Monday, October 22, 2018

NAIBU WAZIRI WA MADINI DOTTO BITEKO AFANYA ZIARA MIGODI YA KISARAWE

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko ametembelea Migodi ya Kaolin ya Wilaya Kisarawe Mkoani na kujionea uzalishaji na kukagua migodi ambayo imefungiwa kwa muda na kutoa maelekezo hili waweze kufunguliwa kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara hiyo Naibu Waziri Biteko amesema lengo la ziara hiyo ni kuhimiza ulipaji wa kodi katika sekta ya madini, kwani kulikuwa na changamoto nyingi katika sekta hiyo hasa ulipaji wa mrabaha.

"tunalipa kodi ya madini haya kulingana na unapouzia sio kulipa mrabaha kwa eneo unalochimbia hivyo tumewaeleza wale wote ambao watakwenda kinyume nataratibu hizo atakuwa amekwepa kodi kwa makusudi kwa tayari wameshapewa taharifa hivyo kwa sehemu kubwa ya wachimbaji niliyowatembelea wamefuata sheria na kanuni tulizowaelekeza "amesema Naibu Waziri Biteko.

Naibu Waziri Biteko ametoa wito kwa wachimbaji wote waendelee kushirikiana na ofisi za madini kwani serikali ipo kwa ajili ya kuwalea wachimbaji wadogo hili waweze kufikia maelengo.amessisitiza kuwa sheria ya Madini ya mwaka 2018 inamtaka kila mwenye leseni ya madini kutunza kila nyaraka ya uchimbaji na mauzo hivyo inamtaka kutoa nyaraka hizo kwa afisa yoyote atakayefika katika eneo hilo na yoyote atakeyshindwa kufanya hivyo atatozwa faini ya Milioni 50 hadi 150 

kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe Mtera Mwampamba amemshukuru Naibu Waziri kwa Maelekezo yake na ofisi ya Mkuu wa Wilaya inaendelea kushughulikia changamoto mbalimbali za sekta ya Madini hili waweze kuwa na uzalishaji mzuri wenye tija kwa wawekezaji na Serikali.
Naibu Waziri wa Madini , Dotto Biteko akimsikiliza Fundi Umeme wa Magari wa kampuni ya Madini ya Caolin, Asinine Ahmed akiteta jambo na Waziri mara baada ya kutembelea mgodi huo kujionea uchimbaji wa madini ya Kaolin yanayotumika kujtengenezea Vigae na Gypsum.
Naibu Waziri wa Madini , Dotto Biteko akimsikiliza Mkurugenzi wa Mgodi wa Rak Caolin ,Adam Nyimbu akieleza namna mgodi wake unavyofanya shughuli za uchimbaji katika eneo hilo.
Kamishna wa Madini Kanda ya Pwani akitoa Maelezo kwa Kamishana wa Madini namna Migodi ya Kaolin inavyoendeshwa.
Naibu Waziri wa Madini , Dotto Biteko akitoa Maelekezo kwa Mmoja wa Wawekezaji kutoka Twyford, Andy He mara baada ya kutembelea eneo la Mgodi wa kaolini Wilaya ya Kisarawe na kumkuta muwekezaji huyo ambaye ni mnunuzi.
Naibu Waziri wa Madini , Dotto Biteko akiwa katika eneo la mgodi wa Rak Caolin Mining Wilaya ya Kisarawe.
Naibu Waziri wa Madini , Dotto Biteko akiwa katika eneo la mgodi wa Madini ya Kaolini Wilaya ya Kisarawe.

No comments: