Thursday, November 29, 2018

MAJAMBAZI SITA SUGU WAUAWA DAR KWA KUPIGWA RISASI

*Wakutwa na mabomu ya kutupa kwa mkono, risasi 217,wamo Waburundi 
*Mambosasa ataja matukio ya kutisha yaliyofanywa na majambazi hayo

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limesema leo Novemba 29 mwaka huu maeneo ya Ubungo UFI jijini Dar es Salaam kupitia kikosi kazi maalum cha kupambana na ujambazi kimefanikiwa kuwaua majambazi sita.

Mbali na kuua majambazi hayo wamekamata silaha moja aina ya AK 47, risasi 11, kitambulisho chenye namba OP 0216239 kwa jina la Theophili Manirakiza mkazi wa Rukana Rugombo nchini Burundi na kitambulisho cha kazi kinachotumiwa na kikundi cha CNDD-FDD chenye jina hilo la Theopili Manirakiza katika majibizano ya risasi.

Kamanda Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amewaambia waandishi wa habari kuwa majambazi hao wameuawa baada ya mtego uliowekwa na askari kutokana na taarifa za watuhumiwa watatu waliokuwa wamekamatwa.

Amewataja watuhumiwa hao ni Willy Irakozes maarufu kwa jina la mandoo ambaye ni wa Burundi, Jean Mugisha raia wa Burudi na Mtanzania Omary Nassoro ambaye ni Mtanzania na kwamba walikuwa na bunduki tatu aina ya AK47 na magazine 8, risasi 217 na mabomu ya kutupa kwa mkono 8,ambao 

walipanga Novemba 29 mwaka huu saa 10 :30 alfajiri kufanya tukio la kumpora mfanyabiashara aliyekuwa akisafiri kuelekea Morogoro akisadikiwa kuwa na kiasi kikubwa cha fedha,Kamanda Mambosasa amesema watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kuwepo kwa matukio ya uhalifu yaliyotokea huko Mabibo External Novemba 3, mwaka 2018 ambapo 

mfanyabiashara wa Tigopesa/Mpesa aliporwa Sh.milioni 50 na huko Tegeta Novemba 15 mwaka huu mfanyabiashara raia wa China ambaye aliporwa 
Sh.milioni 10.

Pia imeelezwa kuwa jambazi Irakozes amekuwa akitafutwa kwa kufanya matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha hasa katika tukio la kuvamia Benki ya NMB Temeke ambapo aliua askari wawili .Pia Machi 15 mwaka 2011 akiwa anashikiliwa kituo cha Polisi Kagongwa Kahama kwa makosa mbalimbali yeye na wenzake walitoroka baada ya kuwaua askari 
polisi wawili na kutoroka na silaha mbili aina ya AK47. 

Mambosasa amesema matukio mengine waliyoshiriki ni pamoja na kuteka mgodi wa Tulawaka Geita mwaka 2011, kuvamia maduka ya kubadilishia fedha za kigeni huko Zanzibar.Pia mwaka 2012 walivamia kituo cha mafuta huko Kagera na kufanya mauaji, walivamia maduka yaliyopo karibu na kituo cha Polisi 

Chato na hivyo kukishambulia kituo ili kurahisisha uporaji ambapo walipora Sh.milioni tatu na mwaka 2010 walivamia mgodi wa Nyamongo na kufanya 
mauaji ya askari mmoja na kujeruhi wengine.

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kuwaua watu sita wanaosadikika kuwa Majambazi katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo huku miongoni mwa wahalifu hao akitambulika kuwa ni raia wa kutoka nchini Burundi akiwa na kitambulisho cha Chama cha CNDD-FDD.Pichani ni kamanda wa polisi wa kanda hiyo SACP LAZARO MAMBOSASA akizungumza na wanahabari.

No comments: