Friday, October 19, 2018

SERIKALI YAOMBWA KUCHUKUA HATUA KALI WAZAZI NA WALEZI WATAKAOKEKETA MTOTO WA KIKE.

Na Frankius Cleophace Tarime.

Serikali imeombwa kuchukua hatua kali kwa wazazi na walezi Wilayani Tarime Mkoani Mara ambao wanakubali kukeketa watoto wa kike ambao ukimbia ukeketaji kipindi hicho na baada ya zoezi kumalizika mabinti hao waliokimbia ukamatwa na kukeketwa hivyo wameiomba serikali kuendelea kusimamia vikali sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 ili kutokomeza suala la ukeketaji kwa mtoto wa kike huku baadhi yao wakikeketwa usiku.

Hayo yamebainisha na baadhi ya wazazi katika kata ya Pemba kipindi wakipatiwa elimu ya kupinga Ukeketaji kupitia Shirika la Tanzania Mindset Network chini ya Ufadhili wa TGNP Mtandao kupitia Shirika la Idadi ya Watu Ulimwenguni UNFPA.

Wazazi hao wamedai kuwa kipindi cha ukeketaji watoto wamekuwakikimbia ili wasikeketwa mpaka msimu wa ukeketaji unamalizika lakini pale wanarudi kijijijini ukamatwa na jamii na kukeketwa kwa Nguvu hivyo wameomba serikali kuwachukulia hatua kali wazazi na walezi watakaoshiriki katika kitendo hicho.

“Pia wazazi hao wamesema kuwa kuna tetesi za watoto wa kike kukeketwa nyakati za usiku baada ya serikali kwa kushirikiana na mashiriki kupinga vikali ukeketaji.Kuna Ngariba tunamfaamu yuko maeneo ya mbali ameibuka hivi karibuni tunajua atakeketa watoto wetu usiku hivyo sasa serikali itambue suala hilo” alisema Mmoja wa wazazi katika kijiji cha Nyabisaga kata ya Pemba.

Thomas Muruga ni Mratibu wa Shirila la Tanzania Mindset Network amesema kuwa kwa sasa wameamua kutoa elimu ya kupinga Ukeketaji kwa kutembelea Nyumbakwa Nyumba huku wakifanya Mikutano ya hadhara katika kata 13 Wilayani Tarime ili kuweza kutoa elimu hiyo kwa lengo la kunusuru mtoto wa kike ili hasikeketwe.

“Kabla ya kufanya Mikutano ya hadhara na kuongea na viongozi wa serikali ngazi za vijiji tunapita baadhi ya Nyumba na kutoa elimu huku tukibaini changamoto na nini cha kufanya lengo ni kunusuru mtoto wa kike mwaka huu hasiweze kukeketwa” alisema Muruga.

Pia Muruga amesema nia ya Shirika hilo ni kuwafikia wazazi, walezi, Watoto wa kike, Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji ili kutoa elimu hiyo nao waweze kuwa mabalozi kwa lengo la kupinga Ukeketaji

Mwita Chacha ni Mwenyekiti wa kijiji cha Nyabisaga anazungumzia suala la Watoto wa kike kukeketwa Nyakati za usiku amesema kuwa bado taarifa hizo kama viongozi hawajapelekewa lakini tayari wamepiga marufuku suala la Ukeketaji na kuhaidi kuchukua hatua kali kwa mzazi au mlezi atakayeshiriki kwa aina yeyote kukeketa Mtoto wa kike.

Naye Rhobi Kemahi ambaye ni Mwenyekiti wa kitongozji cha Nyaibara akishauri elimu kuendelea kutolewa kuanzia kwa viongozi wa vitongoji, vijiji na kata ili kusimamia vikali suala hilo pamoja na kufikisha elilimu hiyo maeneo ya pembezoni na siyo Mjini tu.

Aidha Eliafile Ndossi ambaye ni Mwezeshaji kutoka shirika la Tanzania Mindset Network amesema wazazi na walezi wakipata elimu hiyo itasaidia snaa kwani wao ndo wanaishi na watoto hivyo amewaomba wazazi hao kuacha kupeleka watoto wao ili kukeketwa.

Sasa mnasema wazee wa mila wanawalazimisha kukeketa watoto nyie kama wazazi hebu weka msimamo msipeleke watoto kwa Ngariba kukeketa msipeleke hizo fedha wazee na Ngariba wakose watoto wa kukeketa tuone watafanya kazi gani licha ya kukeketa alisema Ndossi.

huku washiriki wa Mafunzo hayo wakiweno Wenyeviti wa Vitongiji, Vijiji na Wazazi wakieleza nini kifanyike ili kutomeza suala la Ukeketaji.


Eliafile Ndossi ambaye ni mwezeshaji kutoka Shirika la Tanzania Mindset Network akitoa elimu juu ya madhara ya kupinga Ukeketaji kwa viongozi wa Vitongoji, Vijiji pamoja na wazazi na walezi katika kijiji Cha Pemba na Kyoruba.


Christina Edward mkazi wa kijiji cha Nyabisaga kata ya Pemba akibainisha changamoto wanazokumbana nazo kama wazazi katika suala zima la kupinga Ukeketaji baada ya kutembelewa Nyumbani kwake na watoa elimu ya kupinga Ukeketaji kupitia Shirika la Tanzania Mindset Network.
Ghati Samweli ambaye ni mwezeshaji kutoka Shirikala Tanzania Mindset Network akitoa elimu ya kupinga Ukeketaji baada ya kutembelea moja ya familia katika kijiji cha Nyabisaga Wilayani Tarime Mkoani Mara ambapo watoa elimu hiyo wameamua kufika Nyumba kwa Nyumba lego ni kunusuru mtoto wa kike hasiweze kukeketwa.
Picha ya Pamoja baada ya kutolewa kwa elimu ya kupinga Ukekeytaji katika kijiji cha Nyabisaga.
Eliafile Ndossi ambaye ni mwezeshaji kutoka Shirika la Tanzania Mindset Network akitoa elimu juu ya madhara ya kupinga Ukeketaji kwa viongozi wa Vitongoji, Vijiji pamoja na wazazi na walezi katika kijiji Cha Pemba na Kyoruba.
Rouben Makuri mwenyekiti wa kijiji cha Kyoruba akichangia hoja juu ya kupinga ukeketaji kwa mtoto wa kike ambapo amewasihi wazazi na walezi kuondokana na sula la kupeleka watoto ili kukeketwa.

No comments: