Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Mkoani Tanga,Omari
Mwanga akizungumza wakati wa ghafla ya uzinduzi wa kambi ya Vijana wa
chama hicho kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya
Muheza ambapo mgeni rasmi Mbunge wa Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu
alisema ushirikiano uliofanywa na vijana hao wa kushiriki katika mradi
mkubwa kama huo ni jambo la
kuigwa nchi nzima.
Katibu
wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Mkoa Tanga Zawadi
Nyambo akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alisema mpango kazi wa
miaka mitano 2017-2022 ambao uliwasilishwa katika Mkutano Mkuu wa UVCCM
Mkoa ukiwa na lengo la kuanzisha makambi katika ngazi mbalimbali.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Muheza Like Gugu akizungumza
kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu na Mwenyekiti wa
UVCCM mkoa wa Tanga Omari Mwanga kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza
Mhandisi Mwanasha Tumbo
Mbunge
wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katikati akimsikiliza Mkuu
wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto kulia ni Mwenyekiti
wa UVCCM mkoani Tanga Omari Mwanga
MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu
akivalisha taji mara baada ya kuwasili kwenye kambi hiyo ya vijana
MBUNGE
wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katikati akimaliza kukagua
gwaride la vijana mara baada ya kuwasili eneo la mradi wa ujenzi wa
Hospitali ya wilaya ya Muheza Lusanga kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM
Mkoani Tanga Omari Mwanga
MBUNGE
wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katikati akimsikiliza kwa
umakini Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu
MBUNGE
wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katikati akiwa na
Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Tanga kulia Omari Mwanga wakiangalia lori
lililoleta saruji kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa hospitali ya
wilaya ya Muheza inayojengwa eneo la Lusanga
MBUNGE
wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katika akiwa na Mwenyekiti
wa UVCCM mkoani Tanga Omari Mwanga wakipiga makofi wakati vijana
wakiimba nyimbo mbalimbali
UJENZI wa Hospitali ya wilaya ya Muheza mkoani Tanga umeanza kushika
kasi baada ya vijana 300 wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi
(UVCCM) Mkoani Tanga kuungana kwa pamoja kuweka kambi maalumu kwa ajili
ya kujitolea kwenye mradi huo.
Vijana hao wa UVCCM Mkoani Tanga kutoka wilaya zote walianza kambi hiyo
Septemba 10 mwaka huu eneo la Lusanga kunapojengwa hospitali hiyo
walianza kujitolea na wataalamu katika utekelezaji wa mradi huo kwa
awamu ya kwanza kujenga majengo ya utawala,wodi ya wanawake,wodi ya
watoto,jengo la maabara,jengo la utakasaji vifaa na jengo la dharura
ambayo yatagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 3.
Akizungumza katika ghafla ya uzinduzi wa kambi hiyo mgeni rasmi Mbunge
wa Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu alisema ushirikiano uliofanywa na
vijana hao wa kushiriki katika mradi mkubwa kama huo ni jambo la kuigwa
nchi nzima.
Balozi Adadi alisema ipo miradi mingi ambayo inaendelea kutekelezwa
katika Halmashauri mbalimbali na ikiwa watawatumia vijana hao wa chama
ni wazi wanaweza kujengwa kiuzalendo zaidi na kusaidia
kuharikishautekelezaji wake.
Alisema atahakikisha vijana hao wanapatiwa vifaa muhimu vya
kujikingapindi wawapo katika shughuli hiyo ya ujenzi na wanapatiwa
chakula chakutosha na mahitaji mengine muhimu ili azma yao ya
kuyafikisha majengo hayo uwasa wa lenta Sept 25 iweze kutimia.
Kwa Upande wa Mkuu wa Wilaya Muheza Mhandisi Hajat Mwanasha Tumbo
alisema azimio ni kupata Hospitali ya wilaya hivyo waliona vijana
watumike ili kuwajengea uzalendo na kufanya hivyo Serikali inaweza
kufikia malengo yake.
Tumbo alisema jambo hilo liwe chachu kwa chama na Serikali kwenye azma
ya kutatua kero za wananchi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali
ambayo haitekelezwi kwa wakati na kusababisha wananchi kuendelea
kuteseka.
“Tunahaja ya kuwatumia vijana hawa sasa hasa katika miradi yetu ya
kimaendeleo na si kuwaacha tu na tukifanya hivi tutakuwa tunawajenga
kiuzalendo wa kujua chama chao na Serikali nini wanachokifanya kwa
ajili ya wananchi wake”Alisema Tumbo.
Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama hicho Mkoa Tanga
Zawadi Nyambo alisema mpango kazi wa miaka mitano 2017-2022 ambao
uliwasilishwa katika Mkutano Mkuu wa UVCCM Mkoa ukiwa na lengo la
kuanzisha makambi katika ngazi mbalimbali.
Nyambo alisema nguvu itakayotumika kupitia vijana hao ipo imani kubwa ya
kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kitatumika katika shughuli
zingine za maendeleo ya kijamii na kuieleza jamii umoja wa vijana hao
sio siasa pekee bali ni pamoja na ujenzi wa Taifa.
Katibu huyo alisema wameazimia kuwatumia vijana kuwajenga katika suala
zima la uzalendo kama nguvu kazi katika miradi mbalimbali inayoanzishwa
na Serikali”Alisema.
Awali akisoma taarifa fupi mbele ya mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa
Wilaya Juliaus Mgeni alisema Wilaya hiyo tangu ianzishwe miaka 45
iliyopita haina Hospitali ya Wilaya na kuitegemea Hospitali 1 ya Teule
inayomilikiwa na Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga.
Alisema Hospitali inazidiwa uwezo kwa sasa mabpo uwezo wake ni
kuhudiumia watu 1,500 kwa siku hivyo huduma za rufaa ikijumuisha
wagonjwa wenye hali mbaya za kiafya toka vituo vya huduma za msingi
wanalazimka kusafirihwa umbali wa km 72 hadi Hospitali ya Rufaa ya
Bombo Mkoani Tanga.
Mgeni alisema Hospitali hiyo inatarajiwa kugharimu kiasi cha zaidi ya
shili bilini 11 hadi kumalizika kwake ambapo unategemewa kutekelezwa kwa
kipindi cha mika mitatu kuanzia 2017/18 -2019/2020 na itategemea
upatikanaji wa fedha
No comments:
Post a Comment