Monday, November 12, 2018

HATMA YA DHAMANA MWENYEKITI WA CHADEMA NA MBUNGE WA TARIME KUJULIKANA NOVEMBA 23,2018

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema Novemba 23.2018 itatoa uamuzi wa kumfutia dhamana ama la Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko baada ya wiki iliyopita kutoa amri ya kukamatwa kwa washtakiwa hao kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Hatua hiyo imekuja baada ya watuhumiwa hao kufika mahakamani wenyewe na kujieleza.

Akitoa maelezo yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, Mbowe amedai kuwa anaiheshimu mahakama sana na anatambua kama kiongozi na kama raia nafasi ya Mahakama katika kusimamia haki kwenye taifa.

Amesema, ni ukweli usiopingika kuwa yeye na washtakiwa wenzake ni viongozi na wana majukumu mengi ya kiungozi ya kutendaji ndani na nje ya nchi.

Mbowe ameeleza kuwa Oktoba 28, alisafiri kwenda Washington DC kwenye mkutano wa Oktoba 30, mwaka huu na kwamba kwa ratiba yake alistahili kuondoka huko Oktoba 30, usiku na kurejea Dar es Salaam Oktoba 31 kwa ajili ya kuendelea na Kesi Novemba Mosi, mwaka huu lakini bahati mbaya kabla hajaanza safari hiyo alipata matatizo ya ugonjwa ambapo kwa mazingira aliyokuwepo haikumruhusu kusafiri safari ndefu ya ndege kwa ushauri wa kitabibu na miiko ya kinachomsumbua.

Ameongeza, katika jitihada za kujaribu kupata Matibabu nchini Marekani zilikwamishwa na bima yake ya Matibabu ya kimataifa kwa sababu nilikuwa ikimruhusu kutibiwa katika nchi ambazo siyo Marekani wala ulaya bali inaruhusu atibiwe kati nchi za Afrika mashariki, Afrika Kusini na Dubai.

Amedai kufuatia hivyo, ilimlazimu kutafuta miadi kwenda kwenye Matibabu katika nchi za Emirate na kwamba hiyo ni kutokana na ushauri aliopewa mbali na bima, kutokana na utofauti wa Masaa kati ya matano iwapo atatoka alipo kwenda Dubai kwamatibabu na ni zaidi ya 24 iwapo angekuwa nchini.

Alidai kuwa alikwenda Dubai na kpata matibabu lakini Novemba 17, mwaka huu aliona taarifa mbali mbali zenye kupotosha kuhusiana na ugonjwa wake na Matibabu anapopata kwa ujumla.

Pia akaona Mahakama ilivyokwazika kutokana na kutokuwepo kwake na kwamba haikuwa rahisi kwa yeye kutuma taarifa za Matibabu kwa sababu bado wanaendelea namatibabu na kwamba taarifa ya ugonjwa ni siri ya mgonjwa na daktari.

Mbali na maelezo mengine mengi, Mbowe aliieleza Mahakama kuwa yeye ni mgonjwa wa moyo kwa miaka mingi na kwamba magonjwa wa moyo siyo homa na wala siyo ugonjwa wa majeraha ndiyo sababu wazungu wanauita "Silent Killer' Ni ugonjwa ambao unastahili ungalizi.

Pia aliwasilisha nyaraka zake za safari, za matibabu , Bima ya Matibabu kama uthibitisho mahakamani hapo.

Baada ya Mbowe kueleza hayo, Wakili wa Serikali Jacqline Nyantori alidai kuwa amemsilikiza Mbowe kwa umakini akiishawishi Mahakama isimfutie dhamana kwa kukiuka masharti ya dhamana, lakini mshtakiwa Mbowe na wenzake ni kama washtakiwa wengine wowote na kwamba kwa mujibu wa hati ya mashtaka inayowakabili walipaswa kufuata taratibu za Mahakama na masharti ya dhamana na amri walizopewa.

Wakili huyo aliendelea kudai kuwa mdhamini wa Mbowe wakati akitekeleza jukumu lake la udhamini alieleza kuwa Mbowe alikuwa ni mgonjwa Mahututi na alikimbizwa Afrika Kusini kwa Matibabu. Na kwamba kwa Maneno yamdhamini halo aliyokuwa nayo hakuweza hata kuzungumza.

Nyantori alidai kuwa Mahakama ilichukua Maneno hayo katika kumbukumbu za Mahakama na kuahirisha Kesi hadi Novemba 8, huku ikieleza uthibitisho wa kuumwa kwa Mbowe upelekwe mahakamani hapo.

Leo Mbowe anatueleza alikwenda Washington DC badala ya Afrika Kusini na  kwamba anatibiwa Dubai. Hii inaonyesha kuwa udanganyifu kutokana kutofautiana kwa mshtakiwa na mdhamini wake, alieleza Nyantori.

Hata hivyo Nyantori alitoa hati ya kusafiria ya Mbowe akionesha kuwa Novemba 7, alikuwa Dubai ambapo alitibiwa Novemba 8 na Novemba 2 Mbowe alikuwa Brussles Ubelgiji ambapo alitoka Novemba 6, ambapo aliingia Dubai.

Pia Nyatori, aliwasilisha hati ya kiapo kutoka kwa kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala Kamishna Msaidizi Salum Hamduni ambaye washtakiwa walipewa jukumu na Mahakama kuripoti kwake kila Ijumaa ya Kila wiki lakini mshtakiwa wa kwanza na wenzake hawakwenda kuripoti Polisi kama walivyotakiwa na Mahakama wakati walipewa masharti ya dhamana.

Pia aliwasilisha kiapo chaKamanda wa Uhamiaji Steven Mhina ambaye alimuhudumia Mbowe wakati akianza safari na kwamba alidai kuwa siku hiyo Mbowe alikuwa mzima na hakusindikizwa na wala hakuwa na msaada wa mtu yoyote

Baada ya kueleza hayo,Wakili Nyantori aliomba Mahakama iwafutie dhamana washtakiwa wote kwa sababu za uvunjifu wa masharti ya dhamana. Sheria ichukue mkondo wake na shauri liendelee kusikiliza.

Kwa upande wa mshtakiwa Esther Matiko alidai kuwa yeye hajawahi kuidharau mahakama na hatowahi.

Alidai Novemba 8 hakuwepo mahakamani alikuwepo katika ziara ya kibunge nchini Burundi ambazo nilikuwa Novemba 4 hadi 9, mwaka huu na kwamba ulikuwa ni muhimu na alikuwa akiiwakilisha nchi na alimtuma mdhamini wake kumuwakilisha mahakamani hapo akiwa nabarua na tiketi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 23, 2018 kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya. Kutolewa uamuzi kama dhamana dhidi ya washtakiwa ifutwe ama la.

No comments: