Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MTANDAO wa Jumia Tanzania umezindua rasmi kampeni kubwa ya mauzo ya mwaka inayojulikana kama BLACK FRIDAY inayolenga kuwawezesha watanzania kufanya manunuzi kwa ajili nya msimu wa sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya.
Black Friday imekuwa inafanya mauzo ya bidhaa tofauti kwa bei nafuu kutoka kwa wauzaji mbalimbali mtandaoni na kwa kupitia Jumia Tanzania itadumu kuanzia Novemba 16 hadi Desemba.
Akizungumzia uzinduzi wa kampeni hiyo ya Black Friday, Meneja Masoko wa Jumia Tanzania Albany James amesema kuwa, kwa kawaida Black Friday imekuwa inafanyika kila mwaka ifikapo Novemba 23, lakini kwa mwaka huu itakuwa kila Ijumaa na itaanzia Novemba 23 mpaka Desemba 07 mwaka huu.
James amesema, tofauti na siku za kawaida za Black Friday kutakuwa na ofa nyingi zaidi na mapunguzo makubwa ya bei kwa bidhaa zote mpaka kufikia asilimia 70 na hii katika kuhakikisha wateja hawapitwi kunufaika na maununuzi ya bidhaa kutoka kwa wafanyabiashara tofauti wanaoaminika kwenye mtandao wa Jumia."Ukiachana na ofa na mapunguzo ya bei, kutwakuwa na vocha za bure za manunuzi kuanzia shilingi 5,000 mpaka 80,000, mauzo ya bidhaa ya muda mfupi katika siku (flash sales) na kuogesha zaidi Black Friday kutakuwa na 'Treasure Hunt' kila Ijumaa ambapo bidhaa itafichwa kwenye mtandao wa Jumia," amesema James.
"Mteja mwenye bahati atakayefanikiwa kuitafuta na kuipata atauziwa kwa bei yenye punguzo la asilimia 99, na baadhi ya zawadi zitakazokuwepo kuanzia Ijumaa hii ni luninga ya kisasa yenye ukubwa wa inchi 32 inayouzwa kwa shillingi 570,000 mtandaoni na itafichwa na kuuzwa kwa 5,700 kwa mteja atakayeipata, "amesema.
Aidha, ameongeza kuwa lengo kuu la Jumia ni kuwawezesha watanzania kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali kwa urahisi na haraka mahali popote naa muda wowote walipo na mteja atakayenunua bidhaa kupitia Jumia itakayozidi thamani ya 200,000 atapelekewa bure mpaka alipo kwa mkoa wa Dar es Salaam.
Kwa upande wa washiriki wa Black Friday, Kutoka kampuni ya Skymark Meneja wa Kampuni hiyo, Nishit Modessa amesema kuwa wameamua kushirikiana na Jumia Tanzania baada ya kuona ni wazo zuri sana baada ya kuletewa na wakaamua kutoa pikipiki ili wateja wa Jumia washindanie.
Miodessa amesema, huu ni mwanzo wa ushirikiano wao ila wanategemea kuendelea kushirikiana nao zaidi katika kuuza bidhaa zao ambazo ni pikipiki na bajaji kupitia njia ya mtandao.
Meneja Masoko wa Jumia Tanzania Albany James akizungumzia uzinduzi rasmi wa kampeni kubwa ya mauzo ya mwaka inayojulikana kama BLACK FRIDAY inayolenga kuwawezesha watanzania kufanya manunuzi kwa ajili nya msimu wa sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya kupitia mtandao wa Jumia Tanzania, kulia ni Meneja Uhusiano wa Umma Jumia Tanzania Kijanga Geofrey.
Meneja wa Kampuni ya Skymark Nishit Modessa akielezea ushiriki wao kwa mara ya kwanza katika mauzo makubwa ya mwaka yanayofanyika kupitia kampuni ya Jumia Tanzania na kuamua kushirikiana nao kwa kutoa pikipiki na wateja washindanie, Kushoto ni Meneja Masoko wa Jumia Tanzania Albany James.
No comments:
Post a Comment