Sunday, October 7, 2018

TCCIA YAJIVUNIA UWEPO WAKE NA MCHANGO WALIOUTOA KWA MIAKA 30 KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI KWA KUSAIDIANA NA SERIKALINa Said Mwishehe,Globu ya jamii

CHAMA cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo kinajiandaa kusheherekea miaka 30 tangu kuanzishwa kwake huku kikijivunia mafanikio ambayo yamepatikana katika sekta ya kilimo,biashara na viwanda kutokana na uwepo wao nchini.

Kimeeleza namna ambavyo kimeshiriki kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini n katika kipindi hiki cha kusheherekea miaka 30 ya uwepo wao kabla ya kufikia siku ya kilele Novemba mwaka huu watafanya shughuli mbalimbali katika wilaya na mikoa yote nchini.

Akizungumza Dar es Salaam Kaimu Rais wa TCCIA Octavian Mshiu amesema uwepo wao na mchango wake kwa Taifa mbali na kuwaunganisha vyombo mbalimbali vinavyojihusisha na kilimo,viwanda na biashara wamefanikisha uwepo wa mazingira mazuri ya uwekezaji.

Amesema kimsingi huko nyuma watanzania walikuwa hawashiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi lakini kupitia TCCIA watanzania wameweza kushiriki kwa kuanzisha viwanda na kampuni na hivyo kuwa sehemu ya wawekezaji nchini."Kuna mengi ya kujivunia kama TCCIA ,kadri muda unavyokwenda kuelekea kwenye sherehe ya kutimiza miaka 30 tangua kuanzishwa kw TCCIA mengi tutazungumza kupitia viongozi mbalimbali.

" Baadhi ya viongozi hao wameshastaafu baada ya kuitumikia TCCIA na kutoa mchango wao mkubwa nao watapata nafasi ya kuzungumza na kutoa maoni yao,tulikotoka,tulipo na tunakokwenda,"amesema Mshiu.Kuhusu TCCIA na mchango wake kwa jamii anasema watanzania wengi wanamiliki viwanda ndani na nje ya nje ya nchi na TCCIA imetoa mchango mkubwa nchini Tanzania.

Pia ameahidi TCCIA itaendelea kuunga mkono Serikali katika kusaidia kuboresha sekta ya biashara na Novemba mwaka huu ndio wanatarajia kusheherekea miaka 30 ya TCCIA ambayo ilianza mwaka 1988.Wakati huo huo Kaimu Rais wa TTCIA amesema pamoja na maandalizi ya sherehe hizo,pia wapo katika mchakato wa kuanzisha TCCIA China Diaspora .

Amesema lengo ni kuwasaidia Watanzania wanaofanya biashara China kuwa na mazingira mazuri ya kibiashara na Wachina nao kufanyabiashara na shughuli nyingine za kiuchumi bila usumbufu.Mmoja wa wanachama wa TCCIA amabaye aliyekuwa Mkuu wa msafara wa wafanyabiashara wa Tanzania walioambatana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Alli Iddi, Nelson Ngowi ameeleza namna ambavyo alikutana na wafanyabiashara wa Kitanzania wanaoishi China na namna walivyo na shauku ya kuanzisha TCCIA huko China.

" Pamoja na kushiriki maonyesho ujumbe wetu ulipata heshima ya kukaribishwa na Balozi wa Tanzania nchini china Balozi Mbelwa Kairuki na kubadilishana naye mawazo,”amesema.Kwa upande wake aliyekuwa Rais Mstaafu wa TCCIA David Mwaibula ambaye alikuwa Rais wa pili wa chama hicho amesema kuna mambo mengi ambayo yamefanyika kwa nyakati tofauti na kufafanu huko nyuma hakukuna Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)lakini walishiriki kuhakikisha chombo hocho cha kukusanya kodi kinaa zishwa na kuwa na mazingira rafiki ya ulipaji kodi.

Pia amesema pamoja na mambo mengine TCCIA wamefanikiwa kuunganisha vyombo mbalimbali na kwamba katika kushughulika na utatuzi wa changamoto au kujadili mambo kadha kazi ya chombo hicho ni kushughulika na taasisi husika na si mtu mmoja mmoja.

Amezungumzia namna ambavyo TCCIA ilivyoshiriki katika kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri ya ulipaji kodi na pale ambapo haki inawezekana kutotendeka kuna vyombo vyenye mamlaka ya kusikiliza na kutoa uamuzi na hivyo hakuna sababu ya kutoa rushwa ili kupata haki.

"TCCIA tumekuwa tukikaa pamoja na Serikali kujadili mazingira ya uwekezaji .Kwa kweli kuna mambo mengi tunafanya kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji.

"Pia TCCIA imekuwa na jukumu la kutafuta masoko kwa ajili ya mazao ya wakulima.Nakumbuka huko nyuma tumewahi kufanya tafiti kwa kuwashirikisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na lengo ni kutafiti shughuli za kiuchumi," amesema.
 Kaimu Rais wa TCCIA Octavian Mshiu(kushoto) akiwa na aliyewahi kuwa Rais wa TCCIA David Mwaibula wakiwa wameshika cheti
Rais mstaafu wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini(TCCIA)David Mwaibula akifafanua jambo kuhusu Chama hicho ambacho kinatarajia kusheherekea kutimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1988

No comments: