Wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Hospitali ya Rufaa ya Musoma wakiwa katika kaburi la Baba wa Taifa baada ya kumuombea leo ikiwa ni siku ya kumbikizi yake ambayo hufanyika Oktoba 14 kila mwaka.
Baadhi ya wananchi wakielekea katika eneo la kumuombea Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Kijiji cha Mwitongo mkoani Mara.
Baadhi ya wataalam wa Hospitali ya Rufaa Musoma na Muhimbili wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuelekea kwenye nyumba ambako Baba wa Taifa alikuwa akipumzika enzi za uhai wake na wakati mwingine kukutana na wageni wake.
Dkt. Brighton Mushengezi akiwa katika Makumbusho ya Hayati Mwalimu Nyerere yaliopo kwenye Kijiji cha Mwitongo, Butihama mkoani Mara.
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye maadhimisho hayo leo.
Wataalam wakiwa katika sebule ambako Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa akipumzika na Mama Nyerere.
Pichani ni Jengo la Makumbusho ya Hayati Mwalimu Nyerere.
………………………..
Wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) walioko Hospitali ya Rufaa Musoma mkoani Mara wameungana na Watanzania kuazimisha kumbukizi ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Butihama mkoani hapa.
Wataalam hao leo wametembelea Kijiji cha Mwitongo ambako Mwalimu Nyerere amehifadhiwa na kupatiwa maelezo mbalimbali kuhusu histoaria yake. Katika maadhimisho hayo wananchi mbalimbali wamejitokeza wakiwamo wanafunzi, watalam wa afya Muhimbili na kufanyika kwa ibaada ya kumuombea Baba wa Taifa.
Baada ya wataalam hao kushiriki kwenye kumbukizi ya Hayati Mwalimu Nyerere leo, kesho Jumatatu (tarehe 15, 2018) wanaendelea kutoa huduma mbalimbali matibabu kwa wakazi wa mkoa huo na mikoa ya jirani kwa njia ya mkoba pamoja na kujenga uwezo kwa wataalamu wa Hospitali ya Rufaa ya Musoma.
Mwalimu Nyerere alifariki dunia Oktoba 14, mwaka 1999 katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas nchini Uingereza ambako alikwenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Madaktari walieleza kwamba kifo chake kilisababishwa na ugonjwa wa saratani ya damu.
Oktoba 14 kila mwaka imefanywa kuwa siku maalam ya kitaifa ili kutoa nafasi ya kumkumbuka na kutafakari mema na mazuri aliyoyafanya enzi za uhai wake.
No comments:
Post a Comment