Na Francis Godwin, MichuziBlog Iringa
MFUKO wa hifadhi ya jamii (NSSF) umetoa msaada wa mashuka 300 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 4.5 kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na halmashauri ya Iringa mkoani Iringa kwa ajili ya kusaidia hospitali ,zahanati na vituo vya afya vyenye upungufu wa mashuka ya wagonjwa.
Akikabidhi msaada huo leo meneja wa NSSF mkoa wa Iringa Josephat Komba alisema kuwa NSSF imetoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maombi yaliyotolewa na Halmashauri hizo kwa NSSF kuomba kusaidiwa msaada wa mashuka.
Komba alisema kuwa NSSF kama mfuko wa hifadhi ya jamii unayojukumu la kuendelea kuunga mkono jitihada za Halmashauri nchini katika kutoa huduma za afya na pia unaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli kuona sekta ya afya inaendelea kuboreshwa zaidi.
Kwani alisema NSSF pamoja na majukumu mengine itaendelea kuwa karibu na jamii ya kitanzania kwani hatua ya waajiri kuwaunganisha wafanyakazi wao na NSSF ni kutaka kuona maisha yao yanaendelea kuboreshwa zaidi hivyo jukumu lao kuona NSSF inaendelea kuunga mkono azima ya serikali katika uboreshaji wa huduma za afya.
Alisema kuwa NSSF ilipokea maombi kutoka katika Halmashauri ya Manispsaa ya Iringa na Halmashauri ya Iringa kuomba kusaidiwa msaada wa mashuka kwa ajili ya wagonjwa na pasipo kuchelewa wametimiza maombi hayo.
" NSSF imekuwa ikisaidia katika huduma mbali mbali za kijamii pamoja na kusaidia Halmashauri ila pia wamekuwa wakisaidia huduma ya matibabu kwa wanachama wake bure pamoja na familia zao ili mradi awe mwanachama wao ".
Alisema kuwa sehemu ya kuunga mkono kasi ya wanachama kujiunga nakuwekeza katika NSSF ni pamoja na NSSF kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Halmashauri katika uboreshaji wa Afya na wataendelea kufanya hivyo.
Komba alisema kuwa hospitali ya Manispaa ya Iringa Frelimo iliomba msaada wa mashuka 200 na halmashauri ya Iringa iliomba mashuka 100 na NSSF imetoa mashuka yote kama Halmashauri zilizoomba japo itaendelea kusaidia mahitahi mengine kulingana na maombi na upatikanaji wa pesa.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Omary Mkangama alipongeza msaada huo wa NSSF katika Hospitali ya Frelimo na kuomba ushirikiano huo kuendelea zaidi .
Alisema kuwa Hospitali hiyo imekuwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ya mashuka ambayo imetatuliwa na NSSF na ile ya mashine ya kufulia nguo na chumba cha kufulia nguo iliyotekelezwa na CCM wilaya ya Iringa mjini.
kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya Frelimo Dr Benjamin Mhanga alisema kuwa Hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ya upungufu wa majengo kama la kulaza wagonjwa akina mama ,watoto ,magonjwa ya kuambukiza ,chumba cha kuhifadhia maiti na jengo la wanawake pamoja na vifaa tiba.
Huku kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya mbali ya kupngeza NSSF kwa kusaidia msaada wa mashuka bado alisema Halmashauri hiyo inahitaji mashuka zaidi pamoja na vitanda kwa ajili ya vituo vya afya ,zahanati na Hospitali ya wilaya na kuwa zaidi ya mashuka .
Kuwa kuna vituo vya afya 10 ,Hospitali teuli moja na zahanati ambapo hitahji zima ni shuka zaidi ya 1560 zinahitajika hivyo msaada huo wa shuka 100 umepunguza sehemu ya hitaji ya changamoto hiyo.
Hivyo alisema kupitia mbunge wa jimbo la Ismani Wiliam Lukuvi wameendelea kutafuta wahisani kwa ajili ya kutatua tatizo hilo kwa kutafuta wadau wakiwemo NSSF ambao wamejitolea msaada huo wa mashuka ambayo yatakwenda Kalenga na jimbo la Isimani .
Meneja wa NSSF mkoa wa Iringa Josephat Komba(kushoto) akimkabidhi msaada wa shuka 200 kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Omary Mkangama kwa ajili ya Hospitali ya Frelimo
Wafanyakazi wa hospitali ya Frelimo wakitandika mashuka yaliyotolewa na NSSF
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa Robert Masunya (kulia ) akishukuru kwa msaada wa NSSF
Meneja wa NSSF mkoa wa Iringa Josephat Komba akielezea msaada wa uliotolewa na NSSF katika Halmashauri za Iringa
Mashuka yaliyotolewa na NSSF
Wafanyakazi wa hospitali ya Frelimo wakifuatilia tukio hilo
Meneja wa NSSF mkoa wa Iringa Josephat Komba (kushoto ) akimkabidhi msaada wa mashuka 100 mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa Robert Masunya. Picha na Francis Godwin, Michuzi Blog, Iringa
No comments:
Post a Comment