Sunday, November 18, 2018

KUNAMAFANIKIO MAKUBWA MKOANI MTWARA NDANI YA MIAKA 3 YA JPM-RC MTWARA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii, Mtwara

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, amesema ndani ya miaka mitatu ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli wamefanikiwa kupandisha kiwango cha Elimu na kuwaondoa wanyonyaji wa wakulima wa korosho maarufu kwa jina la 'Kangomba' Pamoja na kuimarisha huduma za Afya katika mkoa huo.

Byakanwa Amesema hayo leo Mkoani Mtwara alipokuwa akitoa Mukhtasari wa Mafaniko ya Serikali ya awamu ya tano katika sekta mbalimbali kwenye mkoa wa Mtwara.

"katika sekta ya elimu kulikuwa na dhana ya kuwa wanafunzi awapendi shule lakini tangu nimefika nimeweza kuweka mipango ya kuhakikisha kuwa elimu inakuwa katika hali sawa kwa kutengeneza mpango kazi ambao umeweza kusaidia kuongeza ufaulu kutoka mkoa wa Mwisho kitaifa mpaka kuwa mkoa wa nane kitaifa" amesema Byakanwa.

RC Byakanwa amesema kila mwalimu Mkuu amepewa mpango kazi hivyo Mimi sijapiga ngoma marufuku wala shughuli za kitamaduni hivyo nimewataka walimu watimize wajibu wao na kuacha kuwasingizia wakazi wa mtwara kwani walipoamua kufundisha ufaulu umeongezeka.

Katika hatua nyingine Rc Byakanwa amesema wameamua kusimamia zao la Korosho katika miaka hii mitatu lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha wanamnufaisha zaidi mkulima wa korosho pamoja na kuwaondoa watu hao ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakipata fedha haramu kupitia michezo hiyo.

RC Byakanwa amesema lazima wamlinde mkulima wa korosho ili aweze kunufaika na kuwaondoa watu hao, ambao sasa imeonekana ni utamaduni kwa wakulima wa korosho Mtwara."Ni kweli wapo watu hawa lakini inahitajia muda kuwaondoa kabisa kwa kuwa wanajibadilisha katika mfumo mbalimbali lakini wote ni Kangomba tu, ni lazima tuwaondoe," alisema.

Alisema hata malipo watakayokwenda kuwalipa wakulima wa korosho kuna uhakiki fulani unaofanyika na utaweza kuwabaini kangomba kwa kuwa ni vigumu kwa mkulima mdogo kulipwa zaidi ya milioni 40."Kupitia malipo haya tutajua tu na lazima watuonyeshe hayo mashamba, hivyo tunachofanya kwa sasa kuendelea kutoa elimu kwa wakulima pamoja na kuwa na 'data base' ya wakulima wote ili iwe njia nzuri zaidi ya kuondoa kangomba," alisema.

Mkuu huyo wa mkoa, amesema mbinu hizo ndio zitaweza kuzuia watu hao ambao anaamini wanakwamisha jitihada za mkulima pamoja na kuondoa tatizo la upotevu wa magunia ya korosho kwenye maghala mbalimbali yanayohifadhia."Haiwezekani korosho ipotee tu kwenye ghala halafu kusiwepo na hatua zozote, lazima taarifa itolewe na kila kitu kifuate utaratibu na hii lazima tulikomeshe," amesema.

RC Byakanwa amesema katika vitu ambavyo anajivunia katika mkoa wake ni ujenzi wa vituo vipya vya Afya vya Kisasa vilivyojengwa kwa muda mfupi na serikali ya awamu ya tano kwa kiasi cha fedha Bilioni 4.3 ambazo zimetumika kujenga vituo vya Afya.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Miaka mitatu ya mkoa huo katika serikali ya awamu ya tano
Sehemu ya Waandishi wa Habari walioshiriki Mkutano wa Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa Kuelezea Miaka mitatu ya Rais Magufuli

No comments: