Waziri wa Madini Angellah Kairuki (katikati) akitembelea maeneo
mbalimbali katika kiwanda cha Kuchakata Madini ya Graphite cha
GodMwanga Gems Ltd. Wa kwanza kulia ni Mmiliki wa kiwanda hicho
Godlisten Mwanga na wa kwanza kuli kwa waziri ni Kaimu Mkuu wa Wilaya
ya Simanjiro, Tumaini Magesa.
Mmiliki wa kampuni ya God Mwanga Gems Ltd.Godlisten (kulia) Mwanga
akimwonesha Waziri wa Madini Angellah Kairuki madini ya Grahite ambayo
tayari yamechakatwa.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki (katikati) akipita katika maeneo
mbalimbali ya kiwanda cha God Mwanga Gems Ltd kuona namna shughuli
mbalimbali za uchakataji wa madini ya Kinywe zinavyofanyika.
Na Asteria Muhozya, Simanjiro
Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema anaona fahari kutokana na
uwekezaji wa Kiwanda cha Kuchakata madini ya Kinywe (Graphite)
uliofanywa na Kampuni ya wazawa ya GOD Mwanga Gems Ltd iliyopo
Kata ya Endiamtu, Wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara.
Waziri Kairuki ameyasema hayo leo tarehe 2 Agosti, alipotembelea
kiwanda hicho kwa lengo la kujionea shughuli zinazofanywa na kiwandani
hapo.
Amesema Serikali imekuwa ikihamasisha waombaji wa leseni za madini
kuwekeza katika maeneo mbalimbali hivyo, jambo lililofanywa na kiwanda
hicho ikiwemo malengo ya kiwanda husika kufungua viwanda vingine
katika mikoa ya Tanga na Manyara ni jambo la kujivunia na fahari kwa
Tanzania.
“Nimefurahishwa sana namna kampuni hii inavyofanya kazi. Serikali kupitia
wizara yangu imekuwa ikihamasisha uwekezaji. Tuko tayari kuwasimamia
na kuwasaidia katika hili. Tunataka kutengeneza ajira zaidi, kukuza uchumi
kupitia madini lakini pia serikali kupata kodi,” amesisitiza Kairuki.
Akijibu ombi la kampuni hiyo kupata kibali cha kuuza madini hayo nje,
Waziri Kairuki ameahidi kampuni hiyo kuwa mara baada ya taratibu za
utoaji vibali kukamilika Wizara kupitia Tume ya Madini itatoa kibali kwa
kampuni husika iendelee na taratibu zake za kuuzwa nje ya nchi madini
hayo.
Kufuatia hali hiyo, Waziri Kairuki amewataka wenye leseni za madini
kutozitumia leseni hizo kuziweka rehani kwa kuwa Sheria ya Madini
inakataza jambo hilo badalayake zinatakiwa kutumiwa katika malengo
yaliyokusudiwa.
“Wapo baadhi ya wawekezaji wamepewa leseni lakini hawajafanya
chochote wengine wanaweka rehani leseni hizi. Nafurahi kuona mzawa
mwenzetu amefanya jambo kubwa kama hili, leo nimejionea uhalisia
katika jambo hili,” amesema Waziri Kairuki.
Pia, Waziri Kairuki ameishauri kampuni husika kuendelea kuitumia
Maabara ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti Tanzania (GST) kwa ajili ya
shughuli za utafiti na pia kuwatumia wahitimu wa Chuo Cha Madini
Dodoma (MRI) katika suala la ajira.
Katika hatua nyingine, Waziri Kairuki amesema Wizara imewachukulia
hatua watumishi 40 kutokana na kwenda kinyume na maadili ya utumishi
wa umma katika suala zima la usimamizi katika sekta husika.
“Wapo tuliowahamisha vituo vya kazi, wengine tumewasimamisha.
Tunachotaka ni kuendana na kasi na huku wakizingatia maadili ya
utumishi,” amesema Waziri Kairuki.
Aidha, amesisitiza suala la wawekezaji kuendelea kutoa taarifa za
uzalishaji ili serikali iweze kupata kodi zake huku akisisitiza suala la
ulipaji kodi kwa serikali na wenye leseni zao kuzitumia na kuzalisha kwa
viwango vinavyohitajika.
Kwa upande, Meneja wa Kiwanda hicho Henry Mbando ameiomba serikali
kukisaidia kiwanda hicho kupata kibali kwa ajili ya kuuza madini hayo nje
ya nchi ambayo yana masoko katika nchi za Marekani, Kanada, China na
ulaya.
Ameongeza kuwa, madini hayo yanatumika kutengeneza bidhaa
mbalimbali za viwandani vikiwemo vipuri vya magari, betri za magari na
mitambo mengine.
Ameongeza kuwa, soko la madini hayo ni katika nchi za
Akizungumzia idadi ya wafanyakazi waliopo kiwandani hapo amesema
kiwanda kina jumla ya watumishi 80 huku waanawake wakiwa 2 na
wanaume 78.
Naye, Mmiliki wa kampuni hiyo, Godlisten Mwanga ameishukuru Serikali
kwa msamaha wa kodi katika baadhi ya mitambo aliyoinunu kwa ajili ya
kiwanda hicho na pia kumshukuru waziri Kairuki kwa kuona umuhimu wa
kutembelea kiwanda husika.
Amesema kiwanda hicho kimezalisha tani zaidi ya 2,000 na zilizotayari kwa
ajili ya kuuzwa ni tani 200.
Akizungumzia suala la kibali kwa kampuni husika Kamishna wa Madini
Mhandisi David Mlabwa amesema kuwa, awali kampuni hiyo ilikuwa
haijakidhi vigezo vya kupata kibali lakini baada ya kukidhi viwango hivyo
itapatiwa kibali.
No comments:
Post a Comment