Thursday, October 11, 2018

MRADI WA HAKI YETU WAZUNGUMZA NA VYOMBO VYA DOLA KIGOMA KUHUSU ULINZI WA WATU WENYE UALBINO.

Baadhi ya watendaji kutoka idara za Mahakama, Polisi na viongozi wa vijiji, kata na mitaa kwenye halmashauri ya mji Kasulu mkoani Kigoma wahimiza umuhimu wa kuimarisha ulinzi ili kupunguza madhila kwa watu wenye ualbino, sambamba na kuelimisha jamii zaidi kuhusiana na masuala ya ualbino ili kuondoa dhana potofu, dhidi ya watu wenye ualbino ambayo imejangeka miongoni mwa baadhi ya wananchi.

Pia jamii kukumbushwa kuhusiana na maadili mema, sambamba na kuhakikisha watendaji hao wanazingatia maadili yao ya kazi katika kuwahudumia wananchi.

Maazimio hayo yamefikiwa baada ya watendaji hao kupatiwa elimu kuhusu ualbino, maadili na amani, iliyotolewa na mashirika ya CEFA Tanzania, GNRC Tanzania na Under The Same Sun, ambayo kwa pamoja yanatekeleza mradi wa Haki Yetu.
 Faustine Gwassa, Naibu Meneja wa Mradi wa Haki Yetu akichokoza mada wakati wa mafunzo kwa baadhi ya watendaji wa kata, maafisa kutoka idara ya Mahakama na Polisi kwenye halmashauri ya mji Kasulu,mkoani Kigoma.

 John Richard, Afisa Mawasiliano wa Mradi wa Haki Yetu, akizungumza na baadhi ya watendaji wa kata, maafisa kutoka idara ya Mahakama na Polisi kwenye halmashauri ya mji Kasulu, mkoani Kigoma kuhusiana na utekelezaji wa mradi wa Haki Yetu.
Joyce Mdachi, kutoka shirika la GNRC akifundisha umuhimu wa maadili na amani kwa baadhi ya watendaji kata, maafisa kutoka idara ya Mahakama na Polisi kwenye halmashauri ya mji Kasulu, mkoai Kigoma.

No comments: