Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa (kulia), akikabidhi hundi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka baada ya kununua hisa za benki hiyo muda mfupi baada ya DCB kuzindua zoezi la uuzaji wa hisa kwa mwaka 2018, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa.Uzinduzi huu unawalenga wanahisa waliopo, wawekezaji wapya na umma wa watanzania ikizingatiwa kuwa kwa mara ya mwisho DCB ilitoa fursa kama hiyo mwaka 2012.
UONGOZI wa Benki ya DCB umetangaza rasmi kuanzia Novemba 12 mwaka huu kuanza hisa zake kwa wanahisa wa sasa na umma wa Watanzania kwa ujumla na kwamba uuzaji wa hisa hizo umegawanyika kwenye awamu mbili.
Wakizungumza wakati wanatangaza uuzaji wa hisa hizo jijini Dar es Salaaam uongozi wa benki hiyo umesema hiyo ni fursa ya kipekee ambayo wanahisa na watanzania wote wanatakiwa kuichangamkia na kwamba hisa moja itauzwa kwa bei ya Sh.265 ambayo ni cheni ya bei iliyopo kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam(DSE).
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Biashara ya DCB Godfrey Ngalahwa amesema kuwa "Nachukua nafasi hii kuwataarifu kuwa uuzaji wa hisa za DCB unatarajia kuanza leo 12 Novemba 12, 2018. na kwamba Novemba 5, 2018, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) ilitoa idhini ya uuzaji wa hisa kwa wanahisa wa sasa na umma wa Watanzania kwa ujumla.
"Dhana kubwa ni kuwaruhusu wanahisa waliopo kununua hisa na kutoa nafasi kwa wawekezaji wengine kununua hisa zitakazobaki.
Uuzaji hisa za DCB umegawanywa katika awamu mbili, awamu ya kwanza itaanza leo hadi Desemba 3, 2018, ambapo hisa zitauzwa kwa wanahisa waliopo katika daftari la wanahisa. Aidha, kuanzia Desemba 4 hadi Desemba 18, 2018, hisa zote zitakazobaki zitauzwa kwa wanahisa waliopo na kwa wawekezaji wengine wasio wananhisa wa DCB. Kwa sasa, daftari limefungwa na mauzo ya hisa za DCB zilizopo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) yamesimamishwa kuanzia November 7 kupisha uuzaji wa hisa,"amesema.
Kuhusu utaratibu wa kushiriki kwa wanahisa Profesa amesema wanahisa watakaoshiriki ni wale walioorodheshwa katika Rejista ya Wanahisa baada ya kufungwa kwa jalada ili kupata idadi ya hisa stahili, Novemba 7 mwaka huu na kusisitiza mwanahisa ana haki ya kununua hisa moja kwa kila hisa mbili anazomiliki.
Aidha amesema wawekezaji wengine wanatakiwa kujaza fomu kuonesha idadi ya hisa watakazonunua na baada ya awamu ya pili kukamilika, watagawiwa kwa mujibu wa utaratibu utakaowekwa na uongozi wa benki na maelekezo ya waraka wa matarajio.
Hivyo basi, wanahisa waliopo na wawekezaji wapya, wote wanaruhusiwa, kwa mujibu wa taratibu, kununua hisa zitakazobaki baada ya awamu ya kwanza kukamilika. Amefafanua malipo ya kununua Hisa za Haki yatafanyika kupitia matawi yote ya Benki ya Biashara ya DCB na mawakala wa Soko la Hisa la Dar es Salaam.
Akizungumzia mpango mkakati wa biashara ameseama kuwa kwa njia ya mashauriano, mwishoni mwa mwaka 2017, Benki ilikaa na kufafanua mpango wake wa biashara wa miaka mitano ambao utatekelezwa kwa awamu tatu na kwamba mafanikio yaliyopatikana kati ya Januari na Juni mwaka 2018 yametokana na kuweka msisitizo kwenye mabadiliko ya kiutendaji na kuhakikisha benki inapata faida.
"Kazi hii imekamilishwa ipasavyo na matokeo yake hadi Septemba 2018 benki imefanikiwa kupata faida ya TZS 1.4 bilioni.
Mafanikio haya yametokana na kupungua kwa gharama za uendeshaji na kupunguza uwiano wa mapato na matumizi kutoka asilimia 104 mwaka 2017 hadi asilimia 81 mwaka 2018.Aidha, benki ilianzisha utaratibu wa kuboresha mtandao wa matawi na kutanua wigo wa bidhaa zilizopo na huduma kwa wateja ili kukuza mizania. Mikopo chechefu imedhibitiwa kwa kuanzisha mpango thabiti wa makusanyo ikiwa ni pamoja na kusuka upya idara ya mikopo,"amesema Ngalahwa.
Ameongeza benki hiyo inatarajia kufikia tarakimu moja ya mikopo chechefu mwishoni mwa mwaka 2019.Pia kuhakikisha benki inakuwa na wafanyakazi wenye maadili, utekelezaji wa programu ya mafunzo umefanyika na mchakato wa kuimarisha utamaduni wa utendaji unaendelea ambapo wafanyakazi wote wanahusika.Ameeleza mipango ya benki yao imekuwa kupata faida kabla ya kodi ya Sh.bilioni 1.8 ifikapo Desemba 2018.
Katika kipindi hiki, mtaji wa benki unasimamiwa kwa uangalifu na ufanisi, huku hatua madhubuti za kukusanya mkopo na ufuatiliaji zinaendelea ili kupunguza mikopo chechefu huku tukizidi kukuza biashara.
"Mpango wa biashara uliorekebishwa wa miaka mitano unathibitisha matarajio ya benki kukuza mali zake kutoka Sh.bilioni 154.88 hadi Sh.bilioni 363.20 na amana za wateja kutoka Sh.bilioni 119.20 hadi Sh.bilioni 304.83.
Kuhusu idadi ya wateja benki yetu imedhamiria kukuza mara mbili wateja wake mpaka 300,000 ifikapo mwaka 2022 huku ikiongeza masoko yake katika maeneo muhimu ya kimkakati,"amesema.
Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya DCB Profesa Lucian Msambichaka amesema anayo furaha kubwa kuzindua rasmi uuzaji wa hisa leo Novemba 12, 2018 na kusisitiza . Uzinduzi huo unawalenga wanahisa waliopo, wawekezaji wapya na umma wa Watanzania kwa ujumla na kwamba hiyo ni fursa hii ni adimu kwa kuwa haitokei mara kwa mara ikizingatiwa kuwa mara ya mwisho, Benki ya DCB ilitoa fursa kama hii mwaka 2012.
"Kuhakikisha wananchi wengi wanapata fursa ya kuwekeza katika benki yetu, hisa hizi zitauzwa kwa bei punguzo ya Sh.265 sawa na punguzo la asilimia 22 ikilinganishwa na bei yake halisi iliyopo katika soko la hisa la Dar es Salaam ambayo ni TZS 340 kama ilivyonukuliwa tarehe 9th Novemba, 2018. Kila mwanahisa atapewa stahiki ya kununua hisa moja kwa kila hisa mbili alizonazo na mwekezaji mpya atatakiwa kuomba kununua hisa zitakazobaki.
Uuzaji hisa za DCB umegawanywa katika awamu mbili, awamu ya kwanza itaanza leo hadi Desemba 3, 2018, ambapo hisa zitauzwa kwa wanahisa waliopo katika daftari la wanahisa.
Uuzaji hisa za DCB umegawanywa katika awamu mbili, awamu ya kwanza itaanza leo hadi Desemba 3, 2018, ambapo hisa zitauzwa kwa wanahisa waliopo katika daftari la wanahisa.
Aidha, kuanzia Desemba 4 hadi Desemba 18, 2018, hisa zote zitakazobaki zitauzwa kwa wawekezaji wengine wasio wanahisa wa DCB,"amesema.
Pia Profesa Msambichaka amesema Benki ya DCB inatarajia kuuza jumla ya hisa 33,913,948 ili kuongeza mtaji wa Sh. bilioni 8.9, mtaji huo utasaidia kuongeza uwezo wa benki sambamba na kuchochea ukuaji na mageuzi ya kibenki yatakayoifanya ijiendeshe kibiashara kikamilifu.
Amesema benki ya DCB mpaka sasa ina jumla ya hisa 67,827,897 ambazo tayari zimeishanunuliwa na kulipiwa kikamilifu na kiasi cha mtaji uliolipiwa kuhusiana na hisa hizo ni Sh.bilioni 16.96. Utoaji huo wa hisa mpya utafikisha idadi ya hisa kwa ujumla kuwa 101,741,845.Bodi ya wakurugenzi itapitia kwanza maombi ya wanahisa waliopo kabla ya kugawa hisa kwa wengine walioomba kwa mujibu wa sheria na utaratibu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).
Amesema benki ya DCB mpaka sasa ina jumla ya hisa 67,827,897 ambazo tayari zimeishanunuliwa na kulipiwa kikamilifu na kiasi cha mtaji uliolipiwa kuhusiana na hisa hizo ni Sh.bilioni 16.96. Utoaji huo wa hisa mpya utafikisha idadi ya hisa kwa ujumla kuwa 101,741,845.Bodi ya wakurugenzi itapitia kwanza maombi ya wanahisa waliopo kabla ya kugawa hisa kwa wengine walioomba kwa mujibu wa sheria na utaratibu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).
Amesema wanahisa wa sasa na watarajiwa watafaidika na uwekezaji huu kutokana uuzaji wa hisa kwa bei pungufu ukilinganisha na bei ya soko huku wakiwa na kumbukumbu kuwa ni miongoni mwa fursa adimu zinazoweza kuwaongezea umiliki katika benki kwa kununua hisa mpya. Aidha, thamani ya kila mwanahisa inaweza kuongezeka kutokana na ukuaji wa bei ya hisa unaosukumwa zaidi na ukuaji wa biashara na nguvu ya hisa za benki katika soko la hisa. Vilevile mwanahisa atapata gawio kila mwaka kulingana na mwenendo wa kibiashara wa benki.
No comments:
Post a Comment