Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga
Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia akielezea mipango ya mamlaka hiyo
wakati wa ziara ya ugeni kutoka KFW ya nchini Ujerumani kutembelea mradi
wa maboresho ya huduma ya maji safi Jijini Tanga
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga
Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly katikati akionyesha kitu ugeni kutoka KFW
ya nchini Ujerumani wakati wa ziara yao ya kutembelea mradi wa maboresho
ya huduma ya maji safi Jijini Tanga.kulia ni Katibu Tawala wa mkoa wa
Tanga Mhandisi Zena Saidi
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa ziara
hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia akifirahia jambo na
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maji Mijini kutoka Wizara ya Maji
-Dodoma Mhandisi Lydia Joseph kushoto wakati wa ziara hiyo
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akilakiwa na watumishi wa mamlaka hiyo mara baada ya kuwasili eneo la Mowe
Wageni hao wakishuka kwenye eneo la kusafishia maji Mowe Jijini Tanga wakati wa ziara hiyo
Wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ziara hiyo
MAMLAKA
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)
imenufaika na ruzuku ya zaidi ya Shilingi bilioni 1.2 baada ya kutimiza
masharti ya mkopo wa zaidi ya shilingi Bilioni 3 toka katika benki ya
CRDB ya utekelezaji wa huduma ya Maji safi Jijini Tanga.
Ruzuku
hiyo hutolewa na Benki ya watu wa Ujerumani (KFW) kutokana na Mamlaka
husika kutimiza vema masharti ya mkopo huo ikiwa pamoja na zoezi zima la
marejesho huku likizingatiwa suala la utekelzaji wa mradi uliopewa
fedha hizo.
Hayo
yalibainishwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa
ziara ya ugeni kutoka KFW ya nchini Ujerumani kutembelea mradi wa
maboresho ya huduma ya maji safi Jijini Tanga.
Alisema
mkopo huo umewasaidia kuongeza uwezo wa usambazaji wa maji hasa katika
maeneo yaliyokuwa na mgawo wa maji bila sababu yaliyochangiwa na udogo
wa vipenyo vya mabomba yaliyokuwa yanapeleka maji kwenye maeneo hayo.“Kama
nilivyoonyesha kwamba tumeongeza bomba kubwa la nchi 8 kwa ajili ya
kuongeza mgawanyo wa maji kwenye eneo la Neema na kwengineko na kuwepo
kwa usambazaji mkubwa kwenye maeneo hayo lakini pia tumejenga mtandao wa
km 60 kwa kutumia mkopo huo na ruzuku tuliyopewa”Alisema
Aidha
alisema hivi sasa wamejipanga kuendelea kudumisha ubora wa huduma zao
ili kuhakikisha wananchi wanaowahudumia wanaendelea kupata huduma bora
ya maji katika maeneo yao.Alisema
mbali ya ubora wa huduma hizo za maji lengo kuu ni kuhakikisha
wanapokuwa wageni wahisani waweza kupata mrejesho na taswira nzuri kwa
mamlaka ili waendelee kupata moyo wa kuwasaidia.
Awali
akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maji
Mijini kutoka Wizara ya Maji -Dodoma Mhandisi Lydia Joseph alisema fedha
hizo zinalenga katika miradi inayojenga inalengo la kutoa uzoefu kwa
mamlaka za maji zinazoingizwa kwenye mfumo huo iliziweze kupata uzoefu wa kuwekeza badala ya kuishia kutoa huduma pekee.
Alisema
mamlaka nyingi zimekuwa na lengo la kutoa huduma ya maji kwa wananchi
kwa miundombinu iliyojengwa na serikali tangu zamani hivyo kutokana na
ongezeko la watu na mahitaji yao Mamlaka zinatakiwa kupanua huduma zao.
Mhandisi
Lydia alisema mbali na huduma pia mamlaka hizo za maji zinatakiwa
kuboresha miundombinu ambayo inahitaji uwezeshwaji kutokana na serikali
kuwa na mambo mengi ya kufanya hivyo wakati mwengine huelemewa na
uwekezaji jambo ambalo limepelekea kushindwa kuendana nakasi ongezeko la watu.
“Kwa
maana hiyo Mamlaka zetu kama zitapata mikopo na zikijenga uaminifu
zinaweza kupata miradi kama hiyo na zaidi ya hiyo huku zikijijengea
morali kwa mamlaka zenyewe hasa kwenye uwekezaji na Serikali ikatoa
sapoti ”Alisema Mhandisi Joseph.
No comments:
Post a Comment