Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akifungua semina ya uraghibishaji na uhamasishaji wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa viongozi wa mkoa na Wilaya kwenye ukumbi wa halmashauri wa Benjamin Mkapa Jijini Mbeya.Kulia ni Ofisa mpango toka Wizara ya Afya Osca Kaitaba na mwisho ni Mkuu wa Wilaya ya Kyela Bi.Claudia Kitta.
Ofisa Mpango toka Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Osca Kaitaba akifafanua jambo kwenye mkutano huo
Na.WAMJW,Mbeya
Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yameleta mahangaiko pamoja na athari kwa jamii wa Mkoa wa mbeya ikiwepo ulemavu
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa MbeyaSerikali Mkoani Mbeya imesema kuwa nchi zilizo katika Ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo zinakabiliwa na tatizo la magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele zimeathiri sehemu kubwa ya jamii Mkoani hapa na kuleta mahangaiko kwa wananchi pamoja na ulemavu.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila wakati wa ufunguzi wa semina ya uraghibishaji na uhamasishaji wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa viongozi wa Serikali wa Mkoa na wilaya mkoani hapa.Alisema Magonjwa hayo yamekuwa yakiathiri zaidi wananchi na kiasi kikubwa yakipunguza uwezo wa wananchi katika shughuli za uzalishaji na ujenzi wa Taifa.
“Magonjwa haya, pamoja na kusababisha usumbufu mkubwa kwa waathirika pia yanaongeza matumizi ya rasilimali chache tulizonazo katika kuyakabili “alisema Mkuu huyo mkoa.
Aidha,Chalamila alisema kwamba uwepo wa magonjwa hayo umefanya watoto kutokuwa na mahudhurio mazuri mashuleni kutokana na muda mwingi kuwa wanaumwa.Hata hivyo alisema kuwa jambo la kutia moyo ni kwamba Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau wamekuwa wakitoa Kingatiba za kukinga magonjwa haya katika mkoa wa Mbeya.
“Hii ni kutokana na lengo la Serikali ya awamu ya tano ambalo ni kudhibiti magonjwa haya na hivyo kupunguza gharama kwa wananchi kwa kugawa kingatiba hizo”Alisisitiza Chalamila
Akielezea zaidi Chalamila alisema Mkoa wa Mbeya walikuwa wanakabiliwa na magonjwa yote matano ambayo ni minyoo ya tumbo kichocho, matende na mabusha katika wilaya zote ila kwakuwa na usimamizi na uhamasishaji nzuri mkoa wake hivi sasa wamepunguza magonjwa hayo na hivyo kuwataka viongozi wa mkoa na Wilaya zake kuzidi kuhamasisha na kuelimisha zaidi wananchi kujitokeza kumeze kingatiba ili kutokomeza magonjwa hayo.
Alisema kwa upande wa ugonjwa wa Trakoma kwa wilaya za Kyela, Chunya na mbarali, ugonjwa wa usubi upo kwa wilaya za rungwe, Kyela na busokelo.Kwa upande wake ofisa mpango kutoka Mpango wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele Wizara ya Afya Oscar Kaitaba alisema semina hiyo imejumuisha wajumbe kutoka halmashauri tatu za mkoa wa Mbeya ambazo ni Rungwe, Kyela, Busokelo.Aidha Kaitaba alitaja wajumbe hao kuwa wakuu wa wilaya, wakurugenzi,waweka hazina wa Wilaya, waganga wakuu waratibu pamoja na maafisa usalama wa wilaya
No comments:
Post a Comment