Friday, July 6, 2018

Kampuni ya Asas Dairies Ltd yakabidhi kituo cha Afya mkoani Njombe

 Kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Ltd leo imekabidhi kituo cha Afya kwa wananchi wa Kijiji cha Lulanzi kilichopo katika wilaya ya Wanging'ombe mkoani njombe, katika tukio hilo lililo hudhuriwa na mkuu wa mkoa wa njombe Mh Christopher Olonyokie Ole-Sendeka ambaye alikuwa mgeni Rasmi.
Ujenzi wa kituo hicho cha afya Umeshirikisha nguvu ya wananchi huku kampuni ya Asas ikichangia zaidi ya milioni mia moja pamoja na vifaa tiba ikiwemo Vitanda kumi vya kisasa pamoja na mablanketi kwa kila kitanda kwaajili ya wagonjwa, kitanda maalumu kwaajili ya wamama kujifungulia , jokofu maalumu la kuhifadhia dawa pamoja na chanjo lenye uwezo wa kutumia umeme na gesi.
Wakizungumza kwa furaha sana wakazi wa kikjiji cha lulanzi wameishukuru kampuni ya Asas kwa msaada huo "Tunashukuru wadau hawa kwa ujenzi wa hii zahanati kwaku a tulikuwa tukitembea kwa umbali mrefu kwenda kibena kufuata huduma ya afya ila sasa tunaipata uwanjani kwetu wakati mwingine wamama walikuwa wanajifungulia njiani" amesema mmoja wa wanakijiji aliye jitambulisha kwa jina la Upendo Wikunge.
Akizungumza kwa furaha   mkuu wa mkoa wa njombe Mh Ole-Sendeka  ameseama kwanza amewapongeza wanakijiji wa Lulanzi kwa juhudi zao  "Waswahili wanasema ukiona cha elea ujue kimeundwa kwanza niwapongeze kampuni ya Asas kwa moyo huo nimeguswa sana na juhudi hizi za wanakijiji nimeangalia vifaa hivi vya Kisasa na hili jengo basi nakosa cha kusema ila niwashukuru sana kwa moyo huu na muendelee hivi tunajua mmeweka pesa nyingi sana hapa zaidi ya milioni mia moja katika mradi huu niwapongeze sana".
Baada ya kukabidhi zahanati hiyo ya kisasa kwa mkuu wa mkoa ikafika zamu ya mkurugenzi wa Asas kuzungumza "Mh mgeni rasmi sisi kama Asas tumeamua kufanya hivi ili kuunga mkono jitihada za serikali yetu katika kuboresha huduma za afya na afya kwa wananchi wake tunafahamu usumbufu wanao upata mama zetu na watoto wanapo tembea umbali mrefu kufuata huduma za afya hivyo basi tukaona tuwasogezee jirani hapa, tunatamani siku moja tusikie hakuna vifo kwa mama na mtoto na mwisho kabisa tutatoa na Kompyuta mbili katika zahanati hii ili zikawasaidie kutunza kumbu kumbu zao" amesema ndugu Fuad Abri.
No comments: