MENEJA
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu
akizungumza wakati wa mahafali ya 8 ya Darasa la Saba katika Shule ya
Kana Eglish Medium Central School ya Jijini Tanga ambapo alitumia
nafasi hiyo kuhamasisha mpango wa Toto Afya Kadi kwa watoto na wazazi.
Afisa
Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Nico
Kasebwa kushoto akisisitiza jambo kwa mmoja wa wananchi wa Jiji la Tanga
aliyefika kwenye banda lao kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko huo uli
kuweza kunufaika na huduma za matibabu wakati wanapougua kushoto ni
Afisa Uanachama NHIF Jesca Nyau
Afisa
Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Nico
Kasebwa akimuonyesha kitu kwenye kipeperushi chenye maelezo ya Mpango wa
Toto Afya Kadi mkazi wa Jiji la Tanga Daudi Mbisco mara baada ya
kutembelea banda lao
MFUKO
wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) umewapa mbinu bora za wazazi na
walezi kuwapa zawadi muhimu watoto wao katika maisha yao ni kuwaingiza
kwenye mpango wa Toto Afya kadi ili waweze kunufaika na huduma za
matibabu.
Hayo
yalisemwa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga Ally
Mwakababu wakati akizungumza na wanafunzi na walezi kwenye mahafali ya
nane ya darasa la Saba katika shule ya Kana Central English Medium
Primary School.
Alisema
wakati wa ukuaji wa watoto wamekuwa wakikumbana na magonjwa mbalimbali
ambayo yanaweza kupelekea kukwamisha ndoto zao lakini wanapokuwa
wameandikishwa kwenye mpango wa Toto Afya Kadi wanaweza kupata matibabu
kwenye vituo mbalimbali vya Afya.
“Nimekuja
hapa kwa lengo kuu moja kuhamaisha umuhimu wa wazazi na walezi kuwapa
zawadi ya Bima watoto wao kupitia mpango wa Toto Afya Kadi kwani hakuna
anayweza kuelezea gharama za matibabu wakati mtoto wake anayweza
kuungua”Alisema.
Hata
hivyo alisema kwamba wazazi wanapowaingiza watoto wao kwenye mpango huo
unawapa uhakika wa matibabu na wanaweza kuwa na kumbukumbu nzuri ya
maisha yao .
No comments:
Post a Comment