Monday, November 26, 2018

Dkt.Shein awasili Jijini Nairobi Kuhudhuria Mkutano wa Blue Economy.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Aliu Mohamed Shein, akimsikiliza Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Balozi Dan Kazungu kulia na kushoto Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dkt. Pindi Chana,baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nchini Kenya.akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli katika Mkutano wa Blue Economy unaotarajiwa kufanyika keshi Jijini Nairobi. katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mr. Dan Kazungu, wakiwa katika chumba cha VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta,leo jioni 26/11/2018, akihudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Blue Economy, utakaofanyika kesho Nchini Kenya.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiutambulisha Ujumbe wake kwa Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mr. Dan Kazungu,wakiwa katika chumba cha VIP baada ya kuwasili leo jioni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika chumba cha VIP katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nchini Kenya akiwa anahudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Blue Economy,kulia Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mr. Dan Kazungu na kushoto Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dkt. Pindi Chana. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dkt.Pindi Chana na anayefuata ni Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Balozi Dan Kazungu, alipowasili katika hotelini.Jijini Nairobi. 








Na.Suzan Kunambi. Nairobi..

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amewasili nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa uchumi endelevu wa bahari(Sustaniable Blue Economy Confrence) utakaoanza kesho katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta Jijini Nairobi Nchini Kenya.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi, Dk.Shein amepokelewa na viongozi mbali mbali wakuu wa Serikali ya Kenya wakiongozwa na balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kanzungu pamoja na Balozi wa Tanzania nchini humo Dk. Pindi Chana.

Katika ziara hiyo, Dk. Shein amefuatana na viongozi mbali mbali wa SMT na SMZ, akiwemo Waziri wa Kilimo Maliasili Mifungo na Uvuvi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma,Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe.Dk.Sira Ubwa Mamboya,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais Mazingira na Muungano Mhe January Makamba.

Mkutano huo Mkubwa unaohusu sekta ya uchumi wa bahari ni wa kwanza kufanyika nchini Kenya, ambao utawakutanisha wadau kutoka sekta mbali mbali kutoka nchi zilizoendelea na sinazoendelea kujadili namna bahari,maziwa na mito vinavyoweza kutumika katika kuimarisha uchumi wa nchi na dunia kwa ujumla.

Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Watu wa Kenya Mhe.Uhuru Kenyatta, ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein atatoa tamko la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Uchumi Endelevu wa Bahari, akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muunhano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Magufuli.

Mkutano huo utajadili maswala mbali mbali ya uchumi endelevu wa bahari na mchango wake katika kutekeleza Agenda ya 2030 ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa.vile vile washiriki wa mkutano huo watajadili hatua za utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika ,mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa wa mwaka 2015 wa Paris Ufaransa pamoja na mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari wa mwaka 2017 kwa ajili ya maendeleo endelevu pamoja na usalama na ulinzi baharini.

No comments: