Sunday, July 22, 2018

CCM YAKABIDHI GARI LA KUBEBA WAGONJWA KWA WANANCHI LENG'ATA

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimekabidhi gari la kubeba wagonjwa katika Kata ya Leng'ata wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Kukabidhiwa kwa gari hiyo ni moja ya mkakati wa CCM wa kuendelea kutekeleza ahadi ya kuboresha na kusogeza huduam za afya karibu na wananchi kwa kufanikisha kupatikana kwa gari hiyo.

Gari hiyo imekebidhiwa jana katika kituo cha afya cha Kagongo ambapo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole ndio aliyekabidhi kwa niaba ya Rais John Magufuli ambaye ndiye aliyetoa gari hilo baada ya kupokea kilio cha wananchi kupitia Mbunge wa Jimbo la Mwanga Proesa Jumanne Maghembe

Akizungumza baada ya kukabidhi gari Polepole amesema Rais Magufuli anawapenda wananchi wote bila kubagua vyama vyao."Na CCM nayo inahimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 mpaka 2020 hata katika maeneo yanayoongozwa na upinzani ndio maana gari la kubebea wagonjwa limetolewa katika Kata yenye Diwani wa upinzani ili kuendeleza dhana ya CCM kuwa maendeleo yanayotolewa na Serikali ya CCM hayana chama,"amesema.

Wakati uo huo Polepole ametolea ufafanuzi wa masuala, changamoto na fursa za Serikali ya CCM kwa wananchi wa Wilaya ya Mwanga.Baadhi ya changamoto hizo ni upatikanaji wa mtandao wa simu, ambapo amesema Chama kimeahidi kufuatilia na kupatikana kwa mtandao wa simu katika maeneo ambayo yanayo changamoto hiyo ya mtandao wa simu ikiwepo Kata ya Lang’ata.

Katika masuala ya uvuvi katika Bwawa la Nyumba ya Mungu Polepole amesema napo Chama kimekemea vitendo vya baadhi ya kuwanyanyasa wananchi, kupokea rushwa na kutosimamia haki katika kudhibiti uvuvi haramu.

"Chama pia kimewataka wananchi nao kufuata utaratibu na kutii sheria katika matumizi ya Bwawa hilo kwa faida yao na vizazi vyao,"amefafanua Polepole.Aidha ameielekeza Halmashauri ya Mwanga kujenga maeneo maalumu ya kupokelea samaki ambapo Serikali itapata mapato na wananchi watafaida kibiashara na kiuchumi, Halmashauri itoe mikopo ya uwezeshaji kwa vijana na wanawake na itumie ulinzi shirikishi katika kukabiliana na uvuvi haramu katika Bwawa la nyumba ya Mungu.

Polepole amesema Chama chao kinahimiza haki na usawa,hivyo Halmashauri haiwezei utaka kukusanya fedha kwa wananchi bila kuweka fedha."Jengeni maeneo maalumu ya kupokelea samaki, mtapata mapato, mtawawezesha wananchi kiuchumi na kibiashara na wekeni utaratibu mzuri wa ulinzi shirikishi katika kupambana na uvuvi haramu kwenye Bwawa la nyumba ya Mungu," amesema Polepole

Polepole yupo katika ziara za kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM.


No comments: