Monday, November 26, 2018

ITUMIENI FURSA YA MSAADA WA KISHERIA KUTAMBUA HAKI ZENU- PROF. KABUDI



Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akimpa mkono msanii Afande Sele baada ya kumaliza kutumbuza katika hafla ya ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria nchini uliofanyika mkoani Morogoro
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiangalia kitabu katika moja ya mabanda yaliyohudhuria uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria mkoani Morogoro , Prof. Kabudi alitembelea mabanda hayo baada ya kuzidua maadhimisho hayo mjini Morogoro
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza katika banda la Mahakama ambalo linashiriki maadhimisho ya wiki ya Msaada wa kisheria nchini ambayo ufunguzi wake kitaifa ulifanyika mkoani Morogoro uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria mkoani Morogoro
Wananchi waliofika kupata huduma ya msaada wa kisheria wakati wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria nchini katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe wakati wa uzinduzi wa wiki hiyo mjini Morogoro.
Wanasheria wa kujitegemea mkoani Morogoro katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe wakati wa uzinduzi wa maadhimisho y awiki ya msaada wa kisheria nchini uliofanyika mkoani Morogoro .
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe wakasalimia wananchi waliofika kuhudhuria uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria nchini uliofanyika mjini Morogoro.katika viwanja vya Shule ya Sekondari Morogoro

………………..

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amewataka wananchi kutumia fursa ya huduma za msaada wa kisheria ambayo inatolewa nchini ili kutambua haki zao na kuzipata kwa wakati.

Amesema wananchi wakiitumia huduma ya msaada wa kisheria itawawezesha kutambua haki zao na kuzipata kwa wakati , kufahamu sheria mbalimbali ikiwa ni pamoja na utaratibu unaotumiwa na Mahakama na hivyo kusaidia harakati za kupunguza msongamano Mahakamani. “Wananchi niwaombe mtumie fursa ya msaada wa kisheria ambayo Serikali imeridhia itolewe kwa wananchi wenye uhitaji, hii itasaidia kutambua haki zenu, kufahamu sheria na utaratibu unaotumika na Mahakama na hivyo kusaidia kupunguza msongamano Mahakamani” alisema Prof. Kabudi.

Prof. Kabudi amesema hayo mjini Morogoro alipokuwa akizindua maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria nchini ambayo inafanyika katika mikoa ya Morogoro, Singida, Tabora, Kagera na Kigoma kuanzia tarehe 26 Novemba hadi tarehe 30 Novemba ,2018. Amesema Wizara itaendela kutenga wiki moja kila mwaka kwa ajili ya kutoa msaada wa kisheria nchini ili kuhakikisha wananchi wengi wanafikiwa na huduma za msaada wa kisheia na hivyo kutimiza lengo la kutungwa kwa Sheria Na. 1 ya Msaada wa Kisheria ya Mwaka 2017.

Awali akizungumza katika ufunguzi hu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro DKt. Stephen Kebwe aliomba kupatiwa Mahakama mpya katika baadhi ya wilaya kama Mvomero na kupandishwa hadhi kwa baadhi ya Mahakama katika wilaya za mkoa huo ili kuwaondolea wananchi adha wanayoipata ya kufuata huduma hiyo kwa umbali mrefu. “Mhe. Waziri niombe kuongezewa Mahakama katika baadhi ya Wilaya kama Mvomero na Mahakama nyingine hasa za mwanzo zipandishwe hadhi na kuwa Mahakama za Wilaya ili ziweze kuwahudumia wananchi katika wilaya hizo,” alisema Dkt. Kebwe.

Maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria 2018 yanafanyika kwa kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi wenye uhitaji katika maeneo mbalimbali nchini, katika magereza , kutoa elimu ya sheria kwa umma ana kwa ana na kupitia machapisho.

No comments: