Thursday, November 29, 2018

KAIRUKI KUWAKUTANISHA WAHITIMU WALIOSOMA CHUONI HAPO KUPITIA KONGAMANO KITAALUMA

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WATAALAMU wa afya ambao wamesoma katika Chuo kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU) wametoa mtazamo wao katika sekta ya afya huku wakijizatiti kupanua wigo wao katika kuimarisha sekta hiyo.

Wataalamu hao watakutana katika kongamano la kwanza la kitaaluma ambalo litafanyika kesho Novemba, 30 katika viwanja vya chuo kabla ya kufanyika kwa mahafali ya 16 yatakayofanyika mapema jumamosi wiki hii.

Akizungumza na waandishi wa habari Makamu mkuu wa chuo Profesa. Charles Mgone amesema kuwa kongamano hilo  litazinduliwa na katibu mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya ambapo wataalamu hao watajadili kuhusu  magonjwa yasiyoambukiza pamoja na UKIMWI. Aidha amesema kuwa kongamano hilo litawakutanisha wasomi waliosoma katika chuo hicho, wafanyakazi na wageni mbalimbali.

Kwa upande wake Naibu makamu mkuu wa chuo taaluma Profesa. Moshi Ntabaye amesema kuwa kuna vyuo vya afya 7 nchini na chuo chao kinachangia katika ufundishaji wa wataalamu wanaotakiwa kwenye sekta ya afya na kuhakikisha wanakuwa bora zaidi.

Aidha amesema kuwa wana mpango wa kujenga kampasi mpya katika eneo la Boko jijini Dar es salaam ili kuweza kuongeza uwezo wa kudahili wanafunzi wengi zaidi hasa madaktari na manesi ili kuweza kuimarisha sekta hiyo na wamewaomba wadau mbalimbali wa sekta afya kujitokeza kusaidia katika kufanikisha ujenzi wa kampasi hiyo ili kuweza kuimarisha sekta ya afya nchini.

Kwa upande wake Rais wa kongamano hilo Dkt. Leonard Malasa amesema kuwa kongamano hilo ni sehemu ya kusherekea zaidi ya miaka 20 ya hospitali hiyo huku wataalamu mbalimbali walisoma katika chuo hicho ambao wameanzisha taasisi mbalimbali za afya watatoa neno la kuwahamasisha wanafuzi chuoni hapo na hatimaye   zawadi kutolewa kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwa mwaka 2018.

Aidha amesema kuwa katika kongamano hilo wamiliki wa makampuni na taasisi za afya watapata fursa za kuonesha bidhaa zao na kutoa huduma kwa washiriki.Kuhusiana na mahafali yatakayofanyika jumamosi Makamu mkuu wa Chuo amesema kuwa jumla ya wanafunzi 230 watatunikiwa shahada za awali, uzamili, na stashahada uzamivu.

Amesema kuwa kati ya wahitimu 230 wanawake ni 126 na wanaume 
104 huku idadi ya madaktari ikiwa 153 idadi kubwa zaidi ukilinganisha na miaka iliyopita.

Pia Rais wa wanafunzi chuoni hapo Bernard Mutalemwa amesema kuwa wamefurahi sana kwa idadi kubwa ya madaktari watakaohitimu jumamosi kwa kuwa hitaji la madaktari ni kubwa zaidi.

Na kuhusiana na changamoto ya ajira Mutalemwa amesema kuwa madaktari wasibweteke kwani wanaweza kujiajiri kwa kuanzisha taasisi mbalimbali za afya na ametoa wito kwa Wizara na Serikali kuliangalia hilo ili kuweza kukuza na kuimarisha sekta ya afya nchini.
 Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki  profesa Charles Mgone katikati akizungumza na waandishi wa Habari wakati wakitambulisha kuwepo kwa kongamano la kwanza la kitaaluma la chuo hicho litakalifanyika kesho katika ukumbi wa chuo hicho jijini Dar ea Salaam. Mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarijiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee jinsia na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya. Kushoto kwake ni Ras wa Kongamano la kwanza la kitaaluma la Chuo cha Kairuki, Dr Leornad Malasa na kulia ni Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Bernad Mutalemwa.
 Naibu Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki Dr, Moshi Ntabaye wa kwanza Kushoto akizungumza na waandishi wa Habari hawapo pichani wakati wakitambulisha kuwepo kwa kongamano la kwanza la kitaaluma la chuo hicho litakalifanyika kesho katika ukumbi wa chuo hicho jijini Dar ea Salaam. Mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarijiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee jinsia na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya. Kulia kwake  Rais wa Kongamano la kwanza la kitaaluma la Chuo cha Kairuki, Dr Leornad Malasa akifuatiwa na profesa Charles Mgone na wa mwisho ni Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Bernad Mutalemwa.
Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki  Benard Mutalemwa (kulia) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wakitambulisha kuwepo kwa kongamano la kwanza la kitaaluma la chuo hicho litakalifanyika kesho katika ukumbi wa chuo hicho jijini Dar ea Salaam. Mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarijiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee jinsia na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya. Kushoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Kairuki profesa Charles Mgone, (Picha na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii)

No comments: