NA K-VIS BLOG
BENKI mpya ya China Dasheng Bank Limited, inaanza kutoa huduma leo Jumatatu Novemba 26, 2018, jijini Dar es Salaam, ikiwa na mtaji wa kuanzia wa dola za kimarekani milioni 40 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 92, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya benki hiyo Bw. Yu Jiaqin amesema.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa benki hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Bw. Yu Jiaqin amesema benki hiyo ni benki ya kibiashara inayomilikiwa na makampuni sita ya serikali ya China yakishirikiana na makampuni binafsi kutoka mji wa Shanghai na Jiangsu.
Benki hii inalenga kutoa huduma kwa makampuni makubwa ya kichina yanayofanya miradi mbalimbali hapa nchini, lakini pia watanzania wanaofanya biashara na China ikizingatia makundi yote ya watu wenye kipato cha chini, cha kati na cha juu, alisema Bw. Jiaqin.
“Tutatoa huduma za bidhaa zote za kawaida za kibenki kama vile akaunti za akiba, akaunti za kudumu na za muda maalum, mikopo ya muda mfupi na muda mrefu na mikopo hii itatolewa kwa shilingi za kitanzania pamoja na fedha za kigeni.” Alibainisha Mwenyekiti huyo wa bodi.
Aidha Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bi Nunu Saghaf alishukuru Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kutoa leseni ya kufanya biashara kwa benki yake na kuahidi kuisaidia serikali ya Tanzania katika kufikia malengo yake ya uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.
"Makao Makuu ya China Dasheng Bank Limited, yatakuwa hapa jijini Dar es Salaam kwenye jingo la Ex-telecom, makao makuu ya kampuni ya TCCL barabara ya Samora, tunawakaribisha sana watu wote wanaohitaji huduma za kibenki." Alifafanua Bi. Saghaf.
Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Mhe.Wang Ke, alisema, kufunguliwa kwa benki hiyo hapa nchini ni ishara ya ushirikiano madhubuti na wa muda mrefu baina ya China na Tanzania na benki hiyo itaboresha huduma za kifedha na hivyo kuwa na manufaa makubwa kwa wafanyabiashara kutoka China na Tanzania.
China imefanya mageuzi makubwa sana ya kiuchumi kutoka umasikini na kufikia nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani na hili pia linawezekana kwa Tanzania, alisema balozi Wang Ke.Balozi huyo alisema, anaimani kubwa na uongozi wa juu wa benki hiyo ukiongozwa na mwenyekiti Bw.Yu Jiaqin kwani anao uzoefu wa muda mrefu wa shuhhuli za kibenki.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alisema, anayo furaha kubwa kuona benki hiyo yenye mtaji mkubwa inafunguliwa katika jiji la Dar es Salaam na hivyo itaongeza mitaji ya wawekezaji na wafanyabiashara wa kitanzania.
Alisema kuwa serikali ya Mkoa itaendelea kutoa ushirikiano unaotakiwa na taasisi hiyo kwa lengo la kufikia malengo yanayotarajiwa.“Mimi binafsi nimekwenda China ile dhana kuwa ni wajanja kibiashar ni dhana potofu cha msingi ni kuendelea kushirikiano katika sekta mbali mbali kwa manufaa ya nchi hizi ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa kujituma”, alisema
Katika kuimairisha ushirikiano na jamii ya wachina, Makonda alidokeza kuwa serikali ya mkoa wa Dar es Salaam itaandaa mkutano wa kubaini changamoto wanazokutana nao wafanyabiashara hao kwa nia ya kuzitatua.
Alisema kuwa nia na lengo la serikali ni kuona kuwa wafanyabiashara wa kigeni wanafanya biashara zao katika mazingira sawa na huru.
Balozi wa China nchini Tanzania Mhe.Wang Ke, (katikati), akiungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, (wapili kushoto), Mwenyekiti wa Banki mpya ya China Dasheng Bank Limited, Yu Jiaqin, (wapili kulia), Afisa mwandamizi kutoka Banki Kuu ya Tanzania, Sadaat Mussa (wakwanza kulia) na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka China, Zhujin Feng, baada ya kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Benki hiyo imeanza kutoa huduma leo Jumatatu Novemba 26, 2018 ikiwa na mtaji wa kuanzia wa dola za kimarekani milioni 40 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 92, Mwenyekiti wa benki hiyo amesema.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, akitoa hotuba yake.
Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke akitoa hotuba yake.
Mwenyekiti wa Banki mpya ya China Dasheng Bank Limited, Yu Jiaqin, akitoa hotuba yake.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka China, Zhujin Feng, akitoa hotuba yake.
Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa China Dasheng Banki Limited, Bi. Nunu Saghaf (watatu kushoto mstari wa mbele akiwa na wageni mbalimbali kwenye hafla hiyo ya uzinduzi.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi benki ya China Dasheng ,Limited Bw.Yu Jiaqin, (kulia), akibadilishana hati na Mkurugenzi Mtendaji wa Star Times Tanzania, Bw.Wang Xiaobo, wa ushirikiano baina ya benki na kampuni hiyo, wakati wa uzinduzi wa benki hiyo mpya jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wik.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda (kushoto), akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi China Dansheng Bank Limited, Bw. Yu Jianqin huku Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke, (wapili kushoto) na afisa mwandamizi kutoka Benbki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Saadat Musa wakishuhudia wakati wa uzinduzi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Wang Ke, (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, wakati wa uzinduzi wa benki mpya ya China Dasheng Bank Limited jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Benki hiyo inaanza kutoa huduma Jumatatu Novemba 26, 2018 ikiwa na mtaji wa kuanzia wa dola za kimarekani milioni 40 Sawa na shilingi za kitanzania bilioni 92, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya benki hiyo Bw. Yu Jiaqin amesema. Kulia ni afisa mwandamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Saadat Mussa.
Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Wang Ke, (watau kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda,(wapili kushoto), wakati wa uzinduzi wa benki mpya ya China Dasheng Bank Limited jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Benki hiyo inaanza kutoa huduma Jumatatu Novemba 26, 2018 ikiwa na mtaji wa kuanzia wa dola za kimarekani milioni 40 Sawa na shilingi za kitanzania bilioni 92, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya benki hiyo Bw. Yu Jiaqin (pichani wakwanza kulia) amesema. Wakwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa China hapa nchini, Bw.Zhujin Feng.
Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Wang Ke, (wapili kushoto), akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda,(wakwanza kushoto), wakati wa uzinduzi wa benki mpya ya China Dasheng Bank Limited jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Benki hiyo inaanza kutoa huduma Jumatatu Novemba 26, 2018 ikiwa na mtaji wa kuanzia wa dola za kimarekani milioni 40 Sawa na shilingi za kitanzania bilioni 92, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya benki hiyo Bw. Yu Jiaqin (pichani wapili kulia) amesema. Wakwanza kulia ni Afisa mwandamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Saadat Mussa.(PICHA/HABARI NA K-VIS MEDIA)
No comments:
Post a Comment