Monday, November 12, 2018

MAHAKAMA YAMPA NAFASI YA MWISHO MBUNGE MSIGWA KUTAFUTA WAKILI WA KUMTETEA

Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa nafasi ya Mwisho kwa Mshtakiwa Peter Msigwa ambaye in Mbunge wa Iringa Mjini kutafuta wakili wa kumtetea katika kesi ya uchochezi inayomkabili pamoja na viongozi wenzake nane wa Chadema ma sivyo, Mahakama itaendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo bila uwepo wa wakili wake.

Msigwa pia ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anatukanwa Kisheria na mawakili wa upande wa mashtaka kwa sababu mawakili wake wanajitoa kumtetea.Hatua hiyo imefikwa leo Novemba 12. 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuanza kwa usikilizwaji wa upande wa mashtaka ambao walidai mahakamani hapo kuwa wako tayari kwa kuendela na hatua hiyo na kwa leo walikuwa na shahidi mmoja.

Msigwa amepewa nafasi hiyo ya mwisho baada ya wawakili wake wawili waliokuwa wawili waliokuwa wakimtetea kujitoa kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa kesi.Mchungaji Msigwa ameeleza hayo baada ya wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi kudai kuwa inaonekana Msigwa amepanga njama ili mawakili wake wajitoe.

Kutokana na hatua hiyo, Msigwa alisimama na kueleza kuwa anaona Wakili wa Serikali kama anamtukana kisheria na kumnyanyapaa."Hakimu wewe ni shahidi mawakili wangu wamejitoa kwa sababu ya kutoridhishwa na mwenendo wa kesi, wakili wa serikali hana haki wala haimuhusu kuhusu mawakili wangu,"ameeleza.Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mashauri amesema ni haki ya Kikatiba kwa mshtakiwa kuwakilishwa na Wakili, lakini anatoa nafasi ya mwisho kwa Msigwa na akishindwa ataonekana amefanya makusudi na kesi itaendelea bila ya yeye kuwa na wakili

.Kesi imeahirishwa hadi November mshtakowa 23 2018. Msigwa ametakiwa siku hiyo kuwa na wakili.Mbali na Msigwa, washtakiwa wengine ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya, na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji, Esther Matiko na mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam.

No comments: