Saturday, November 24, 2018

MANYANYA AZIAGIZA TAASISI ZA UDHIBITI WA BIDHAA,CHAKULA NA DAWA NCHINI KUWA KARIBU NA WAJASIRIAMALI

Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Stella Manyanya akizungumza wakati akifungua maonyesho SIDO ya Kanda ya Kaskazini yanayoendelea kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Joyce Meru
 MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Stella Manyanya
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Joyce Meru akizungumza katika ufunguzi huo
Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Stella Manyanya kulia akipata maelezo kutoka kwa Banda la Tanga Fresh
Mjasiriamali akimuhudumia mteja wake kama alivyokutwa
Sehemu ya bidhaa mbalimbali zikiwa kwenye maonyesho hayo 
Sehemu ya wananchi wakiwa kwenye ufunguzi huo
NAIBU Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Stella Manyanya kushoto akigawa vyeti kwa washiriki wa maonyesho hayo 
NAIBU Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Stella Manyanya katikati akiwa kwenye picha ya pamoja



NAIBU Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Stella Manyanya ameziagiza taasisi za udhibiti wa bidhaa,chakula na dawa nchini kuhakikisha zinakuwa karibu na wajasiriaamali ili kuweza kuwasaidia badala ya kuwakamata kwa kigezo cha kutokufanya vizuri. 

Hayo ameyazungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Kanda ya Kaskazini ya SIDO alipokuwa akiwahutubia wajasiriamali hao na kusema wataalamu wa taasisi hizo wanapaswa kutoa elimu ya kuwajengea uwezo badala ya kutoza faini. 

Aidha alisema wajasiaramali wengi nchini hasa wadogowadogo bado hawajakuwa na uwelewa mpana wa namna ya kuweka mpangilio mzuri wa maswala mazima ya shughuli zao hivyo wanahitaji kuelimishwa. “Tunao wataalamu toka TBS,TFDA na taasisi nyingine za udhibiti lakini wanatakiwa kuelimisha zaidi badala ya kuwafungia baadhi ya wajasiriamali au kuwatoza faini na haya sio malengo ya Serikali”Alisema Manyanya. 

Manyanya alisema lengo la Serikali hadi kufikia 2025 kufikia katika uchumi wa viwanda jambo ambalo linahitaji nguvu ya ziada ikiwa pamoja na kuwaelimisha wajasiriamali hao na kuwawezesha kimitaji. Hata hivyo aliwataka wajasiriamali wote Nchini kuhakikisha wanaimarisha ubora wa viwango wa bidhaa zao wanazozalisha ili kuendana na ushindani wa soko na kuongeza ubunifu ili waweze kuuza katika nchi za Afrika Mashariki. 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Joyce Meru alisema Shirika hilo la kuhudumia viwanda vidogo nchini (SIDO) kwa mwaka 2017/2018 limefanikiwa kuwapatia mafunzo wajasiriamali 2605. Meru alisema mbali na kutoa mafunzo kwa wajasiriamali hao pia shirika hilo lilifanikiwa kutoa mkopo 2071 yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.37 ambayo ilitengeneza ajira za watu 3964. “Haya ni mafanikio kwetu kwa kutambua dhana ya serikali ya uchumi wa viwanda na tutaendelea kuwasaidia zaidi wajasiriamali hasa wale wadogowadogo”Alisema Meru. 

Aidha alisema Shirika linatekeleza program mbalimbali kupitia ofisi zilizopo mikoani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwa pamoja na mkakati wa wilaya moja bidhaa moja muungano wa viwanda vya wajasiriamali kwa kina mama. Hata hivyo aliwaomba wajasiriamali wanaojiweza kuwekeza katika vifungashio ili waweze kuwauzia wajasiriamali wadogowadogo ambao bado wanahangaika na bidhaa hiyo ya vifungashio. 

Naye Mkuu wa Wilaya Tanga Thobias Mwilapa alisema maonyesho yamekuwa na tija hasa Mkoa huo ambapo watu wengi wamenufaika na biashara zilizoonyeshwa ambazo ni matunda ya Watanzania. Mwilapwa alitumia fursa hiyo kuwaomba wajasiriamali hao kujitokeza kwa wingi kwenye maonyesho hayo ambayo yanawaongezea uwezo wa kuweza kuongeza thamani ya mazao na kuijiongezea kipato. 

No comments: