Saturday, November 10, 2018

CGP KASIKE ATEMBELEA MAGEREZA YA MGAGAO NA ISUPILO, LEO MKOANI IRINGA

Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati) akiangalia vitalu vya miche ya miti aina ya misindano(pines) alipowasili katika Gereza la Mgagao, Wilaya ya Kilolo leo Novemba 10, 2018. Kushoto kwake ni Mkuu wa Gereza hilo, ASP. Peter Sahani(kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Iringa, ACP. Hassard Mkwanda.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(wa kwanza kulia) akikagua moja ya shamba la miti aina ya misindano alipofanya ziara ya kikazi leo Novemba 10, 2018 katika Gereza la Mgagao, Wilayani Kilolo.
Askari wa Gereza Mgagao, Koplo Stephen akieleza changamoto mbalimbali za kiutendaji mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza alipotembelea gereza hilo leo Novemba 10, 2018.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akijibu hoja mbalimbali wakati akiongea na Maafisa na askari wa Gereza Mgagao alipotembelea gereza hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akikagua shamba la mifugo katika Gereza la Kilimo na Mifugo Isupilo, lililopo Wilayani Mfindi Mkoa wa Iringa.
Askari wa Gereza la Isupilo wakiimarisha ulinzi wakati Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiongea na Wafungwa na Mahabusu wa Gereza Isupilo(Picha na Jeshi la Magereza).

No comments: