Sunday, October 7, 2018

RUDI TTCL KUMENOGA-MWANRI


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri( wa pili kutoka kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania Waziri Kindamba (kushoto) na viongozi wengine wa Shirika hilo wakiwa na bango lenye maneno ya lugha ya Kinyamwezi yenye maana RUDI NYUMBANI KUMENOGA wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo jana mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania Waziri Kindamba( wa pili kutoka kushoto) wakionyesha umahiri wa kuzirudi ngoma jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA mkoani humo.
1
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(katikati) akipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania juu ya huduma mbalimbali zinatolewa na Shirika hilo jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA mkoani humo.
2
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwapungia mkono wakazi wa Manispaa ya Tabora wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ilifanyika mkoani humo jana .
3
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kulia walikaa) akiwa na wakazi wa Manisapaa ya Tabora wakisikiza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania Waziri Kindamba( hayupo katika picha) juu ya huduma mbalimbali zinatolewa na Shirika hilo jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA mkoani humo.
4A
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania Waziri Kindamba akitoa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinatolewa na Shirika hilo jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA mkoani humo.
5A
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akipata maelezo  wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA mkoani humo jana.picha na Tiganya Vincent
RS TABORA



NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

WAKAZI wa Mkoa wa Tabora wametakiwa kuliunga mkono Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kujiunga na huduma mbalimbali wanazotoa ili liweze kuendelea kutoa gawio kubwa kwa Serikali kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi wote hapa nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya rudi nyumbani kumenoga mkoani humo.

Alisema kuwa kupitia gawio ambalo Shirika hilo linatoa kwa Serikali kati ya fedha hizo zinakuja Mkoani humo kwa ajili ya kuimarisha miundo mbinu ya barabara, huduma za maji, shule , ununuzi wa dawa, ulipaji wa mishahara ya watumishi na shughuli mbalimbali za maendeleo.

“Ndugu zangu TTCL kumenoga turudi…ukiongeza salio kwenye simu yako hata usipotumia mwezi salio lako liko salama…hivi sasa huduma zao hazihitaji kupanda kwenye mti ndio ufanye mawasiliano, bali popote unawasiliana…hakuna kusema sogea pembeni sikusikii ndio upige simu…hivi sasa hata ukiwa hata porini TTCL inapatikana” alisema.

Mwanri alisema kwa kuunga mkono huduma za TTCL watakuwa nao wajiwekea akiba ya kurudishiwa sehemu ya huduma walizochangia kwa njia ya Serikali kupata gawio na hatimaye kurejesha sehemu ya fedha hizo katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwa kuwa huduma zake zinapatikana katika maeneo mengi hapa nchini ni muhimu kwa wakulima na wafanyabiashara kulitumia kwa kutafuta masoko ya mazao.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Waziri Kindamba alisema Shirika hilo hivi sasa limeanza kutoa gawio kwa Serikali ambapo mwezi Juni mwaka huu lilitoa bilioni 1.5 , jambo ambalo lilishindikana kwa kipindi takribani maika 17.

Alisema juhudi za Shirika hilo linalenga kuhakikisha huduma zake zinapatikana nchini kote na kuwafikia wananchi popote walipo kwa asilimia 100 katika muda mfupi ujao.

Kindamba alisema lengo ni kusaidia katika kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa viwanda , huduma za jamii na maendeleo ya Sekta nyingine kwa kutumia huduma za Shirika hilo.

Alisema mwelekeo wa Shirika pia ni kusaidia juhudi za Serikali katika kukusanya mapato kupitia malipo yanayofanyika kwa njia ya Mtandao.

No comments: