Thursday, July 5, 2018

WASHINDI WA KWANZA WA SHINDANO LA ‘TUSUA MAISHA NA GLOBAL’ WAZAWADIWA

WASHINDI wa Shindano la Tusua Maisha na Global, wamekabidhiwa zawadi zao leo katika ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.Washindi waliokabidhiwa zawadi ni Richard Tanganyika aliyejishindia pikipiki, Shaaban Kamoye aliyejishindia dinner set, Nasoro Juma aliyejishindia headphones za kisasa za Beats by Dre na Novart Magere aliyejishindia jezi, akiwa amewakilishwa na ndugu yake, Hassan Mathias.

“Najisikia furaha sana kuibuka mshindi wa pikipiki, naamini itanisaidia sana kwenye biashara yangu ya genge na mgahawa kwani mimi ni mfanyabiashara; nawasihi watu wengine pia washiriki kwenye hili shindano kwa sababu ni kweli zawadi zinatolewa bila upendeleo,” alisema Tanganyika baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya pikipiki.
Naye Shaaban Kamoye aliyejishindia dinner set, amesema zawadi hiyo ataenda kumpa mama yake kwani yeye ndiye aliyenunua Gazeti la Amani lakini yeye (Shaaban) akaamua kujaribu bahati yake na kuibuka mshindi.
“Mimi ni mpenzi wa gazeti la Championi lakini mama ndiye aliyenunua gazeti la Amani ambalo kuponi yake ndiyo iliyoleta hii zawadi, namshukuru sana Mungu kwa hii zawadi na nitamkabidhi zawadi mama kwani japokuwa mimi ndiye niliyeshiriki, lakini yeye ndiye aliyenunua gazeti.
Namna ya kushiriki kwenye shindano hilo; nunua gazeti lolote linalochapishwa na Global Publishers, kati ya Uwazi, Amani, Ijumaa, Risasi, Ijumaa Wikienda, Championi na Sport Xtra, fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya namna ya kushiriki, jaza kuponi hiyo kisha chukua simu yako, fungua uwanja wa meseji na uitume namba maalum iliyopo kwenye kuponi kwenda namba 0719 386 533.
Ukituma meseji utakuwa umeingia moja kwa moja kwenye shindano na endapo ukibahatika kuibuka mshindi, utapigiwa simu na kupewa maelekezo ya namna ya kushiriki.“Nawasihi wasomaji wetu washiriki kwa wingi kwani kuna zawadi kibao, kila wiki pikipiki moja itakuwa inatolewa na zawadi nyingine kemkem,” alisema Antony Adam, Mkuu wa Idara ya Usambazaji na Masoko ya Global Publishers.
Mhariri wa magazeti ya Global Publishers, Aziz Hashim (katikati) akizungumza na washindi (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kuwakabidhi zawadi leo katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Usambazaji, Keffa Massaga, na kulia ni Meneja wa Masoko wa Global Publishers, Anthony Adam.
Mwakilishi wa SokaBet, John Joseph, akiongea na washindi (hawapo pichani).
John Joseph akimkabidhi jezi Hassan Mathias (kushoto) ambaye ni mwakilishi wa mshindi wa jezi, Novati Magere.
Meneja wa Masoko wa Global Publishers, Anthony Adam (kulia) akimkabidhi zawadi mshindi wa head phones, Nasoro Juma.
Ofisa Usambazaji, Jimmy Haroub (kulia) akimkabidhi mshindi wa Dinner Set, Shaban Kamoge.
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja.
Ofisa Usambazaji, Keffa Massaga (kushoto) akimkabidhi funguo mshindi wa pikipiki, Richard Tanganyika.
PICHA: RICHARD BUKOS | GPL

No comments: