Wednesday, July 11, 2018

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola atembelea jeshi la Magereza

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola (Mb) akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika ziara yake ya kikazi ya siku moja ndani ya Jeshi hilo leo Julai 11,2018 jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola (Mb) akipokea salaam ya heshima kutoka kwa gadi maalum iliyoandaliwa kwa ajili yake ikiundwa na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola (Mb) akikagua gadi ya heshima iliyoandaliwa kwa ajili yake alipofanya ziara ya kikazi katika Jeshi la Magereza leo Julai 11,2018 jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola (Mb) akisalimiana na baadhi ya maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza mara baada ya kukagua gwaride maalum. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa na aliyeshikanaye  mkono ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Musa Kaswaka.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola (Mb) (katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwa Makao Makuu ya Jeshi hilo kabla ya kuendelea na ziara yake katika Kiwanda cha Seremala gereza Kuu Ukonga, Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji na baadaye kuongea na Maafisa na askari Bwalo Kuu la Maafisa Ukonga. Picha zote na Jeshi la Magereza.

No comments: