Thursday, November 22, 2018

DC MURO ALETA SULUHU KWENYE MGOGORO WA KANISA ULIODUMU KWA TAKRIBANI MIAKA 13 ARUMERU



Baadhi ya Wachungaji na viongozi wa Makanisa ya Ameki nchini waliohudhuria ibada hiyo ya shukrani wakiwa na Baba askofu pamoja na makamu wa askofu katika ibada ya pamoja
Makamu wa Askofu wa kanisa la Ameki William Msafiri Ayo akizungumza katika Ibada hiyo ya Shukrani akiwashukuru kwa uvumilivu wao wa msukosuko wa kanisa ndani ya miaka 13
Makamu Askofu wa Kanisa la AMEKI William Msafiri Ayo Tanzania Baltazari Kaaya akishikana mkono Baba Askofu Baltazari Kaaya mbeke ya waumini wao kama ishara ya Amani ya kumaluza tofauti zao zilizodumu kwa takribani miaka 13
Askofu wa Kanisa la AMEKI Tanzania Baltazari Kaaya akishikana mkono na makamu wa askofu William Msafiri Ayo mbele ya waumini wao kama ishara ya Amani ya kumaluza tofauti zao zilizodumu kwa takribani miaka 13
Katibu mkuu mstaafu wa kanisa hilo Mchungaji Mshana akimshika mkono Baba Askofu Baltazari Kaaya kama ishara ya kutangaza Amani mara baada ya kumaliza tofauti zilizokuwepo ndani ya miaka 13
Baadhi ya mchungaji kutoka kanisa la Ameki akidhikana mkkono na Baba Askofu Baltazari Kaaya akimpongeza kwa hatua hiyo ya maridhiano.
Msaiduzi wa Askofu katika kanisa hilo la AMEKI akizungumza na waumini katika ibada hiyo ya kumshukuru Mungu kumalizika kwa mgogoro uliodumu kwa takribani miaka 13
Baadhi ya waumini katika kanisa la Ameki waliohuduria katika Ibada ya shukrani baada ya mgogoto huo uliodumu zaidi ya miaka 13 kumalizika
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza katika la AMEKI mara baada ya pande mbili hizo kuondoa tofauti zao na kuamua kuwa wamoja na uongozi mmoja
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro Akizungumza katika ibada hiyo ya shukrani katika kanisa la AMEKI ambapo yeye alikuwa chachu ya kusuluhisha pande zote mbili zikizokuwa na mgogoro ndani ya miaka 13
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akiteta jambambo na msaidizi wa Askofu katika kanisa la AMEKI katika ibada ya shukrani.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akimpongeza Baba Askofu wa kanisa la Ameki lililopo Wilayani hapo kata ya Usariva mara baada ya kuondoa tofauri zao na kutangaza Amani
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akimpongeza Makamu wa Askofu wa kanisa la Ameki lililopo Wilayani hapo kata ya Usariva mara baada ya kuondoa tofauri zao na kutangaza Amani
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akimpongeza Katibu mkuu mstaafu wa kanisa la Ameki lililopo Wilayani hapo kata ya Usariva mara baada ya kuondoa tofauri zao na kutangaza Amani


Na. Vero Ignatus, Arusha


Mgogoro uliodumu kwa takribani miaka 13 wa kanisa la AMEKI wilayani Arumeru kata ya Usariva umemalizika kwa pande mbili kukubaliana kwa kuondoa tofauti zao na kuamua kuwa na kanisa moja na uongozi mmoja

Akizungumzia mgogoro huo uliodumu kwa miaka 13 mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro amewapongeza viongozi kwa hatua kubwa waliyoifikia kwani kwa miaka yote hali ilikuwa nzito na mgogoro ulidumaza maendeleo ya kanisa ,ustawi wa wananchi,maendeleo ya shughuli za serikali katika wilaya hiyo.

"Mhe. Baba Askofu, Mhe. Msaidizi wa , Askofu nimesimama hapa kwa niaba ya serikali kuwapongeza kwa hatua kubwa mliyofikia, tumekuwa na changamoto za mgogoro uliodumu kwa miaka 13''alisema Jerry.Jerry amesema kuwa serikali itaendelea kusimama na kanisa la AMEKI kuwaunga mkono katika juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo sambamba na ukuaji wa kiroho na maendeleo ya waumini wao

'' Ndani ya miezi mitatu kama mkuu wa wilaya namshukuru sana Mungu kunifanya kuwa chachu ya kuwapatanisha viongozi hawa wa kanisa na leo wamekuwa wamoja na kanisa moja naamini sasa baraka zaungu zitaonekana''alisema Jerry .Sambamba na hayo amesema kwakuwa mgogoro umeisha,serikali inaanza kazi mara moja ndani ya wiki moja serikali itahakikisha kuwa inatatua changamoto zote ya maeneo yote ambayo yalikuwa ya kanisa

Nitangazia Arumeru,Arusha,Tanzania Afrika dunia ,Tanzania na Arusha kuwa mogoro uliodumu kwa takribani mika 13 sasa tumeumaliza umemalizika tukiwa wamoja na tukiendelea mbele kwa umoja wetu"alisema Jerry

Akizungumza juu ya mgogoro huo ulioligawa kanisa hilo Askofu Baltazari Kaaya amesema kuwa wameamua kuwa na maridhiano kwani ulisababisha kukosekana kwa amani na maendeleo yalidorora.Amesema kuwa waliamua kuwaita wawakilishi wawakristo na wachungaji wa pandezote mbili ili kuwajulisha kuwa wameshaungana ndipo baadae wakaamua kwenda kwa mkuu wa wilaya

Askofu amesema kuwa baada ya maridhiano hayo wamekubaliana wote kwa pamoja ndani ya miaka 4 kuunda katiba ya kanisa hilo."Tumeondoa tofauti zetu na tukaanza kupita sharikani nuongozi wote kwa pamoja tarehe 27.9.2018 tulikwenda usharika wa Ambureni na kuongeza ibada ya pamoja na washirika walifurahi sana kwani mgogoro wetu ulikuwa umewaathiri na wao pia" alisema askofu Baltazari

Kanisa la Ameki lilianzishwa mwaka 1995 ambapo lilimeguka kutoka Dayosisi ya Kaskazini kanisa la KKKT, mara baada ya kumeguka waliwezakufanya mkutano mkuu wa kwanza wa kumchagua mchungaji Abel Pallangyo(marehemu kwa sasa) kuwa kuwa askofu wa kwanza wa kanisa hilo. Mchungaji Mshana alichahaguliwa kuwa katibu mkuu wa kwanza, ikumbukwe kuwa kanisa hilo halikuwa moja ya vuguvuvu ya vurugu ya Dayosisi ya mlima meru bali ilichangia kuanzishwa kwa kanisa hilo.

Wakati makanisa mengine yakiwa na historia ya wamishionari kutoka nje ya nchi kanisa hilo linabakia kuwa na historia ya kuazishwa hapa nchini pasipokuwa na ufadhili kutoka wamishionari wa nje.Aidha kanisa hilo lilifanikiwa kufungua makanisa katika mikoa mbalimbali apa nchini ikiwemo Arusha ambapo ndipo makao makuu yalipo Kilimanjaro, Manyara, Kagera, Dar es salaam Tabora, na Manyara

Viongozi na waumini wa kanisa la Ameki, Wamemshukuru Rais Magufuli kwa kumpeleka mkuu wa wilaya Arumeru Jerry Muro kwani kwa ujio wake wilayani hapo wameshuhudia suluhu imepatikana kwa Amani.Wakati makanisa mengine yakiwa na historia ya wamishionari kutoka nje ya nchi kanisa hilo linabakia kuwa na historia ya kuazishwa hapa nchini pasipokuwa na ufadhili kutoka wamishionari wa nje

No comments: