Monday, July 23, 2018

RAIS MAGUFULI APOKEA GAWIO LA SH.BILIONI 723 KUTOKA KWA KAMPUNI NA MASHIRIKA

*Atoa maagizo kuhakikisha gawio linaendelea kuongezeka 
*Awaambia Serikali yake haipendi shirika bali inapenda pesa 
*Wasiotoa gawio awataka waone aibu, kisha wajitathamini 

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 

RAIS Dk.John Magufuli amepokea gawio la Sh.bilioni 723 kutoka kwa kampuni na taasisi mbalimbali huku akieleza wale ambao hawajawahi kutoa gawio menejimenti yake ijitathimini na ione aibu. 

Pia amesema kutokana na uwekezaji mkubwa ambao Serikali umeufanya bado gawio hilo halitoshi na hivyo ameomba mamlaka husika kuhakikisha zinasimamia kampuni na mashirika hayo ili kuongeza gawio kwa serikali. 

Kampuni mbalimbali ikiwamo Kampuni ya mafuta Puma Energy ambayo nayo nimiongoni mwa walitoa gawio kwa kuipa Sh.bilioni 9.Utoaji huo wa Gawio umefanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo Rais Magufuli amepongeza kampuni na taasisi zote ambazo zimetoa gawio nakueleza kwamba kuna baadhi ya kampuni tangu nchi kupata uhuru hazijawahi kutoa gawio. 
“Tukio la kupokea fedha hizi za gawio Sh.bilioni 723 ni tukio muhimu katika nchi yetu kwani fedha hizi ndizo ambazo zinatumika kufanya maendeleo,”amesema Rais Magufuli na kuongeza Serikali haipendi shirika bali inapenda fedha, hivyo ambao hawajatoa na wenyewe watoe. 

Pia amefafanua duniani kote kuna njia mbili za kupata mapato, njia ya kwanza ni kwa makusanyako ya kodi na njia ya pili ni ile ambayo haitokani na makusanyo ya kodi ikiwamo hiyo ya gawio. “Kwa njia moja au nyingine Serikali imejitahidi kuimarisha ukusanyaji wa kodi ambapo Mwaka wa fedha wa 2016/2017 wamekusanya Sh.Trilion 15.5 . 

“Wananchi kutokana na mambo ya maendeleo yanayofanyika wamehamasika katika kulipa kodi na ndio maana makusanyo yameongezeka,”amesema Rais Magufuli. Wakati huohuo amesema kuna mashirika zaidi ya 90 yanayostahili kutoa gawio kwa Serikali lakini kampuni ambazo zimetoa ni 47 tu.Amesema mwaka 2016 mashirika 25 yalitoa gawio na hata hivyo gawio hilo halikuridhisha Serikali. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya TIPER Profesa Abdulkarim Mruma  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi cheti maalumu kwa wachangiaji waliovuka malengo kwa  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Bw. Allan Kijazi  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa  Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Bonde la Ngorongoro Profesa Abiud Lucas Kaswamila akiwa a Mhifadhi Mkuu wa  Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Dkt. Freddy Manongi  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akikabidhi Cheti cha kutambua kuvuka malengo ya gawio  kwa  Mwenyekiti wa Bodi Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA)  Dkt. Jonas Kilimbe akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kulaba  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Irene Isaka, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Bw. Edwin Rutageruka.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mfuko wa Misitu Tanzania akiwa na Katibu Dkt. Tuli Salum Msuya  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na (EWURA) Maji Profesa Jamidu Kamika akiwa na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa  EWURA Bw. Nzinyangwa Mchani  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekliti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Profesa Rutasitara akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Balozi Ben Moses akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa TFDA Bi. Agnes Kijo   katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Shirika la Viwango (TBS)  Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko akiwa na  Mkuruigenzi wa TBS Profesa Egird Mubofu  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari  Profesa Ignas Rubaratuka aliye pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi Deusdedit Kakoko  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu wakipata picha ta pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumua ya Bunge ya Uwekezaji wa Mtaji wa Umma baada ya kupokea magawio kutoka katika taasisi, mashirika na Makampuni ya Umma katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018. Picha na IKULU

No comments: