Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi
na viongozi wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO)
wakati wa ziara ya kujitambulisha mapema leo ofisi za DAWASCO. Picha
zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam
(DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja alitoa maelekezo machache wakati wa
ziara ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa ofisi za
DAWASCO mapema leo alipofanya ziara ya kujitambulisha.
Wafanyakazi
wa DAWASCO wakifuatilia maelezo ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la
Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian
Luhemeja.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa akipokelewa na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam
(DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati akipokelewa ofisi za DAWASCO
mapema leo alipofanya ziara ya kujitambulisha.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa akiagana na wafanyakazi wa
Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO) wakati wa ziara
ya kujitambulisha mapema leo ofisi za DAWASCO.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam
(DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya ziara ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Makame
Mbarawa.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Waziri
wa Maji na umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa ameliagiza Shirika la Maji
Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASCO) kuhakikisha linabadili mfumo
wa mita zinazotumika sasa kuhamia kwenye mfumo wa kieletroniki ambao
utawafanya wateja wake walipe kabla ya kutumia hatua ambayo itasaidia
katika ukusanyaji wa mapato na kudhibiti upotevu wa mapato.
Maagizo
hayo ameyatoa mapema leo Julai 4, 2018 alipotembelea shirika hilo mara
baada ya kuteuliwa mwishoni mwa wiki kuingia kwenye wizara ambapo
amesema awali aliwahi kuteuliwa lakini alikaa muda mfupi ambapo aliacha
maagizo kadhaa ikiwemo hilo la mita ambalo kwa sasa amewataka walitilie
mkazo.
Amesema
kuwa malengo ya wizara yake kuwa ni kuwafikishia wananchi wanyonge
huduma ambayo ni muhimu na hivyo amewataka watendaji wa DAWASCO kutoka
na kwenda kushughulikia kero za wananchi na kuhakikisha zinatatuliwa kwa
wakati.
"Nawaomba tufanye kazi kwa uadilifu na kuacha kuwanyanyasa wananchi kwa
kuwapelekea bili zisizoeleweka kabisa maana hizi mita za zamani
zinapoteza maji na vile vile fedha ya shirika,"
Amesema
Prof. Mbarawa.
Aidha ameongeza suala la wafanyakazi kuingia mikataba ya kiutendaji
ambayo anaamini endapo itafuatwa itaweza kubadilisha sura ya shirika
hilo huku akiigiza bodi ya wakurugenzi kuhakikisha inaongeza wateja
kutoka 290,000 waliopo sasa hadi kufikia 850,000 kwa mwaka hatua ambayo
itaongeza mapato zaidi ya mara tatu lakini pia amesema suala la upotevu
wa maji lipewe kipaumbele ili kudhibiti fedha nyingi zinazopotea kupitia
upotevu huo.
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja
amesema kwa sasa DAWASCO ina mipango mingi ambayo inakwenda kutekelezwa
na ndiyo maana ameamua kuingia mikataba na watumishi wa shirika hilo ili
kufikai malengo hayo kwa urahisi huku likiendelea kubuni mbinu
mbalimbali za kukabiliana na changamaoto zinazojitokeza ikiwemo upotevu
wa maji ambapo mita 155 zitabadilishwa ambazo zilikuwa chakavu.
No comments:
Post a Comment