukuru Watanzania hasa wanariadha walioshiriki mbio hizo kwa kujitokeza kwao kushiriki na kuhamasisha malengo ya mbio

“Nashukuru Mungu kuwa miongoni mwa walioshiriki mbio hizi na kumaliza kilometa mbili na nusu.Nawashukuru sana washiriki na Watanzania wote kwa kuja kutuunga mkono katika safari yetu ya kujenga maendeleo ya sekta ya afya,” amesema Kiziga. Pia amepongeza jitihada za wadhamini wa mbio hizo Mantra Tanzania na Uranium One kwa ushirikiano mzuri wanaouonesha kwa wana namtumbo na watanzania kwa ujumla.

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo akimvalisha medali ya dhahabu mshindi wa kwanza KM21 wa Namtumbo Marathon Godfrey John Masaki kutoka JKT Arusha,wemgine ni washindi wa pili na wa tatu
mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza KM21 wa Namtumbo Marathon Godfrey John Masaki kutoka JKT Arusha,  wengine ni washindi wa pili na wa tatu ambao pia walijinyakulia zawadi ya Fedha, Simu ya kisasa pamoja na medali.

Mshindi wa kwanza wa kike KM21 Magdalena Crispin (katikati) baada ya kukabidhiwa zawadi ya ushindi na Andrei Shutov(kulia) mwakilishi kutoka Uranium One Urusi, wa pili kutoka kulia ni mshindi wa pili Fabiola John na wa kwanza kushoto ni mshindi wa tatu Adelina Irasias. 

Picha ya baadhi ya Wanariadha mbalimbali walioshiriki Namtumbo Marathon.

No comments: