Thursday, November 15, 2018
BARAZA LA MADIWANI JIJINI TANGA LAAMUA SEHEMU ITAKAPOJENGWA HOSPITALI YA WILAYA.
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapha Selebosi akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akipitia taarifa kwenye kikao hicho
MKURUGENZI wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza katika kikao hicho
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga akisikiliza kwa umakmini hoja mbalimbali kwenye kikao hicho
NAIBU Meya wa Jiji la Tanga Mohamed Haniu akipitia kabrasha wakati wa kikao hicho kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji hilo Alhaj Mustapa Selebosi
Diwani wa Kata ya Mnyanjani (CUF) Thobias haule akiuliza swali kwenye kikao hicho
Diwani wa Kata ya Kirare
Baadhi ya madiwani wakiwa kwenye kikao hicho
Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO) Dkt Jery Khanga akifuatilia hoja mbalimbali kwenye kikao hicho akiwa na wataalamu wengine wa Halmashauri hiyo
BAADA ya mjadala wa muda mrefu hatimaye Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Tanga limeamua rasmi eneo la Mwakidila lililopo Kata ya Tangasisi kuwa sehemu sahihi ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya Tanga ambao utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.5
Awali hospitali hiyo ilitarajiwa kujengwa katika kata ya Masiwani ambapo tayari jengo la utawala la ghorofa moja lilikwisha jengwa ambalo linadaiwa kugharamia kiasi cha shilingi Milioni 700.
Mjadala uliibuka ndani ya kikao hicho cha baraza hilo ambapo madiwani walipingana eneo gani linaweza kuwa sahihi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo ambayo mchakato wake unadaiwa kuanza tangu mwaka 2005.
Akizungumza Mwenyekiti wa baraza hilo Mstahiki Meya Mustafa Seleboss alisema kweli yapo maeneo matatu yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ambayo kila eneo linachangamoto zake huku akibainisha umuhimu wa hospitali hiyo kujengwa katika eneo hilo la Mwakidila.
Aidha alisema Halmashauri imekwisha pokea kiasi cha shilingi Milioni 500 kati bilini 1.5 toka Serikali kuu kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa hospitali hiyo ambayo itaondoa sitofahamu ya kutokuwepo kwa Hospitali hiyo ndani ya Wilaya.
Seleboss alisema hakuna haja ya kuendeleza malumbano juu ya wapi Hospitali hiyo itajengwa huku fedha hizo zikiwa zimetolewa na Serikali kwa mashari ya utekelezaji wa haraka wa ujenzi wa hospitali hiyo ambayo itapunguza msongamano katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo.
“labda niwaeleze ukweli ndugu zangu madiwani plani ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya eneo la masiwani lipo palepale ila kutokana na mgogoro uliopo wa ardhi tunalazimika fedha hizo kuanza kujenga Mwakidila badala ya masiwani”Alisema Seleboss.
Hata hivyo aliwanasihi madiwani na wananchi wa kata ya masiwani ambao walitarajia kupata hospitali hiyo ya Wilaya kuwa ndoto hiyo haijafutika na itajemgwa Hospitali nyingine kwa kupitia fedha toka vyanzo vya ndani vya Halmashauri.
“Tulikuwa na maeneo matatu ya mwakidila,masiwani na kihongwe lakini kutokana na changamoto ya maeneo hayo mawili ya kihongwe na masiwani tumeona ni bora mradi huu tuuelekeze mwakidila eneo lililopo karibu na barabara kuu ya Tanga-Pangani”Alisema.
Awali akizungumzia mkanganyiko huo Diwani wa kata ya Duga Khalid Rashid(CUF) alisema hapingani na maamuzi ya baraza lakini jambo la msingi ni kuangalia gharama zilizotumiaka eneo la masiwani za ujenzi wa jengo la ghorofa moja la utawala kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya.
Alisema ipo haja kwa Halmashauri kuwa makini juu ya taarifa za wataalamu ambao awali waliishauri Halmashauri kujenga Hospitali hiyo eneo la masiwani ambapo zaidi ya shilingi milioni 700 zimetumika katika ujenzi wa jingo la utawala.
“Mstahiki Meya sipingi na wala sikatai hospitali hiyo kujengwa mwakidila lakini tuwe makini na wataalamu wetu tumewekeza fedha nyingi kwa nini hizi bilioni 1.5 zisiendeleze pale masiwani? lakini ni maamuzi ya baraza wacha tuyaheshimu”Alisema Rashidi.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapa alisema kumekuwepo na maneno ya fitina juu ya mradi huo wa Hospitali lakini jambo muhimu muafaka umefikiwa wa wapi itajengwa hilo ndio jambo la msingi.
Alisema hakuna haja ya kulumbana hasa katika maswala ya msingi na maendeleo ya wanachi makubaliano ndio jambo muhimu ili pande zote mkubaliane kwa pamoja wapi hospitali hiyo itajengwa na lengo ni kumsaidia mwananchi katika swala la afya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment