Kamati ya kusimamia ofisi ya viongozi wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa maendeleo ya jamii Ladislaus Mwamanga (mwenye suti ya rangi ya ugolo) na baadhi ya viongozi mkoani Pwani na halmashauri ya Kibaha Vijijini, wakipatiwa maelezo wakati walipotembelea kilimo cha bustani huko Disunyara Kibaha Vijijini. (picha na Mwamvua Mwinyi)
Naibu waziri ,ofisi ya makamu wa pili Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mihayo N’hunga akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya kusimamia ofisi ya viongozi wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyofanyika Kibaha Vijijini Mkoani Pwani. (picha na Mwamvua Mwinyi)
…………………………………………….
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
MKURUGENZI wa mfuko wa maendeleo ya jamii -TASAF, Ladislaus Mwamanga amesema, bado zipo kaya maskini 6,048 sawa na asilimia 30 Tanzania Bara na Visiwani, ambazo hazijafikiwa katika utekelezaji wa mpango kunusuru kaya maskini .
MKURUGENZI wa mfuko wa maendeleo ya jamii -TASAF, Ladislaus Mwamanga amesema, bado zipo kaya maskini 6,048 sawa na asilimia 30 Tanzania Bara na Visiwani, ambazo hazijafikiwa katika utekelezaji wa mpango kunusuru kaya maskini .
Aidha , wale ambao wameshanufaika awamu ya kwanza ya mpango huo watafanyiwa tathmini, na wameandaa mkakati wa kuwapima kwa vigezo vya kuwa na hali nafuu kwa utaratibu ili watoke na wapishe wengine.
Akiweka bayana juu ya masuala hayo, wakati wa ziara ya kamati ya kusimamia ofisi ya viongozi wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyofanyika Kibaha Vijijini Mkoani Pwani, alisema maeneo ambayo hayakufikiwa ,utekelezaji utaanza mwezi april 2019 ,ili kukamilisha maeneo yote nchi nzima 16,048.#
Mwamanga alisema vijiji,sheia na mitaa 10,000 wameshavifikia hadi sasa .
Alifafanua, kuna kaya maskini ziliachwa kwenye mpango kwa sababu mbalimbali nao wataingizwa kwenye mfumo thabiti ili kuwa na rekodi sahihi kwa nchi nzima.
Hata hivyo ,alisema kaya ambazo zina wazee na wenye ulemavu wataendelea kuwasaidia ili kukidhi mahitaji yao ya msingi.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Naibu waziri ,ofisi ya makamu wa pili Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mihayo N’hunga alisema, serikali ipo katika hatua za mwisho za kisera kutatua changamoto ya muda mrefu kwa kaya ambazo hazikujumuishwa katika mpango .
Alifafanua ,kaya hizo hazikuweza kujumuishwa kutokana na kutofanyiwa dodoso na baadhi ya walio fanyiwa dodoso kukataa mpango kwa madai kwamba hauna manufaa kwao.
N’hunga alisema, kupitia madodoso hayo ,serikali ikajumuisha watu hao kwenye mpango kupitia changamoto hizo ,kuboresha sera na utaratibu uliopo ili kupunguza changamoto hiyo Bara na Visiwani kwa lengo la kuwafikia watanzania maskini katika ngazi ya sheia,kata, mitaa na vitongoji .
Hata hivyo alieleza dhamira ya serikali zote mbili kufikia april 2019 kaya zilizopo kwenye vijiji,sheia na kata ambazo hazijafikiwa waweze kufikiwa .
Katibu tawala msaidizi mkoani Pwani ,Abdulrahman Mdimu alisema, wanakabiliwa na changamoto ya baadhi ya kaya maskini katika vijiji 86 ,mitaa 33 kutofikiwa kutokana na upungufu wa raslimali fedha .
Alitaja changamoto nyingine ni baadhi ya walengwa kukataa kuingizwa kwenye mpango kwa madai serikali haiwezi ikatoa fedha bure ,mitazamo hasi wakidhani kuwa kaya ikitambuliwa ni maskini ni kufedheheka.
Kamati hiyo ilitembelea pia ,mradi wa kutoa ajira ya muda -uvunaji wa maji ya mvua katika zahanati ya Disunyara kata ya Kilangalanga na kilimo cha bustani ,ambapo kaimu mratibu TASAF halmashauri ya Kibaha Vijijini Halima Bira, alisema mpango huo umekuwa mkombozi katika jamii .
Halima alisema ,mpango huo ulianza kutekelezwa 2012 na jumla ya kaya 7,250 zilitambuliwa na kati ya hizo kaya 5,600 kutoka vijiji 45 ziliandikishwa kwenye mpango.
Shuhuda wa utekelezaji wa mpango wa TASAF ,huko Disunyara Athumani Shabani alisema,ameweza kusomesha watoto ,wameibua miradi na wazee wananufaika kupitia mradi huo
No comments:
Post a Comment